Waziri Nyanga afukuzwe SMZ

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
264
"Mishahara ya askari wa Kikosi cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM), kiasi cha Sh. milioni 92.2,lliibiwa katika Makao Makuu ya kikosi hicho, Kibweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar"

"Zaidi ya Sh. milioni 14 ikiwa ni mishahara ya askari wa Kikosi cha Kujenga Uchumi (JKU) imeibwa na watu wasiojuilikana kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo."

"Zaidi ya Sh. milioni 20 za mishahara ya ya askari wa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Zanzibar imeibwa"

Cha ajabu baada ya kuibiwa fedha zote hizi Walioshtakiwa walikuwa watu chini kabisa ambao wengi wao wamepoteza kazi. Huku wakuu wa vikosi hivyo na Wasaidizi wao ambao hata chunguzi za Polisi zilizofanyika walitakiwa wapelekwe mhakamani hawakuguswa na mpaka sasa wanakula raha na wanatumbua mapesa hayo. Jee kweli wizi huuu unaweza kufanywa na askari wa Chini kama hawa hasa ktk kambi zenye ulinzi mkali?.Waziri nyanga mwenyedhamana ya vikosi anawalinda wakubwa hao ,Nao CUF ndani ya barza la wawkilishi wako kimya hwalipiganii kelele jambo hili kwa kuwa halikutokea Mtambwe nao kwahiyo nao ni mafisadi wa siasa. Mh Bimani nae kwa hili ni fisadi wa mawazo?
 
Last edited by a moderator:
Waziri nyanga mwenyedhamana ya vikosi anawalinda CUF nao wako kimya nao ni mafisadi.

Kwanza karibu sana JF, naona hii ndio post yako yakwanza. CUF nao ni mafisadi kivipi?, manake hujaeleza Waziri anawalinda kwa ufisadi upi.
 
Kwanza karibu sana JF, naona hii ndio post yako yakwanza. CUF nao ni mafisadi kivipi?, manake hujaeleza Waziri anawalinda kwa ufisadi upi.

Huyu si mgeni hapa bwana Mfumwa!
Hawa si ndo walewale akina Surambili?
Akiona kaharibu kwenye thread moja , basi anaregister kwa jina lingine!

Kimsingi mada yake ni nzuri.
Kukamatwa mtu mdogo ndo kawaida jeshini mdogo wangu, kuapa kile kiapo ni pamoja na kukubali kuwa mbuzi wa sadaka at any time `t`.
Hata yule mjeshi aliyewekwa ndani kwa kumpiga Trafiki pale Ubungo ni mtu mdogo sana, wakati wakubwa wake walikuwepo na walisupport ishu yote!
 
Kwanza waziri Nyanga kapelekwa pale kupumzika baada ya kuonekana anawabania wakubwa mambo yao alipokuwa Wizara ya Fedha. Huyu jamaa musimuonee kabisa. Halafu CUF wanalindaje? Nadhani hapa ameteleza
 
Watu wengine cjui wanakuwa wamekunywa mataputapu ,mtu anakurupuka huko yaani ni maajabu yapo hapa JF ,Haya CUF wamekusikia na wanakwambia ili hayo yasitokee wachana na CCM .
 
CUF waseme marangapi?
Wakisema maovu ya viongozi wenu mnaanza kuwaandama wao. Sote tunakumbuka jinsi Mh. Mulla alivyo weka hadharani ufisadi wa Wizara ya Elimu unaopelekea matokeo mabovu ya mitihani ya kitaifa ya watoto wetu, matokeo yake Waziri Haroun Ali Suleiman akalia lia kwa Kificho(spika) aombwe radhi kakashifiwa, nini kilitokea?
Matokeo mengine mabovu ya mitiahani ya kidato cha 4&6 mwaka uliofuata.
Hakuna aliewajibika licha ya kelele na waziri Haroun anasema eti hata Wakati wa Maalim Seif alipokuwa waziri kulikuwa na matokeo mabovu mbona hakujiuzulu na wananchi wakamfurahia majibu yake pumba!
Mi naona wakati mwengine bora wajinyamazie tu "mabunju" wajionee wenyewe.
 
