Mfugale awavimbia Waziri Mkuu na Waziri wa Ujenzi kwa kivuli cha Rais Magufuli?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Siku kadhaa zilizopita, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo kwamba kutokana na meneja wa Tanroads wa Morogoro Godwin Andalwisye kufanya uzembe wa kutoyafanyia ukaguzi madaraja ya barabara ya Morogoro hadi Dodoma na kusababisha uvunjikaji wa daraja, basi aondolewe mara moja Morogoro na kurudishwa wizarani kupangiwa kazi nyingine. Wazirir Mkuu alikasirishwa na kitendo hicho kwa kuwa fedha za kufanyia ukaguzi zilikuwapo na alibainisha kwamba daraja hilo lingefanyiwa ukaguzi lisingevunjika.

Aliporudi Morogoro kuangalia maendeleo ya kazi, Waziri Mkuu ameshangaa kukuta meneja wa Tanroads Morogoro bado hajaondolewa. Alikerwa na hilo na kuuliza kwa nini meneja huyo bado hajaondolewa licha ya agizo lake. Kwa kujiamini kabisa, Mfugale alimjibu Waziri Mkuu kwamba "Andalwisye ni mmoja wa mainjinia wachache wenye utaalamu wa ujenzi wa madaraja, kwa hiyo huduma yake bado inahitajika hapa. Wewe ulitoa agizo na mimi ndio mtekelezaji, lakini bado tunahitaji utaalamu wake".

Ukweli ni kwamba si kweli kwamba Tanzania hatuna mainjinia wa kutosha wa ujenzi wa madaraja. Wapo wengi sana. Na tangu lini amri ya Waziri Mkuu inapingwa kwa sababu anaetuhumiwa anaonekana bado anahitajika? Watumishi wangapi wanaondolewa kwa amri toka juu licha ya utumishi wao kuhitajika?

Waziri Mkuu ni kiongozi anamuwakilisha Raisi kiutendaji. Je Raisi Magufuli anaweza kutoa amri na mteule wa chini akaikiuka kwa kuwa mtu aliyetumbuliwa bado anahitajika?

Katika hali ya kawaida Mfugale anatakiwa kuwajibishwa. Kufuata protokali, alitakiwa akamuombe Waziri Mkuu Majaliwa kwamba huyo Meneja wa Morogoro abaki kwa sasa - kitu tunaita "no surprise" katika mambo ya utawala. Kitendo alichofanya Mfugale ni kumdhalilisha Waziri Mkuu na Waziri wake wa Ujenzi.

Kwani kulikuwa na ubaya gani kwa Mfugale kuteua meneja mpya wa Tanroads Mororgoro na kumpeleka Andalwisye kwenye site kama mtaalamu tu kutoka Wizarani kama ni kweli anahitajika kiasi hicho? Kwani hilo daraja ni lazima lijengwe Andalwisye akiwa ndio meneja wa Tanroads Morogoro?

Sasa suala la kujiuliza ni kwamba Mfugale ametoa wapi ujasiri wa kumvimbia Waziri Mkuu na hata Waziri wake wa Ujenzi? Mengi sana yamesemwa kuhusu uhusiano wa Magufuli na Mfugale kuhusiana na miradi ya barabara wakati Magufuli ni waziri wa ujenzi. Watu hawakushangazwa na flyover ya Tazara kupewa jina la Mfugale.

Je, hilo ndilo linalomfanya Mfugale aone kwamba yuko "untouchable" na Waziri Mkuu Majaliwa na anaweza kumvimbia? Tangu lini amri ya Waziri Mkuu inakuwa "overruled" na mtu kama Mfugale ambaye kimadaraka yuko chini ya Waziri wa Ujenzi? Kumbuka amri hii ilitolewa na Majaliwa kwa Waziri wa Ujenzi, kwa hiyo kimsingi, Mfugale amemvimbia Waziri wake wa Ujenzi pamoja na Waziri Mkuu.

Source:
Majaliwa ahoji aliyemhamisha kuendelea na kazi
PM aghast to find manager he transferred still at work

Uzembe wa TANROADS sijaanza kuuandika leo. Ukweli ni kwamba mimi nachukia watu wazembe, wawe TANROADS au Polisi au hata serikali. Ajali nyingi Tanzania naona zinatokea kwa uzembe tu wa TANROADS, pamoja na hili suala la daraja. Angalia hii thread ya 31 Dec 2019.

Ajali iliyoua watu 6 Dodoma: Wanaopaswa kukamatwa na kuwekwa ndani ni Mfugale na Meneja wa Dodoma wa TANROADS Dodoma, sio dereva wa lori
 
Bila sauti , ama video ni kama unafanya umbeya. Muhimu kazi inakwenda. Pia katika maisha kuna majanga ya asili mfano mafuriko, vimbunga nk. si busara kutoa adhabu ama hukumu kwa mwanadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesoma source? Kwa hiyo mimi na IPPMedia na Mwananchi tunafanya umbea? Kuna watu ni wazi hamna elimu ya kutosha kuwa members wa JF wa kujibu thread kama hizi.
 
Kama hilo jibu alipewa waziri mkuu basi protocally haifuatwi! Kwa hiyo Mfugale kwa vile ni mtekelezaji wa agizo mpaka aamue anatekeleza lini agizo la Waziri Mkuu? Anasema ni kati ya Mainjinia wachache lakini wakati huohuo ameshindwa kufanya ukaguzi wa madaraja!!
 
