Waziri Mkuu Pinda asitisha utekelezaji wa agizo la Magufuli la Bomoa bomoa

ufanisi? Ni ule uliosababisha serikali kulipa fidia ya bilioni 3 kwa kubomoa petrol station jijini mwanza kwa madai kuwa imejengwa katika hifadhi ya barabara au upi?

Jatropher usilete chuki zako kuhalalisha upuuuzi kama huo!, usihadae wana jf kwa kurejea kesi ambazo serikali ilipoteza! Nani hajui kama ''law'' ni ''art''? Mbona mkataba dowans ulisitishwa kihalali lakini kesi tukapoteza?, nani hajui kama Zombe na wenzake waliua lakini wako mtaani wanakula kuku?, nani hajui kama babu seya na wanae hawakubaka lakini wako wanaendelea kunyea debe?, sheria ni sanaa na hapa tanzania inaongozwa na rushwa, na kama ujuavyo serikali haitoi rushwa kwa hiyo haishindi kesi nyingi!, hilo unalijua. Magufuli ni mchapa kazi na anafuata sheria. Sio ndugu yako huyo anakurupuka kusema wanaoua arubino wauawe halafu analia mwenyewe! PM AMECHEMKA, usitetee ujinga eti kisa magufuli aligusa interest zako! Koma

MENGINE YOTE ULIYOSEMA YANA BENEFIT OF DOUBT LAKINI LA MAGAFULI KUFUATA SHERIA NALIPINGA KABISA KWA SABABU MAGUFULI NI MMOJA WA WABUNGE WALIOKUWA KATIKA BUNGE LILILOPITISHA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI NA 5 YA 1999, HIVYO ANAFAHAMU FIKA KUWA VIFUNGU NAMBA 15 NA 16 VINAWALINDA WATU WALIOGAWIWA ARDHI KATIKA OPERESHENI VIJIJI (SOMA KIAMBATANISHO). ILIKUWAJE MWAKA 2001 TENA BILA KUSHIRIKISHA NAGZI ZA MKOA. WILAYA, MANISPAA NA SERIKALI ZA MITAA AKAMWAGIZA MKANDARASI WA WIZARA KUINGIA MITA 120 NDANI YA ARDHI NA MAKAZI YA WANANCHI PANDE ZOTE MBILI ZA BARABARA KWA KUTUMIA KANUNI ZA SHERIA YA BARABARA YA MWAKA 1967, AMBAZO KIMSINGI KUTOKEA 1999 HAZIWEZI KUFANYA KAZI MAHALI POPOTE PALIPOKUWA NA ARDHI YA VIJIJI?

IKIZINGATIWA KUWA MWAKA 2001, WAKATI ANAAGIZA ARDHI NA MAKAZI YA WANANCHI KUINGILIWA, ILIKUWA NI MIAKA MIWILI TU KUTOKEA KUPITISHWA KWA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI NA 5 YA 1999; NA KAMA ILIVYO ADA SHERIA HIYO ILIKUWA HAIJACHAPISHWA, KUSAMBAZWA NA WANANCHI KUPATIWA ELIMU YA SHERIA HIYO. HIVYO WAKATI HUO WANANCHI WALIKUWA HAWAJUI HAKI ZAO NDIO MAANA AKAWABURUZA KWA KUWAPANDIA MAWE NA MABANGO YA KUONYESHA MWISHO WA HIFADHI YA BARABARA KATIKA ARDHI NA MAKZI YAO ISIVYO HALALI?

WATANZANIA NI LAZIMA TUJIFUNZE KUWA WAKWELI, HUYU MTU ALIWAFANYIA WANANCHI HAWA HILA. NA AMEWAATHIRI SANA KIJAMII NA KIUCHUMI, WATU WAMESHINDWA KUENDELEZA ARDHI NA MAKAZI YAO, MABENKI YAKASHINDWA KUTOA MIKOPO N.K. NDIO MAANA KATI YA UBUNGO HADI KIRUVIA HAUWEZI KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI WALA ATM KAMA ILIVYO MBAGALA KATIK ABARABARA YA KILWA AU TEGETE, BUNJU N.K KATIKA BARABARA YA BAGAMOYO.

