Mizengo Pinda: Wananchi wa Loliondo wanaohofia kuhamishwa, wasiwe na Wasiwasi (Machi, 2013)

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Salaamm Wakuu,

Hapa chini ni barua ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliyomuandikia Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati huo Magesa Mulongo, akitaka akawaondoe Wasiwasi Wananchi wa Loliondo wanaohofu kwamba Watahamishwa. Tuisome kwa Pamoja na tutafakari, je kulikuwa na Lazima ya kutokukaa meza na Wananchi ili kuwahamisha?

======

Mheshimiwa Magesa S. Mulongo,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, S. L. P. 3050, ARU S H A.

YAH: MGOGORO KUHUSU ENEO LA PORI TENGEFU LOLIONDO (LOLIONDO GAME CONTROLLED ÁREA)

Tafadhali husika na somo tajwa hapo juu.

Tarehe 19 Machi, 2013 Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, ilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu kusudio Ia kupunguza ukubwa wa eneo ia Pori Tengefu Ia Loliondo, kutoka Kilomita za Mraba 4,000 hadi

Lengo Ia Serikali Ia kutoa Tamko hilo ni kulinda mazalia ya Wanyamapori, mapito na vyanzo vya maji kwa ajili ya ustawi wa hifadhi kwa manufaa ya Wananchi wenyewe na Taifa kwa ujumla.

Aidha, kuhakikisha usimamizi endeievu wa Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro na Pori Tengefu Ia Loliondo kwa ajili ya Kizazi cha sasa na kijacho.

Kutokana na Tamko hilo, Wananchi wanaoishi katika Vijiji vilivyomo ndani ya Pori Tengefu Ia Loliondo ambao wamekuwa wakiishi katika eneo hilo kwa muda mrefu, hususan katika eneo Ia Kilomita za Mraba 1,500 ambazo Serikali iliamua ziendelee kubaki na hadhi ya Pori Tengefu wamepata hofu ya kuhamishwa na hivyo wametuma Wawakilishi mbalimbali kufika Dodoma kuniona ili kupata ufafanuzi wa Tamko hilo.

Kimsingi, Sheria ya Uhifadhi wa Aina mbalimbali za Wanyama (Fauna Conservation Ordinance) Sura ya 302 ya Mwaka 1951 ndiyo iliyoanzisha Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu Nchini. Sheria hii ilianzisha Mapori Tengefu 49 Nchini kwa Tangazo la Serikali.

Mwaka 1974, Sheria ya Hifadhi ya Wanyamapori ilianzishWa na kufuta Sheria ya awali ya Fauna Conservation Sura ya 302. Chini ya Sheria hizo mbili, masuala ya malisho na makazi hayakukatazwa katika maeneo ya Mapori Tengefu ikiwemo Pori Tengefu la Loliondo. Sheria hiyo ya Hifadhi ya Wanyamapori iliendelea kutumika hadi mwaka 2009 ambapo Sheria mpya ya Uhifadhi wa Wanyamapori (The Wildlife Conservation Act) Namba 5 ya Mwaka 2009 ilianzishwa na kufuta ile ya awali ya mwaka 1974.

Chini ya Sheria hii mpya ya Mwaka 2009, masuala ya malisho na makazi katika maeneo ya Mapori Tengefu yamezuiliwa, mpaka kwa kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori. Kutokana na masharti hayo ya Kisheria, Vijiji ambavyo awali vilianzishwa katika maeneo ya Mapori Tengefu vimejikuta katika hali ya kuvunja Sheria hiyo ya Mwaka 2009.

Kimsingi, Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya 2009 Chini ya Kifungu cha 16(1), Waziri mwenye dhamana na Uhifadhi wa Wanyamapori amepewa Mamlaka ya kutamka na kutangaza katika Gazeti la Serikali eneo lolote la Tanzania kuwa Pori Tengefu, baada ya kushauriana na Mamlaka husika za Serikali za Mitaa.

Aidha, Sheria hiyo Chini ya Kifungu cha 16(4) inamtaka Waziri husika, baada ya mwaka mmoja tangu kuanza kutumika kwa Sheria hiyo, kupitia upya Orodha ya Mapori Tengefu kwa madhumuni ya kudhibiti uhifadhi wa Wanyamapori katika maeneo hayo.

