TANZIA Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

Posted Date::10/25/2007
Rais Kikwete aongoza mamia kupokea mwili wa Salome Mbatia Dar
Na Salim Said, MUM
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete, jana aliongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuupokea mwili wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia aliyefariki kwa ajali ya gari iliyotokea juzi wilayani Njombe, Iringa.

Ndege ya serikali 5H-TGF iliyobeba mwili wa marehemu ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Zamani majira ya saa 7:45 mchana ikitokea Iringa.

Baada ya kuwasili uwanjani hapo mwili huo ulishushwa kutoka katika ndege hiyo na Mawaziri na Manaibu Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Daniel Nsanzugwanko na kusogezwa karibu na viongozi mbalimbali waliokuwa uwanjani hapo kuupokea akiwamo Rais Kikwete, Makamu wake Ali Mohamed Shein Waziri Mkuu Mkuu wa Edward Lowassa na viongozi mbalimbali na wananchi walisimama kwa dakika chache ikiwa ni ishara ya kutoa heshima zao.

Wengine ni Naibu Waziri wa Usalama wa Raia, Mohamed Aboud, Naibu wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ludovic Mwananzila, Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Gaudence Kayombo na Nibu Wziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera .

Wengine waliofika uwanjani hapo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), John Malecela, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abass Kandoro na Kamishina wa Kanda Maalumu Alfred Tibaigana.

Baada ya zoezi hilo mwili huo ulingizwa katika gari maalum la wagonjwa (ambulance) la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kupelekwa kwa msafara katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi, Andrew Chenge alisema mwili wa marehemu utapelekwa nyumbani kwake saa 1.30 asubuhi leo kwa ibaada ya maalumu ya kuuaga na wananchi kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho.

Hali katika uwanja wa ndege ilikuwa ya huzuni ambapo vilio na nyimbo za maombelezo kutoka kwa kikundi cha akina mama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zilitawala uwanjani hapo.

Kututoka Iringa, Hakimu Mwafongo, anaripoti kuwa mamia ya wananchi wa mkoa wa Iringa jana waliojitokeza kuuaga mwili wa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Wanawake, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia aliyefariki juzi katika ajali ya gari wilayani Njombe.

Hata hivyo, wengi wao hawakufanikiwa kuuga kutokana na muda kwuwa mfupi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Bernard Nzungu aliwaambia wananchi waliokuwa wamekusanyika nje ya nyumba ya kuhifadhi maiti katika hospitali ya Mkoa wa Iringa jambo hilo haliwezi kufanyika kutona na muda kutotosha.

Mwili wa marehemu na wa dereva wake Anakleti Mogella ambaye pia alikufa katika ajali hiyo ilisafirishwa kwa ndege kuelekea Dar es Salaam jana, majira ya saa 6:30 mchana.

Baadhi ya viongozi waliokuwa katika msafara huo ukiongozwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi, Selina Kombani ni pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Dk Lawrance Masha na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Emanuel Nchimbi.

Wengine waliokuja ni pamoja na mume wa marehemu, Dk Mbatia, mtoto wake wa kiume na baadhi ya wanafamilia wa waziri huyo.

Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania, aliyemuwakilisha Inspekta wa Polisi, Said Mwema,

Kamishna wa Polisi Pualo Chagonja alisema ajali zinazoendelea kutokea sehemu mbalimbali zinaendelea kuwakumbusha watumia barabara kuzingatia sheria za matumizi ya barabara.

Katika ajali hiyo, gari la Waziri huyo aina ya Nissan Patrol liligongana uso kwa uso na gari No T 299 AFJ Mitsubishi Fuso mali ya Jackson Kilagwa (30) wa Rujewa Mbeya.

Alisema pamoja na Naibu Waziri na dereva wake kufariki papo hapo, msaidizi wa dereva wa loli hilo, Castory Kilangwa pia alikufa papo hapo. Dereva wa lori hilo, anayedaiwa kuwa mkazi wa Makambako wilayani Njombe aliyenusurika katika ajali hiyo alitoroka baada ya ajali hiyo na Polisi limeahidi kumsaka mpaka apatikane.

Wengine waliokufa kwenye ajali hiyo Nicholaus Lubuva (33) Mkazi wa Mufindi na Dastun Gonze (26) ambaye ni mkulima wa Igowole wilayani Mufindi woliokuwemo katika lori hilo walijeruhiwa vibaya kwa kuvunjika miguu na mikono ambapo walipelekwa katika Hospitali ya Kibena Njombe.

Naye Tausi Mbowe anaripoti kuwa, Makao Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana yalikuwa katika hali ya utulivu tofauti na siku nyingine huku baadhi ya wanachama wa chama hicho wakionekana wenye huzuni kufuatia msiba huo.

Mwandishi alishuhudia baadhi ya wanachama hao wakiwa katika makundi makundi wakijadili juu ya msiba huo, huku wakionyesha huzuni kubwa.