KUCHAGUA SHERIA ZA KUFUATA NA KUWAFANYIWA WANANCHI HILA NDIO UNAKUUITA KUFUATA SHERIA?
 
jatropha anavyojitahidi kuhadaa watu kuonesha mapungufu ya magufuli nadhani ataku na mrema aliekua tanroads!

nijibu kulingana na vifungu vya sheria ninavyoweka humu, sio kuleta poroja tupu. Tatizo letu watanzania ni wavivu kujisomea ndio maana magufuli anadanganya wengi kuwa mtu wa kufuata sheria, si anajua wengi hatusomia hataukipatiwa attachment
 
ukikaa na kundi la wajinga hata wewe unakuwa jinga: Haya niliyategemea kwa pinda! Hata hivyo hawa nao wanang'ang'ania nini ccm kama siyo wezi tu' eeehh huyo sita na magufuli hata mwakyembe???? Nashindwa kuwavumilia ama watoke huko ccm ama nao waendelee kuwa wabaya wa wapenda maendeleo tanzania

watoke ccm waende wapi, nani atapokea mbabe kama huyu asiyefuata sheria na kanuni za utawala bora?
 
Waziri wa ujenzi John Magufuli ameanza kupunguzwa kasi na serikali katika kusimamia zoezi la bomoa bomoa kwenye hifadhi ya barabara baada ya kuagizwa kusimamisha zoezi hilo mpaka itakapoamuliwa vinginevyo na baraza la Mawaziri.
Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri mkuu Mizengo Pinda leo wakati akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Chato ambapo alimwagia Waziri huyo sifa lukuki katika kutekeleza majukumu yake.
Pinda alisema kasi aliyoanza nayo Magufuli katika wizara yake mpya imeitisha serikali na kuwa ameagizwa kusimamisha zoezi hilo mpaka litakapojadiliwa na baraza la mawaziri.
“Rais aliona kwenye bara bara panale lega na kumrudishaMagufuli kwenye wizara hiyo,huyu serikalini tunamwita ‘buldoza’ hata hiyo ameanza kwa speed kubwa na tumwemwagiza asimamishe zoezi hilo mpaka litakapojadiliwa na baraza la Mawaziri”alisema Pinda
Akisema baraza hilo litakaa na kuangalia upya maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya bomoa bomoa na kusema kuwa kabla ya kuruhusu zoezi hilo kuendrlea lazima wakubaliane kwanza kwenye baraza la mawaziri.
Akiwahutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara katika shule ya msingi Chato jana jioni Waziri mkuu Pinda alisema inabidi pia itolewe elimu kwanza akidai maeneo mengine bomoa bomoa sio lazima.
Aidha alisema zoezi hilo ambalo lilizua malalamiko nia ya kulisimamisha ni kujipanga upya huku akisisitiza kuwa serikali inamwamini Waziri Magufuli kama kiongozi mwenye uwezo na ilimpa ofisi hiyo ili pia aweze kuwabana makandarasi wazembe.
Pia katika mkutano huo ambao awali waziri Magufuli aliutumia kujifagilia kwa kukiponda chama cha Chadema kilichofanya maandamano ya amani hivi karibuni wilaya kwake,Pinda alisema waziri huyo amekuwa akitumiwa kunyosha mambo kwenye wizara zinazolega lega.
Kasi ya Magufuli ambayo pia inaonekana katika jimbo lake kwa nyumba nyingi zilizo katika hifadhi ya bara bara kuwekewa mkasi wa kuziondoa ilianzia katika ubomoaji wa ofisi za Tanesco jijini Dar es saam zoezi ambalo alisema litaendelea kuyakumba majengo mengi ya serikali.

Sasa kama waliona panalegalega mbona wanamstopisha kwa speedi yake!

speedi gani walitaka? Ari mpya iko wapi? Nguvu mpya iko wapi? kasi mpya kwa maendeleo iko wapi?

Jamaa kaanza kufanya kazi kwa kasi kwa mujibu sheria wanampiga STOP! sasa mabasi ya kasi yataanza lini? Ahh!

Kufuaata kanuni na sheria za road reserve ni kuwa buldozer!!
 
yaani pinda sijui yukoje huyu baba...hivi anafanya haya kwa manufaa ya nani?hivi hapa kuna serikali au mautumbo yanayojaza nzi tu hapa
 
yaani pinda sijui yukoje huyu baba...hivi anafanya haya kwa manufaa ya nani?hivi hapa kuna serikali au mautumbo yanayojaza nzi tu hapa

PINDA KACHUKUA UAMUZI HUO KWA MANUFAA YETU WANYONGE.

Ibara ya 2 ya Kanuni za Sheria ya barabara (Tangazo la Serikali Namba 161 la tarehe 5/5/1967) inatamka kuwa hifadhi ya barabara kuu zote hapa nchini (Trunk roads) ni Futi 75 kutoka katikati ya barabara. Vivyo hivyo Ibara ya 29 ya Kanuni za Sheria mpya ya barabara namba 13 ya 2007 (Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009) (a) inatamka kuwa eneo la hifadhi ya barabara zote Kuu (Trunk Roads) za njia moja (Single Carriage way); na (b) kwa njia mbili (Dual Carriage ways) eneo la hifadhi barabara litakuwa ni Mita 60, yaani Mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara.