Pamoja na mamlaka hayo, kwa kuzingatia Kifungu cha 16(4), Kifungu cha 16(5) kinaelekeza kuwa, Waziri lazima ahakikishe kuwa hakuna ardhi yeyote ya Kijiji inayojumuishwa kwenye Pori Tengefu. Ingawa katika kutekeleza azma hii Waziri atazingatia maslahi ya uhifadhi wa Wanyamapori
kama ilivyoelekezwa na Kifungu cha 16(4) pale ambapo itabainika kuwa eneo fulani lina umuhimu wa kuendelea kubaki na hadhi ya eneo
lililohifadhiwa.

Pori Tengefu la Loliondo:

Pori Tengefu la Loliondo ni miongoni mwa Mapori Tengefu 49 yaliyopo Nchini, na ambalo lipo katika Ekolojia ya Arusha-Masai ikijumuisha Mapori mengine Tengefu ya Enduleni, Kitwai, Lake Natron, Lolkisale, Meserani Dam, Mto wa Mbu, Ngeju-Njiro Dam, Ngorongoro, Ruvu-Maasai, Simanjiro, n.k. Pori hili lipo katika Wilaya ya Ngorongoro yenye ukubwa wa Kilometa za Mraba 14,036 na idadi ya Wakazi wake ni 174,278. Wilaya ina jumla ya Tarafa tatu.

Tarafa hizo ni Tarafa ya Ngorongoro yenye ukubwa wa Kilomita za Mraba 8,300 wakati Tarafa ya Sale na Loliondo Zina ukubwa wa Kilomita za Mraba 5,736. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Tarafa ya Ngorongoro ina jumla ya Watu 70,084, Tarafa ya Sale ina jumla ya Watu 59,367; na Tarafa ya Loliondo ina idadi ya Watu 44,827.

Maeneo yanayohusika zaidi na mgogoro huu ni Tarafa ya Loliondo na Tarafa ya Sale. Tarafa ya Loliondo ina Kata nane ambazo ni Orgosorok, Enguserosambu, 01erien/Magaiduru, Soitsambu, Oloipiri, Ololosokwan, Arash na Maalon. Aidha, Tarafa hiyo ina Vijiji 25 na Vitongoji 85. Kwa upande wa Tarafa ya Sale ina jumla ya Kata 6 ambazo ni Samunge, Digodigo, Oldonyosambu, Sale, Pinyinyi na Malambo; Vijiji 14 na Vitongoji 45.

Aidha, Pori Tengefu la Loliondo linapakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa upande wa Magharibi, Pori Tengefu la Ziwa Natron upande wa Mashariki, Hifadhi ya Ngorongoro kwa upande wa Kusini na upande wa Kaskazini, Pori hili linapakana na Hifadhi ya Masai Mara iliyoko Nchi jirani ya Kenya.

Nimeelezwa kuwa, ndani ya eneo ambalo Serikali inapendekeza liendelee kubaki na hadhi ya Pori Tengefu la Kilomita za Mraba 1,500 kutokana na umuhimu wake kiuhifadhi, ndani yake Vipo Vijiji vilivyosajiliwa na Serikali. Kwa mujibu wa taarifa nilizozipata kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ni kuwa, jumla ya Vijiji sita (6) pamoja na miundombinu iliyopo katika Vijiji hivyo vitaathirika.

Kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2009, na Tamko la Waziri wa Maliasili na Utalii kuhusu kupunguza ukubwa wa eneo la Pori Tengefu la Loliondo kutoka Kilomita za Mraba 4,000 hadi 1,500, ni dhahiri kuwa Wananchi waliopo katika Vijiji vilivyo ndani ya Kilomita za Mraba 1,500 zilizotengwa kwa ajili ya uhifadhi kama nilivyovitaja, watatakiwa kuondoka katika maeneo hayo.

Kama utakavyoona, hapa ndipo penye tatizo kubwa.

Kimsingi, Vijiji vyote hivi vimeanzishwa na Serikali na kupewa hadhi ya kuwa Vijiji, ingawa kwa mujibu wa Sheria ilibidi ardhi hiyo iondolewe kwenye hadhi ya Pori Tengefu kwanza kabla ya kuanzisha Vijiji hivyo. Kwa msingi huo, Vijiji hivi vimekuwa ni makazi ya Watu na kuwa na miundombinu ya kudumu ya kutoa huduma kwa Jamii. Hivyo, zoezi zima linalotarajiwa kufanywa chini ya Tamko la Wizara, litakuwa na athari kwa Wananchi hao na ustawi wao.