2025 iwapo Kassim atakuwa Rais ole wake Kassim awe mtu wa visasi yale mashamba na matreka aliyojimilikisha huyu bwana kwa kiburi cha bwana Yohana kwake itakuwa kilio cha kusaga meno.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sidhani kama Majaliwa atasahau hili. Akija kuwa raisi kitu cha kwanza ni kubadilisha jina la flyover ya Tazara. Na usisahau kwamba Majaliwa alikuwa na moto sana mwanzoni, siku moja akazimwa hadharani na raisi na kuambiwa hata yeye anaweza kutumbuliwa kama wengine. Hiyo ilimnyamazisha sana Majaliwa.

Lakini tambua kwamba Magufuli anajua hilo. Sio rahisi Majaliwa kuja kuwa raisi katika mazingira kama hayo.
 
Suala la muda tu huyo Mhandisi atahamishwa, kwa amri ya PM
Katika hali ya kawaida hata Mfugale anatakiwa kuwajibishwa. Alitakiwa akamuombe Majaliwa kwamba huyo Meneja wa Morogoro abaki kwa sasa - kitu tunaita "no surprise" katika mambo ya utawala. Kitendo alichofanya Mfugale ni kumdhalilisha Waziri Mkuu.

Kwani kulikuwa na ubaya gani kwa Mfugale kuteua meneja mpya wa Tanroads Mororgoro na kumpeleka Andalwisye kwenye site kama mtaalamu tu kutoka Wizarani kama ni kweli anahitajika kiasi hicho? Kwani hilo daraja ni lazima lijengwe Andalwisye akiwa ndio meneja wa Tanroads Morogoro?

Na ukweli ni kwamba Mfugale ni mwongo, wtalaamu wa madaraka ambao zaidi n structural engineers wapo wengi tu hapa nchini. Hilo sio daraja la kutoka Dar kwenda Zanzibar kwamba liko complicated sana kulijenga linahitaji utalaamu wa juu. Hata Technician wa Arusha Tech anaweza kulisimamia.

NI wazi Mfugale alitaka kumuonyesha Waziri Mkuu Majaliwa yeye ni nani katika watu wa Magufuli. Au labda Magufuli alimwambia Mfugale don't bother kumhamisha Andalwisye, maana huko sio kujiamnini kwa kawaida.
 
Mfugale = Magufuli na Magufuli = Mfugale tena tokea walipokuwa katika Docket hiyo muhimu kwa Maendeleo ya Watanzania.

Mshaurini Premier Wenu awe makini kwani kuna Watendaji ndani ya Awamu hii hawagusiki na asipoangalia hao hao anaowagusa sasa wanaweza wakamchomea Utambi na akajikuta anakuwa Premier kwa miaka Mitano tu na huenda Awamu ijayo Mmoja wapo wa wale anaoonyesha Kuwagusa Kiutendaji akawa Mbunge au akatoka huko huko Bungeni na akawa Premier kwa Kipindi cha mwisho kisha nae akajikuta ananyooshwa Yeye, wana Ruangwa pamoja na Timu yake ya VPL ya Namungo FC.
 
Yes, huu utawala umetengeneza "vipenzi vya Rais" hao wanajua Rais yuko upande wao, wanajiamini, kina Sabaya, Makonda ni mfano mwingine.

But inapofikia level ya Mfugale kutotii agizo la Waziri Mkuu, hii inakuwa imevuka mipaka yote, sijui Waziri Mkuu atakuwa anajisikiaje.

Ila nao ni vile waoga wa kuwajibika, kama unaoneshwa dharau za sampuli hiyo na mtu aliye chini yako kwa cheo, andika barua JIUZULU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Synthesizer,

Mi naona kuna tatizo kubwa zaidi kwanza kumekuwa na maagizo yanayotolewa kuwa ondoa mtu fulani pale au pale wakati huyo mtu kiutendaji haripoti kwa huyo anayeelekeza aomdolewe.

Utaratibu mtu kama utendaji wake una mapungufu yanaonekana na boss wake anayemsimamia sasa anapotokea kiongozi wa juu anaruka wasimamizi anakwenda kuondoa mtu ambaye siyo yeye anayemsimamia haieleweki ametumia utawalam gani kuona mapungufu ya mtu ambaye hasimamiwi na yeye na hivyo kuwajengea hofu watendaji wa chini bila sababu.

Kama Waziri Mkuu angekuwa yuko makini alitakiwa kumuondoa yule anayeripoti kwake moja kwa moja kuhusiana na hayo na kama hana mamlaka ya uteuzi wa huyo mtu angeweza kuelekeza mamlaka ya uteuzi lakini siyo kumwambia waziri ondoa yule pale kwani huyo Waziri hamuoni huyo mtu utendaji wake hadi asubiri kuelekezwa na Waziri Mkuu.

Hiwezekani kiongozi wa juu aniagize mimi nimfukuze msaidizi wangu wakati sioni mapungufu ya utendaji wake wa kazi na yeye bosi wangu hawezi kuona mapungufu ya msaidizi wangu yeye ataona mapungufu ya mimi na ana haki ya kuniwajinisha mimi kwa mapungufu anayoyaona na siyo kuniruka mimi na kuanza kuwajibisha mtu wa chini yangu Hiyo siyo sahihi.

Mimi kwa hili nasimama na Mfugale, nina imani litaondoa hofu kwa wafanyakazi wa Ngazi ya kati kufanywa kafara wa kila pungufu linapotokea wakati katika uhalisia hakuna mapungufu yoyote yanayokuwa yamenainishwa na viongozi wao isipokuwa kusema wanatekeleza maagizo kutoka juu kama vile kuna chuki tu binafsi kwa baadhi ya watendaji wa kati.
 
Back
Top Bottom