Ibara ya 27 ya Kanuni za sheria mpya ya barabara zilizotajwa hapo juu zinatamka kuwa upana wa njia moja ya barabara (lane) kwa barabara ya njia moja utakuwa si chini ya Mita 3.25 kwa njia moja ya kuelekea upande mmoja. Hivyo katika upanuzi wa barabara ya Morogoro, Mita 60 za hifadhi ya barabara zilizotengwa kama ilivyoelezwa hapo juu, zina uwezo wa kuzalisha njia 18 za barabara zenye upana uliotajwa hapo juu, yaani njia 9 za barabara za kutoka DSM kwenda Kibaha, na 9 za kutoka Kibaha kuja DSM.

Hivyo madai ya Wizara ya Miundo Mbinu kuwa msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro katika DSM na Kibaha husababishwa na wananchi waliojenga nyumba za makazi katika eneo lililo nje ya Mita 60, zilizotengwa kama hifadhi ya barabara hayana ukweli wowote. Eneo lililo nje ya Futi za 75 kutoka katikati ya barabara kwa mujibu wa Kanuni zilizotajwa hapo juu za 1967 liligawiwa kwa wananchi wakati Serikali ya awamu ya kwanza ilipokuwa kitekeleza sera ya Operesheni Vijiji.

Kimsingi Kanuni za Sheria ya barabara ya 1967 zilizokuwa zikitenga upana hifadhi ya barabara unaozidi Futi 75 (kati ya Mita 90 hadi 120) kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha zilikoma baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungo wa Tanzania kupitisha kwa Sheria inayolinda ugawaji wa ardhi uliofanyika chini ya operesheni vijiji kati ya Tar 01 Januari 1970 hadi kuanza kutumika kwa Sheria ya Ardhi namba 5 ya 1999 (Vifungu 15 na 16 vinatamka kuwa ugawaji wa ardhi uliofanywa mahali popote katika kijiji chini ya operesheni vijiji hata kama ni kwa kukiuka sheria yoyote ni halali na wenye kutoa haki ya wagawiwa kumiliki ardhi husika………).

Hivyo kitendo cha Wizara ya Ujenzi kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi Mita 90 hadi 120 pande zote mbili za barabara uliofanyika mwaka 2001, kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha na kupanda wa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara ya Morogoro pasipo kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa na Serikali za Mitaa ambazo zinzwafahamu na kuwatambua wananchi wanaohusika na sheria ya ardhi ya vijiji iliyotajwa hapo juu ulifanyika kimakosa na kusababisha athari kubwa sana za kijamii na kiuchumi kama vile kuwakosesha wananchi maeneo ya kutengeneza fursa za ajira, kujiajiri, huduma kama vile za kibenki, ATM n.k.

Mwaka 2010,ikiwa ni miaka 9 tokea uingiaji huo haramu, kitendo cha TANROAD kwa maagizo ya Wizara ya Miundo Mbinu kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi zaidi ya Futi 75 au Mita 22.86 na kufanya maendelezo yoyote ikiwemo ni pamoja na kuweka alama za X katika nyumba za wananchi ni haramu na ni cha kuwanyanyasa wananchi.
 
Eh, ina maana huyo Mheshimiwa Magufuli alikuwa anfanya bomoa bomoa bila ridhaa ya sheria? Kama sheria ya ardhi inaelekeza umbali wa kutoka barabarani wakati kujenga sasa Baraza la Mwaziri linajadili nini, au rekebisha sheria ili kupunza huo umbali.
 
Bongo mm inaniacha hoi, hivi hawa wakubwa, hawakai kwanza wakakubaliana wafanye nn na wasifanye nn? This is disgusting!
Ni sawa na familia, mama anawambia mtoto nenda shule, baba baadae anamwambia usiende, mwishowe mtoto anachanganyikiwa! anaona baba na mama wote wazushi!
 
