Askari Polisi wa Arusha mbaroni akisafirisha shehena ya mihadarati

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linamshikilia askari Polisi, Mrakibu Msaidizi wa Kituo cha Polisi Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, John Shauri kwa kosa la kusafirisha shehena ya dawa za kulevya aina ya Mirungi gunia nne yenye bunda kilo 264.

Askari Polisi huyo alikamatiwa Jiji Arusha baada ya kufanikiwa kuwakimbia polisi katika kizuizi cha ukaguzi cha Minjingu Mkoani Manyara Julai 14, 2023.

Kukamatwa kwa Askari huyo kumethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara,Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Nchini (ACP) Lucas Mwakatundu na kusema kuwa askari huyo alikamatwa julai 16 mwaka huu Jijini Arusha.

Kamanda Mwakatundu alisema kuwa baada ya kukamatwa alipelekwa Makao Makuu ya Polisi Babati na kusweka rumande ili aweze kujibu shitaka linalomkabili ndani ya jeshi hilo kabla ya kupata maelekezo mengine kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo.

‘’Ni kweli askari Shauri anashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma hizo na yuko rumande akisubiri taratibu za Kipolisi ndani ya Jeshi hilo kabla ya maelekezo mengine kutoka kwa viongozi wa Juu wa Jeshi hilo’’alisema Mwakatundu

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Manyara zilisema kuwa askari shauri aliyekuwa akiendesha gari aina ya Noah Vox rangi nyeusi yenye namba za usajili T465CUS ilikamatwa majira ya ya saa 2.30 asubuhi akiwa na shehena hiyo ya mirungi ikiwa imejaa kwenye gari hiyo.

Awali askari huyo alisimamishwa na kikosi cha doria cha Polisi Babati na kikosi hicho kilikuwa kikiongozwa na operesheni ofisa wa Polisi Babati Mrakibu Msaidizi{jina tunalo} baada ya kupata taarifa fiche kutoka kwa raia wema juu kusafirisha mara kwa mara kwa mirungi hiyo kunakofanywa na askari huyo asiye na weledi kutoka Arusha kwenda Babati.

Vyanzo vya habari vya polisi Babati viliendelea kusema kuwa askari Shauri alikuwa akifanya biashara hiyo haramu ya kusafirisha Mirungi akiwa na sare za jeshi la polisi ili iwe njia rahisi yeye kupita katika vizuizi mbalimbali vya polisi Makuyuni,Minjingu na Babati.

Habari zaidi zilisema kuwa alipofika katika kizuizi cha Minjingu alisimamishwa na askari na aliposogelewa ili kufanyiwa ukaguzi aliondoa gari kwa kasi na kukimbia ndipo hatua ya kulikimbiza gari hilo ilipoamuriwa na Mkuu wa Operesheini Babati.

Vyanzo vya Kipolisi Babati vilisema kuwa baada ya kukimbizwa na kufikiwa kwa karibu ili aweze kuzuiwa na crusser ya polisi ,askari Shauri alipaki gari pembeni na kulitelekeza gari hilo na kutokomea msituni kusikojulikana.

Vyanzo viliendelea kusema kuwa baada ya hatua hiyo ya askari Shauri kutokomea kusikojulikana,Mkuu wa Operesheni Babati akiwa na askari wengine kwa kushirikianana raia wema waliokwenda katika tukio hilo walipekua gari hiyo na kukuta sare kadhaa za Jeshi la Polisi ,Kitambulisho cha Polisi,Kadi za Benki mbalimbali ,vitambulisho vya NIDA,Tume ya Uchaguzi,Bima ya Afya na ikabainika kuwa askari huyo ni wa kituo cha Polisi Arumeru Mkoani Arusha.

Baada ya upekuzi huo kumalizika garui hiyo ilivutwa na break Down hadi Kituo Kikuu cha Polisi Babati na kukabidhiwa kwa Kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara kwa hatua zaidi.

Hata hivyo habari zaidi kutoka Polisi Babati na Arusha zilisema kuwa askari Shauri ambaye yuko katika mafunzo ya utimamu wa mwili katika Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoani Arusha{FFU} chini ya Mrakibu Mwandamizi{CCP} Mikidadi Galilima ambaye ndiye msimamizi Mkuu wa Mafunzo hayo aliombwa ruhusa siku hiyo majira ya saa 11.30 alfajiri julai 14 mwaka huu na askari huyo kuwa anaumwa nas alipewa mapumziko siku hiyo bila kupewa hati ya matibabu{sick sheet}.

Vyanzo vilisema kuwa baada ya kupewa ruhusa hiyo ndipo safari ya kuanza kusafirisha madawa ya kulevya aina ya Mirungi ilipoanza kutoa Arusha kwenda Babati.

Baadhi ya askari Polisi Mkoani Arusha na Manyara walisema kuwa kuendelea kwa matukio ya uhalifu kwa askari wakubwa wa jeshi hilo katika Mikoa hiyo ni kutokana na baadhi ya hatua stahiki kutochukuliwa kwa baadhi yao kwani kuna matukio mengine manne yamefanyika arusha hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.

Vyanzo kutoka ndani ya jeshi hilo Arusha na Manyara vilisema kuwa miongoni mwa matukiuo hayo ni pamoja na askari kukiri kupokea rushwa na kurudisha zaidi ya shilingi milioni 9 katika matukio ya Ngaramtoni na Kwa Mrombo kwani Vigogo wa polisi Arusha wamekuwa wakiwalinda vigogo wenzao.

Ends...


MANYARA: ASKARI POLISI MBARONI AKIDAIWA KUSAFIRISHA SHEHENA YA MIHADARATI
Taarifa za awali zilieleza mtuhumiwa alikuwa akisafirisha Mirungi Kilo 264, alipofika Minjingu akasimamishwa na Askari ambao wakataka kukagua gari alilokuwa akiendesha aina ya Toyota Noah, ghafla akaliondosha kwa kasi kisha kwenda kulitelekeza njiani na kuondoka kwenda katika kituo chake cha kazi Mkoani Arusha.

Inadaiwa kabla ya kukamatwa mtuhumiwa amekuwa na tabia ya kusafirisha biashara hiyo haramu akiwa na sare za Jeshi la Polisi ili iwe njia rahisi kupita katika vizuizi mbalimbali vya Polisi #Makuyuni, #Minjingu na #Babati.

Alipoulizwa na JamiiFirums, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa #Manyara, Lucas Mwakatundu amesema “Tunawashikilia Watuhumiwa watatu kuhusu tukio hilo, wawili ni Askari Polisi na mmoja ni raia, walikamatwa wakiwa katika vituo vyao vya kazi kwa kuwa gari iliyokutwa na mihadarati halikukutwa na mtu yeyote."

Kuhusu majina ya watuhumiwa amesema “Ni mapema kwa sasa kuyataja kwa kuwa uchunguzi unaendelea na kila mmoja anasema sio yeye.”
 
Hayakua manne ,yaani voxy ichome wese kubeba manne tu,operation unit imejiongeza
 
Back
Top Bottom