Hakika siasa za Zanzibar , tunazijua wenyewe tu. zimetawaliwa zaidi na siasa na wala sio maslahi ya nchi.

kama ilivyo katika Bunge la muungano linavyotawaliwa na UDINI
 
CUF waseme marangapi?
Wakisema maovu ya viongozi wenu mnaanza kuwaandama wao. Sote tunakumbuka jinsi Mh. Mulla alivyo weka hadharani ufisadi wa Wizara ya Elimu unaopelekea matokeo mabovu ya mitihani ya kitaifa ya watoto wetu, matokeo yake Waziri Haroun Ali Suleiman akalia lia kwa Kificho(spika) aombwe radhi kakashifiwa, nini kilitokea?
Matokeo mengine mabovu ya mitiahani ya kidato cha 4&6 mwaka uliofuata.
Hakuna aliewajibika licha ya kelele na waziri Haroun anasema eti hata Wakati wa Maalim Seif alipokuwa waziri kulikuwa na matokeo mabovu mbona hakujiuzulu na wananchi wakamfurahia majibu yake pumba!
Mi naona wakati mwengine bora wajinyamazie tu "mabunju" wajionee wenyewe.
Kama CUF iansema hawananyama mabunju wajionee wenyewe kwa hivyo siasa imewashinda wakauze kahawa. kazi ya siasa ni kuzungumzia kwa manufaa ya nchi. ikiwa miaka 15 angu cUF IANZISHWE ishanza kuchoka, miaka 50 itakuaje. au ndio imekosa madaraka na kazi basi?
 
Kama mabunju yana miba si afadhali wayaache yachomane weeeee!!! kwani CUF mara ngapi imepiga kelele za ufisadi na ubovu wa viongozi lakini Mibunju imelishwa nini sijuwi haitaki kuelewa au inafanywa isielewe. Saivi mambo yanaharibika wamebaki "...oooh lakini CUF wamesema ivyo..." wapi!! wapeni serikali muone kama itafika miaka 10 nchi ipo masikini tu!!! Miaka 50 ya mafisadi badala ya kuwaletea wananchi maendeleo wanaendelea wao na familia zao tu, wanatwambia "...nchi zote za ulimwengu wa tatu mambo ndo hivi hivi..." uwongo mtupu, mbona wao wanaishi maisha ya ulimwengu wa kwanza????
 
Cuf si inasema inashinda kila chaguzi, sasa inalalamika nini kama hawapewi kura. au ndio tuseme haipewi kura na wananchi na sio kunyanganywa ushindi?
 
Kwanza waziri Nyanga kapelekwa pale kupumzika baada ya kuonekana anawabania wakubwa mambo yao alipokuwa Wizara ya Fedha. Huyu jamaa musimuonee kabisa.
Tunaomba ufafanuzi Bwana mkubwa. Kwani huko SMZ kuna Mawaziri wa kupumzika na Mawaziri wa kufanya kazi. Jee ni vipi hiyo kazi ya awali Bw. Nyanga aliifanya-fafanua- tafadhali ili tuweze kuichangia hii mada.
 
nasikia hata waliohusika hawakuguswa
 
Last edited by a moderator:
Mwacheni(Nyanga) jamani Mzee wa "express yourself".Karume kamuweka pale asije kufa njaa maana hana aliwezalo zaidi ya hayo mambo ya mtandao wa kujiachia.
 
inasemekana zile pesa za kmkm kuna mzee mmoja bonge hivi ambae kwa sasa amestaafu amehusika kuzibeba. lkn Nyanga anamuogopa sijui kwa sababu ni ndugu wa karibu na yeye
 
Back
Top Bottom