waziri mkuu tunaye sana, tatizo lako kapotolo umelishwa propaganda za magufuli na wewe kuzichukulia zilivyo. Imebidi waziri mkuu aingile kati ili kuokoa fdha za serikali kulazimika kuwalipa watu fidia baada ya kushinda kezi zao mahakamani kama ilivyotokea 2001 wakati magaufuli alapoagiza petrola station mjini mwanza ibomolewe kwa kuwa imejengwa katika hifadhi ya abarabara kumbe sio kweli hata kidogo. Serikali ililazimika kulipa fidia ya bilini 3 kwa mmiliki wa petrol station iliyobomolewa. Baadaye ukweli halisi ulifichuka kuwa magufuli alikuwa na chuki na mahndisi wa jiji la mwazana mahandisi tizeba toka hapo wizarani, tume ya jiji mpaka alipohamishiwa jiji la mwanza kama mhandisi wa jiji la mwanza. Aliwahi hata kufanya jitihada za kujaribu jina la mhandisi huyo kufutwa katika orodha ya wahandisi waliosajiliwa hapa nchini. Katika kutimiza kiu ya chuki zake na mhanddisi huyo ndipo akaamuru ibomolewe.

Jumamosi iliyopita ulikuwepo na mkutano wa waathirika wa eneo la ubugo kimara, zaidi ya watu 50 wana hati miliki, na nyumba zao tayari zimechafuliwa kwa kuweka alama ya x na "maneno bomoa mali ya tanroad" je huo si ukiukwaji wa sheria za nchi? Mtu kama huyu unaweza kusema nafuta sheri kweli? Kwani magafuli anatumika serikali ipi na ni serikali ipi iliyowapatia wananchi hao hati miliki?

Ibara ya 2 ya sheria ya barabara ya 1967 inatamka wazi wazi kuwa hifadhi ya barabara zote kuu (trunk roads) hapa nchini itakuwa futi 75 au mita 22.86 kila upande sawa na futi 150 au mita 45 pande zote mbaiuli. Ibara ya 27 ya kanuni za sheria ya barabara ya 2007 zilizopitishwa kupita tangazo la serikai na 21 la tar 23 januari 2009 inatamka kuwa upana wa chini kabisa wa "lane" moja ya barabara kuu hapa nchin utakuwa si chini ya ni mita 3.25. Hivyo eneo la hifadhi ya barabara la mita 45 lina uwezo wa kuzalisha lane 14; lane 7 za kwenda upande mmoja na lane 7 za kwenda upande mwingine. Nitajie barabar gani hapa nchini imewahi kutumia na kumaliza upana huo uliotengwa kiasi cha magafuli kuwavamia watu walioko mita 120 kutoka katakati ya barabara? Hivyo ni propaganda kudai kuwa msongamano wa magari unasababsihwa na watu kujenga katika hifadhi ya barabara.

Kifungu cha 15 na 16 cha sheria ya aradhi namba 5 ya 1999 vinatamka kuwa ugawaji wa ardhi uliofanyikia wakati wa operesheni vijiji ni halali (soma attachement) hivyo sheria ya barabara ya 1967 anayotumia magufuli mwaka 2001 hadi 2010 imeshafutika na haiapo kabisa. Maaufuli anatakiwa kwanza kujenga lane 14 katika hifadhi ya barabara iliyopo ndipo aje kuwaingilia walioko nje ya eneo hilo. Kwa hali hii utagundua kuwa mambo anayoyafanya magufuli ni matokeo ya kukurupuka kwake katika yote hamshirikishi ofisi ya waziri mku, wizara zingine, ngazi za mkoa, wilaya, manispaa, serikali za mitaa

Hapo kwenye red ni kuwa anatumikia serikali ya wala rushwa ambao wamezitelekeza sheria za nchi kwa kukumbatia matakwa ya mafisadi.

Na hii inamuwia vigumu sana Magufuli kutimiza matakwa ya sheria kwa sababu wezi wakuu wa nchi hii wameiweka serikali mfukoni.

Halafu unaongelea lane 14, unajua maana ya lane wewe!!
 
Naamini Dk. Magufuli sio mropokaji hata kidogo na hawezi kukurupuka kama huyo bepari Pinda, huyu Dk. yuko vizuri na alichotaka au atakachofanya is quite right!! sasa kama kweli Pinda ana akili si angeongea na Magufuli kwanza? iweje akurupuke na kutangaza hadharani kabla ya kuwasiliana na mtendaji wake? CCM wamekufa na wachache waliobaki ndio wanamaliziwa kabisaaaa
 
Serikali iliyoparanganyika Raisi,Waziri Mkuu,Makamu wa Raisi,Wakuu wa Majeshi,Wakuu wa Mikoa,Maraisi na watendaji serikali kila na mtu na kivyake kila mtu anajichezea muziki wa tune yake he he he wengi walisema kuna ombwe la uongozi huwezi kumpinga waziri wako mbele ya Kadamnasi amedharilisha Magufuli pole sana Mzee,usipokuwa macho na serikali hii utarudishwa ujerumani kwenye machela tena
 
Ndo maana mimi nasema kwa mtu yeyote anayedhani CCM ni chama cha watu wenye akili.....basi nayeye ni mwehu. Pinda navyomjua sikutegemea atasikila ushauri wa akina kikwete na Lowasa kwani....yote aliyosema Pinda katumwa na Jk na lowasa na akaambiwa kabisa kwamba akayasemee chato ambako ni nyumbani kwa Magufuli.