Baadhi ya wanachama hao walionekana wakiwa wamevalia nguo nyeusi kuashiria hali ya maombolezo huku wengine wakiwa wamevalia nguo za rangi ya chama hicho.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM Taifa, Agrrey Mwanri alisema chama kimepoteza mtetezi wa wanyonge, mpiganaji, mwanamapinduzi na kiongozi mchapa kazi.

Mwanri alisema alikuwa karibu sana na Mama Mbatia na akaongeza kwamba chama kimepokea msiba huo kwa majozi makubwa

"Mbatia alikuwa mtetezi wa wanyonge mwanamapinduzi, kada, na mpenda maendeleo," alisema Mwanri.
 
Kuna ulazima gani kuvaa jezi za chama ambacho tena kinatawala, wana wasiwasi gani hadi kuwa na tabia za kiajabu ajabu. Sasa kumbe kiongozi akifariki tuwaachie wazike peke yao. Hii ni tabia mbaya ambayo inataka kuwagawa Watanzania na inastahili kukemewa kwa nguvu zote. Natumaini kusikia tamko rasmi kutoka CCM.
 
Hakuna ubaya wowote watu kuvaa mavazi ya vyama vyao kwenye matukio kama haya. Tusianze kukuza mambo basi na ulazima wowote after-all alifariki pamoja na kuwa ni waziri ifahamike pia ni mjumbe wa Halmashauri ya CCM na alishawahi kuwa Mjumbe wa kamati kuu ya CCM chombo cha juu kabisa na pia mweka hazina. Sioni tatizo hapo tusianze kupangiana hata namna ya kuvaa hii kila mtu yupo huru kuvaa atakavyo muradi havunji mipaka ya kisheria. Hapo ni sawa na kumlaumu shehe wa kiislam kuja na kanzu yake kwa kisingizio ni msiba wa kikristo.

Nimeshuhudia mazishi ya viongozi wa vyama upinzani wakizungushia jeneza bendera za vyama vyao kwangu mimi ni sawa tu, na ktk hili la mama Mbatia laiti asingekuwa waziri sanduku lingezungushiwa bendera ya CMM!
 
Nasubiria kusikia kama watamwagwa ffu kwenye mazishi ya huyu mwanaccm. Mlioko bongo mtwambie maana ule msiba wa kiongozi wa cuf musoma kulikuwa na ffu wa kumwaga kama vile walitaka kurudia mauaji ya mwembechai na pemba! nchi hii!
 
Kuna ulazima gani kuvaa jezi za chama ambacho tena kinatawala, wana wasiwasi gani hadi kuwa na tabia za kiajabu ajabu. Sasa kumbe kiongozi akifariki tuwaachie wazike peke yao. Hii ni tabia mbaya ambayo inataka kuwagawa Watanzania na inastahili kukemewa kwa nguvu zote. Natumaini kusikia tamko rasmi kutoka CCM.

Hakuna dhambi au kosa kuvaa jezi za chama, after all Mama Mbatia alikuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

Ni vitu vya kawaida askari kuvaa nguo za jeshi, masista kuvaa nguo zao na hata wanafunzi kuvaa ngua za shule wanazotoka wanapoenda kumzika au kumuaga mwenzao. Nashindwa kuelewa kwanini hiki kikukere? Pole sana.
 
Watu wa kuzua, kama kawaida. Just to put the record straight:-

- Mh Mbatia hakusafiri na dereva wake wa siku zote. Dereva alichelewa na yeye akaamua kumchukua kijana ambaye wamekuwa naye siku nyingi nyumbani na ambaye amejifunza gari pale nyumbani na kusafiri naye.

- Kutokana na dereva huyu, ambaye ni kama "house boy" pale nyumbani kutokuwa na uzoefu wa siku nyingi alikosa ajali nyingine kabla ya hiyo na basi. Dereva wa basi anasema dereva alionekana kutokuwa na uzoefu.

- Barabara ile ina lami nzuri sana na sio mashimo kama wengi wanavyodai.

- Ajali ilisababishwa na dereva wa lori kula roger (kuibia kwenye kona) na gari la Nissan lilikuwa na mwendo wa kasi na dereva asiyekuwa na uzoefu.

Nawaomba Watanzania wenzangu tuelekeze mawazo yetu kuipa familia rambirambi na kumzika dada yetu, mama yetu, rafiki yetu kwa pamoja.

Tukianza kuzua hatusaidii familia na Watanzania wote kwa ujumla.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi.
Bwana ametoa, bwana ametwaa.
 
nenda ukampuzike kwa salama mama mbatia, Tanzania itakukumbuka kwa yale mema ulioifanyia.

pole sana mzee Mbatia pamoja na wanafamilia, mola akupeni moyo wa subira na kuweza kuyashinda majaribu.

na mola asitufitinishe baaada yake
 
resize_imagefront.jpg
Rais Jakaya Kikwete, akigusa jeneza lenye mwili wa marehemu Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana. (Picha na Athumani Hamisi).
 
akaamua kumchukua kijana ambaye wamekuwa naye siku nyingi nyumbani na ambaye amejifunza gari pale nyumbani na kusafiri naye.

