Waziri Mkuu: Tumejiandaa vema kupambana na mgomo wa madaktari

cant believe this.so pinda anajaribu kutuambia kwamba wanatunishiana misuli na madoc.Omg
 
Kuna habari kuwa serikali inatayarisha Tangazo la ajira kwa nafasi za Udaktari na udaktari bingwa haraka iwezekanavyo.

Je, hii inaweza kuwa long term solution ya matatizo ya mgomo wa madaktari.
 
Serikali imeagiza madaktari Cuba na Russia
kama wana hizo pesa za kuwalipa hao madaktari wa Russia (ambao kipato chao ndani ya Russia ni kikubwa kuliko cha madaktari wa Tz, pia mazingira yao ya kazi ni bora zaidi.... Take it from me!) pamoja na hao wa Cuba, kwa nini wapoteze hizo pesa? kwa ajili ya thamani kubwa sana ya Mponda na Nkya? Na wataweza kuwamaintain hao madaktari wa nje mpaka lini? Kutishiana nyau watu wazima tu huku!!! Acha utani!
 
Sasa nao watalipwaje? Je vifaa vya kufanyia kazi navyo watanunulia hao ma-doctor wapya? sirikali yetu inaweka mambo ya siasa ndani ya utaalamu,wamewaleta mamuraa wakashindwa kufanya kazi sasa hao wapya wataelekezwa na nani?
 
kwani kuna madaktari ambao hawana kazi hapa nchini?
Hiyo hela itakayotumika kwa ajira mpya kwa nini isitumikew kulipa madai ya waalimu kwanzza?
 
Ni TBC news ya Saa 10 alasiri, Waziri mkuu amesema wanasubiri waone kinachoendelea na wamejiandaa vema kukabiliana na hali itakayotokea.
Wanasema misimamo kama serikali na baadae wanakaa tena kufikia muafaka.
Anayetesa wananchi kwa sasa ni Waziri na Afya na naibu wake, Nadhani wangekubali kuwa wao ndiyo kero namba 1 wakajishusha kuokoa taifa.
Acha tuone kama wanakuja Doctors kutoka China au la
Wanasubiri waone jinsi watu watakavyokufa kutokana na mgomo ndio wachukue hatua! kazi tunayo
 
Safiii,, hiyo ndiyo dawa,, Ndiyo dawa haswa ya paka mramba tui,, kama hataki panya na wali usimpe
 
Kuna habari kuwa serikali inatayarisha Tangazo la ajira kwa nafasi za Udaktari na udaktari bingwa haraka iwezekanavyo.

Je, hii inaweza kuwa long term solution ya matatizo ya mgomo wa madaktari.

sasa daktari Bingwa atakua hana kazi huko aliko ? atakua anakunywa chimpumu na mkewe ? ama atakua anauza Gongo ?
anakuwaje Bingwa bila kazi jamani ? UPUNGUANI UNAWAZUNGUKA WAATENDAJI WETU WAKUU
 
kuna habari kuwa serikali inatayarisha tangazo la ajira kwa nafasi za udaktari na udaktari bingwa haraka iwezekanavyo.

Je, hii inaweza kuwa long term solution ya matatizo ya mgomo wa madaktari.

na ikitangza tu hao wapya wanagoma hapohapooo
 
Kuna habari kuwa serikali inatayarisha Tangazo la ajira kwa nafasi za Udaktari na udaktari bingwa haraka iwezekanavyo.

Je, hii inaweza kuwa long term solution ya matatizo ya mgomo wa madaktari.

Mkuu Sr. Magdalena,
Tunaomba source ya habari hii, plse!!
 
Hii siyo tetesi ni kweli, serikali inataka kuajili madaktari na madaktari wa sasa watatakiwa kuomba ajira upya.

Nice move.
 
binafsi naona madoctas wamejaa misifa ya kijinga vichwani mwao. sababu inayowafanya wagome ni kwa ajili ya lucy na haji tu? this is crazy. wakijiuzulu hawa wawili then what? mimi nashangaa wameacha kushughulikia mambo ya msingi sasa wanahangaika ni vitu vya kipuuzi. interlectual yao iko wapo. mbona naona pumba tu kwenye vichwa vyao.
huyu ni ***** tu! hata kingereza chake ni broken, anatuletea sisi watu wazima hapa! (huwezi kusema intellectual yao ukitumia simple grammar, aende akarudie madaftari yake ya shule ya msingi kabla ya majigambo na kingereza chake cha ugoko!)
 
Ngwendu nafikiri hawa madaktari hujawaelewa vizuri! kuna mambo ambayo walikubaliana na serikali wakati wanarudi kazini kuwa watu ambao ni kikwazo pale wizarani ni hao mawaziri na inabidi watoke, maana hao madaktari wakifikia makubaliano na serikali hayo makubaliano yao inabidi yatekelezwe na wizara ya Afya sasa yatatekelezwaje na watu ambao madaktari hawana imani nao? Nafikiri PINDA anatakiwa kujifikiria kwanza kabla hajafungua kinywa chake maana tunaoumia ni sisi raia wa kawaida.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
sasa daktari Bingwa atakua hana kazi huko aliko ? atakua anakunywa chimpumu na mkewe ? ama atakua anauza Gongo ?
anakuwaje Bingwa bila kazi jamani ? UPUNGUANI UNAWAZUNGUKA WAATENDAJI WETU WAKUU

Mkuu kwa kifupi ajira za madaktari wa serikali zinafutwa na kuajiliwa upya, wanasheria watatuelezea kisheria hii imekaaje.

all in all, big up Pinda.
 
Back
Top Bottom