Najipa moyo tu kwamba hata wafanye nini CCM Magufuli hata akienda CHADEMA atapata ubunge kirahisi sana.
 
CCM mtabaki kuwa wajinga tu......kwa nini mnaendekeza siasa kwenye masuala ya kisheria zaidi???? Nani aliyeweka/Tunga hizo sheria za mita 30 kutoka barabarani?? Si ni bunge???........Pinda na CCM yako nyote ni hovyo tu.
 
Yale yaliyomkuta spika wa bunge la tisa, Samuel Sitta sasa huenda yakamkuta waziri wa ujenzi Joni Magufuli.Inaaminika Sitta aliwekwa pembeni kwa hila katika kinyang'anyiro cha uspika kwa sababu tu"ya kusimamia bunge la tisa katika misingi ya uwazi,haki,viwango na kuisimamia serikali vizuri.

Sitta alienguliwa kwenye kinyang'anyiro cha uspika wa bunge la kumi kutokana kile ambacho ccm walikiita "mda umefika kwa wanawake kuongoza mhimili ya serikali" lakini ukweli wa mambo zile zilikuwa ni hila za kumwanusha bwana Sitta" zilikuwa njama za mafisadi waliojeruhiwa na bunge makini la tisa"

Pinda waziri kuu amemdhoofisha bwana Magufuli kwa kutoa amri ya kusimamisha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa karibu na hifadhi ya barabara. Awali magufuli alikuwa ametoa amri ya kubomoa nyumba ambazo zimejengwa maeneo ya hifadhi ya barabara.

Amri ya magufuli ipo katika misingi ya sheria za nchi ambazo kamwe hazitakiwi kuvunjwa wala kupindishwa kama amri ya Pinda alivyopindisha. Lakini bwana Pinda ameamua tu kumdhoofisha, kumdhalilisha maghufuli mbele ya umma wa watanzania. Pinda anatumiwa,pinda yupo kimkakati.

Wakati sasa wakosaji na waliovunja ile sheria ya kujenga kwenye hifadhi ya barabara wanamzomea Magufuli anaonekana kachemka ukizingatia Pinda aliotoa amri hii ya kinafiki akiwa jimboni kwa Magufuli.

Lakini kuna haja ya kutafakari kwa undani juu ya kile kilichomsukuma Pinda kutoa amri ya kupindisha taratibu,kama anasukumwa, basi ni kwa maslahi ya nani.Pinda amenukuliwa na gazeti la mwananchi akisema bomoabomoa isimishwe kwanza mpaka hapo baraza la mawaziri litakapoketi kujadili suala hilo. Magufuli anateleza sheria ambazo zimewekwa na bunge kwa niaba ya wananchi.

Kabla ya kupelekwa bungeni baraza la waziri liliridhia sheria hiyo. pinda anataka kuwaaminisha kwamba Magufuli anakurupuka ,amri ya kubomoa haina baraka za baraza la mawaziri.

Kule kukaa tena kwa baraza la mawaziri ni kwa maslahi ya nani. Mafisadi?

Serikali hii imelala, inathibitiwa na mafisadi kwa "REMOTE"

Pole sana Magufuli kwa kudhalilishwa na bosi wako pinda,chukua maamuzi magumu. Fanya kama Martha Karua, aliyekuwa waziri sheria wa kenya katika serikali ya mseto.
 
Insubordination of Magufuli at its highest degree for 2015....... tena kwa kumtumia kiranja mkuu..... CCM hureeeeee............. Kwa wana-mapinduzi lets applaud CCM.....
 
Naona ingekuwa vizuri kama WM (PM) angemwagiza yeye mwenyewe Makufuri kusitisha zoezi hilo ili kuepuka kumdhalilisha na kumvunja moyo waziri wake? Yawezekana kweli kukawepo na jambo mgongoni mwa agizo hilo
 
amemvunja moyo waziri mwenye maamuzi kwa serrikali yao hii ya kipuuzi imeniuma sana.Ukiwa intellectual person huwezi kufanya upuuzi huu wa pinda hata kidogo.
 
Back
Top Bottom