Chadema yakataa Unyonge, sasa kuhamia kwenye Makao Makuu mapya

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,026
Chama cha Chadema kimemaliza Utata wa kuwa na Makao makuu yasiyorudhisha ambapo hivi karibuni watahamia kwenye Makao makuu Mapya

Kwa muda mrefu Chadema imekuwa ikidhihakiwa kwamba ofisi zake za Makao makuu Ufipa st Kinondoni Shamba hazina hadhi

Source Mwananchi

==========

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kumaliza utata na lawama za kutokuwa na makao makuu yenye hadhi pale kitakapohamia katika ofisi mpya za kisasa, imefahamika.

Kupatikana kwa ofisi hizo kunakwenda kuhitimisha mjadala wa lawama na kebehi zilizokuwa zikielekezwa kwa chama hicho hakina ofisi zenye hadhi ya chama kikuu cha upinzani wengine wakihusianisha na kiwango cha ruzuku kiliyowahi kuipata.

Kwa sasa ofisi za makao makuu ya Chadema zipo Mtaa wa Ufipa Kinondoni, jijini Dar es Salaam ambako kuna majengo matatu ya kawaida mali ya chama hicho, yanayotumiwa na katibu mkuu na manaibu wake, ofisi za idara, mwenyekiti na nyingine za mabaraza ya chama.

Ofisi za makao makuu ya Chadema zilianzia Kisutu jijini Dar es Salaam, kisha kuhamia Kinondoni miaka 2000.
Taarifa ambazo Mwananchi imezipata zimeeleza kuwa kikao cha Kamati Kuu kilichoketi siku chache zilizopita kilibariki ununuzi wa majengo mawili yatakayotumika kwa ajili ya ofisi za makao makuu Dar es Salaam na Zanzibar.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kamati ndogo iliyoundwa ikiongozwa na Ezekiah Wenje kuwasilisha mapendekezo hayo mbele ya kikao cha kamati kuu kilichoketi Aprili 10, mwaka huu, Dar es Salaam.

Wenje, aliyewahi kuwa mbunge wa Nyamagana ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria alipotafutwa na gazeti hili alisema moja ya mapendekezo ya kamati kuu Chadema lilikuwa ni ama kununua au kujenga makao makuu mapya ya chama ya Zanzibar na Bara.

“Ni kweli nilikuwa mwenyekiti wa kamati, kazi imeshafanyika na tumeshanunua jengo, liko wapi au maelezo zaidi subirini ‘surprise’ siku tunafungua jengo. Mchakato wa kupata jengo la ofisi mpya ya Zanzibar bado unaendelea.

“Wakati ukifika wa kuizindua rasmi mtaiona, sasa itoshe kusema haya kwa sasa,” alisisitiza Wenje, ambaye katika uchaguzi wa mwaka 2020 aligombea jimbo la Rorya.

Mjumbe mwingine wa kamati kuu aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa alisema, katika kikao hicho “zilikuja nyumba kama nne hivi, zilikuwa za Masaki na Mikocheni, lakini tumechukua ya Mikocheni.

Yatakuwa makao makuu ya kisasa sana. Tunataka kuondokana na zile propaganda kuhusu ofisi.

“Sh2 bilioni zimetengwa kwa ofisi za Tanzania Bara na kati ya Sh300-400 milioni kwa ofisi za Zanzibar, kila kitu kinakwenda vizuri. Ila makao makuu ni yenye hadhi hasa.”

Mjumbe huyo wa kamati kuu aliendelea kueleza, “yaani vikao vyote kama vya kamati kuu, baraza kuu vitakuwa vinafanyikia hapo, ni mkutano mkuu pekee ndio utafanyikia nje ya makao makuu.

“Chadema hii si cha mtoto, tunakwenda ku-brand hiki chama, ofisi za kisasa, usajili wa wanachama unakimbia kwelikweli, hadi kufika mwaka 2025 mtaona wenyewe kwenye uchaguzi tukianza na wa Serikali za mitaa,” alisema.

Mwananchi lilimtafuta Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu ambaye hakutaka kukubali wala kukataa kuhusu mkakati wa chama chake kuwa na ofisi za kisasa, badala yake alisema kila jambo lina wakati wake.

“Hicho unachoniuliza au kuniambia bado hakijafikia wakati wake, lakini naamini ukifika kitawekwa hadharani kwa utaratibu wake. Bahati mbaya Chadema hatujawahi kuwa na vitu vya siri.” alisema.

Wakati Mwalimu akieleza hayo, mjumbe mwingine wa Kamati Kuu ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini alidokeza kuwa bajeti ya jengo la ofisi ya makao makuu imetengwa zaidi ya Sh2 bilioni na ofisi ndogo ya Zanzibar kati ya Sh400 milioni hadi Sh 500 milioni.

Kwa mujibu wa mjumbe huyo, fedha za majengo hayo zitatokana na malimbikizo ya ruzuku ya Chadema ambayo chama hicho hakikuichukua tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kutokana na kukataa matokeo yake na mazao yake.

Akizungumzia uamuzi huo, Mchambuzi wa masuala ya siasa na uchumi, Gabriel Mwang’onda alisema ni jambo zuri inga-wa chama cha siasa mtaji wake si jengo bali ni sera mbadala za kuinua nchi na si ofisi nzuri. Alisema kikubwa zaidi ni wanaongoza vyama hivyo kuwa na sera mbadala zitakazowasaidia Watanzania.

“Suala la majengo ni usasa tu umekuja, unajua Chadema ili-wahi kununua magari fulani hivi mengi, ule ndio mtaji kwa sababu unakuwezesha kuwafikia wananchi kueneza sera za-ko. Hii ndio mitaji ya kisiasa si jengo, maana mnaweza kukaa hata chini ya mti mkapanga mambo yenu vizuri.

“Sipingi kabisa chama kuwa na jengo ingawa jambo moja-wapo katika chama ni itikadi watu wanafikiria nini kuhusu sera mbadala. Jambo la pili ni usafiri watu wanafikaje mae-neo ya vijijini kueneza sera, unaweza ukawa na jengo zuri lakini sera mbovu,” alisema Mwang’onda.

Mbali na hilo, mtoa taarifa huyo alisema kamati kuu ilijadili pia kufanya operesheni maalumu itakayoongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuanzia Mei katika Kanda ya Magharibi yenye mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi.

Mwananchi
 
Hahaha kuna yule jamaa yangu wa kupost vyoo vya chadema sijui hili limemfikia???
 
Back
Top Bottom