..mawazo ya kwamba dereva hakuwa na uwezo wa kutosha yalinijia pia.


Ajali ilisababishwa na dereva wa lori kula roger (kuibia kwenye kona) na gari la Nissan lilikuwa na mwendo wa kasi na dereva asiyekuwa na uzoefu.

..yalitokana na kujiuliza,alishindwa kumkwepa hata kuingia porini au pembeni[potelea mbali,lakini si sawa na head on]

..anyways,ndo hivyo,yakishamwagika!
 
Kuna ulazima gani kuvaa jezi za chama ambacho tena kinatawala, wana wasiwasi gani hadi kuwa na tabia za kiajabu ajabu. Sasa kumbe kiongozi akifariki tuwaachie wazike peke yao. Hii ni tabia mbaya ambayo inataka kuwagawa Watanzania na inastahili kukemewa kwa nguvu zote. Natumaini kusikia tamko rasmi kutoka CCM.

Huko mikoani kuna watu wanashindia hizi nguo za CCM. wengine wanalimia, wanaendea kwenye nyumba za ibada, kwenye sherehe,misiba n.k. Haina shida kuzikuta kwenye matukio kama haya.
 
Mkuuu Ole,

Heshima mbele kwa kutuletea live, huu msiba na hizo picha, hiyo ni moja ya tofauti kubwa kati ya hii forum na zingine,

Salute Kwa Hilo mkuu!

Kwa wana-familia ya huyu mama marehemu, kwa kweli ni masikitiko sana kuziangalia picha hizi, poleni sana wote ndugu wa familia.
 
m28mbi4.jpg


Viongozi wote wa juu walikuwepo uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar kuupokea mwili wa hayati Salome Mbatia ukitokea Iringa.


m24mwv5.jpg


m26mtb0.jpg


m25mux1.jpg


JK, waziri mkuu mh. EL na makamu wa rais Dr. Ali Mohamed Shein wakiwapa pole watoto wa hayati Salome Mbatia baada ya mwili wa mama yao kuwasili Dar leo kwa ndege toka Iringa.


m22myo1.jpg


m23mdw7.jpg


Waombolezaji toka kada mbalimbali walifika kuupokea mwili wa marehemu Salome Mbatia leo.


m27mvw9.jpg


Watoto wa marehemu Salome Mbatia wakisaidiwa kwenda kuupokea mwili wa mama yao leo Dar.


m29mje4.jpg


Jeneza lililobeba mwili wa hayati salome mbatia ukiwasili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar, leo, kufuatia ajali mbaya ya barabarani ambapo watu watatu walikufa papo hapo. habari toka Iringa zinasema dereva wa lori la fuso lililoigonga nissan ya hayati mbatia hakufa na aliyekufa ni utingo wake. yeye dereva ametoweka na hadi naingia mitamboni bado alikuwa hajulikani aliko.


m21mkf1.jpg


Msafara wa kwenda nyumbani kwa marehemu tayari kuanza.

Picha kwa hisani ya Michuzi blog
 
jamani kumbe zitto katoa msaada ili ajinufaishe kisiasa? mbona sumaye alikuwepo, mh mathayo na hatuwasikii, iweje iwe yeye tu?

msiba haupaswi kutumika kisiasa kujitoa namna hii.

ndiomaana akapiga mapicha na kumletea mzee Ole aonekane kafanyakazi, loooh hii hasara kubwa.

mapigano ya kifikra ! piga kote kote kuanzia magazetini, mtandaoni, kazini, vijiweni, hadi kwa wachambawima hiyo !
 
Huu ni msiba mkubwa kwa Taifa na familia ya marehemu. Pamoja na malumbano makali yaliyokuwa yanaendelea hapa ukumbini kuhusiana na hali halisi ya nchi yetu, nawaombeni huu msiba tuuheshimu na kusiwe na malumbano yoyoye kuhusiana na msiba huu. Tumwache huyu Mama akapumzike kwa amani.
 
Wakuu mi naomba kuuliza, Mwili wa dereva aka house boy haukuletwa na hiyo ndege? Kama ndio, mbona haitakuwa haki kuuacha mwili wa huyo kijana huko Iringa?

Sasa wewe bwana mbangaizaji kama mimi hapa, hukusikia kitu SUMAYE alichosema asubuhi kwenye kipindi cha nipashe? Namnukuu. "Madereva wanaowaendesha viongozi wanatakiwa wawe makini sana" Mwisho wa kunukuu. Wewe unayejiita mbangaizaji pamoja nami mbangaizaji mwenzio (wengi hupenda kuniita mkoku) ni kwamba tujifie tu!! Sisi ni halali yetu kufa bwana!! Na ndo maana hausiboi hakupakiwa na wala hatujui aliko. Sijui hata kama wanakazungumzia ka-hausiboi ka watu maskini ya Mungu. Sumaye ameshakuweka wazi hivyo usiulize ndugu yangu MBANGAIZAJI.
 
Back
Top Bottom