Kutokana na hatua hiyo, Vijiji ambavyo vilianzishwa na vipo katika eneo hilo la Kilomita za Mraba 1,500 vimezua hofu ya kukosa eneo la malisho ya mifugo na eneo la kuishi baada ya kuishi hapo kwa miaka mingi kabla na tangu kuanzishwa rasmi kwa Vijiji hivyo.

Aidha, hofu ya kuharibiwa kwa hifadhi hiyo ipo pia kwa upande wa Serikali, na ndio maana Wizara ya Maliasili na Utalii imekuja na Mpango huu wa kuondoa eneo la Kilomita za Mraba 2,500 ili liwe nje ya Hifadhi na kusimamiwa na Wananchi wenyewe kwa kuzingatia Mpango endelevu wa Matumizi Bora ya Ardhi.

Pamoja na kwamba Tamko la Serikali lilitolewa kwa nia njema ya kuendeleza uhifadhi endelevu, kumejitokeza malalamiko kutoka kwa Wananchi wa Loliondo kwamba, Serikali ina Mpango wa kuwahamisha. Serikali imepokea mapendekezo mbalimbali kutoka kwa Wadau na Makundi mbalimbali ya Wananchi kutoka Loliondo wakiwemo Viongozi wa Wilaya, Halmashauri, Wazee wa Kimila, Akina Mama na Vijana kuhusu namna bora ya kuendeleza uhifadhi katika eneo hilo.

Makundi yote haya yameshauri kuwa eneo hilo
liendelee kumilikiwa na Wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia Taratibu za Kimila na Desturi za Jadi kulihifadhi.

Kimsingi, kama utakavyoona suala hili limeleta changamoto kubwa ambayo inahitaji tafakuri kubwa. Ni kutokana na changamoto hizo zinazojitokeza katika Mpango huu wa Wizara, Serikali imepokea mapendekezo hayo na kusikia kilio cha Wananchi hao ambapo inakusudia kupitià tena Mpango huo ili kuzingatia maoni hayo na kuwianisha na Sheria zilizopo bila kuathiri nia njema ya Serikali ya kuhifadhi na kutunza Pori hilo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Nia ya Serikali ni kuona kuwa, Mpango huo endelevu unaandaliwa kwa kushirikisha kikamilifu Wananchi wa maeneo hayo.

Kwa kuzingatia changamoto mbalimbali zilizojitokeza baada ya Tamko la Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu kupunguza ukubwa wa Pori Tengefu la Loliondo kwa kugawa eneo la kilometa za mraba 2,500 kwa Wananchi wa Loliondo na kubakiza eneo la kilometa za mraba 1,500 ambalo ni muhimu kwa uhifadhi wa wanyamapori, Serikali kwa sasa inafanya mambo yafuatayo:

i) Kupitia upya Tamko lililotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuzingatia Sheria zilizopo za Wanyamapori pamoja na zile za Ardhi;

ii) Kubaini miundombinu iliyopo katika eneo linalopendekezwa kubaki na hadhi ya Pori Tengefu; na
iii) Kuangalia changamoto zilizojitokeza kwa pande zote mbili (Wananchi na Serikali) kuhusu eneo hilo la Kilomita za Mraba 1,500 kuendelea kubaki na hadhi ya Pori Tengefu na kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kuendeleza uhifadhi katika Pori la Loliondo kwa kuwashirikisha Wananchi.

Wakati Serikali ikiendelea na hatua hizo, inaomba Wananchi waliomo ndani ya Pori hilo la eneo la Loliondo waendelee kuvuta subira wakati Serikali ikiendelea kukamilisha mazungumzo ya ndani kuhusu suala hili.

Lengo la kukuandikia barua hii ni kukutaka kufikisha taarifa na maelekezo haya ya Serikali kwa Wananchi wanaoishi ndani ya Pori Tengefu la Loliondo ili waweze kuelewa Azma ya Serikali na kuondoa waSiwasi uliopo kwa Wananchi wa Loliondo, na kwamba hatua zozote zitakazochukuliwa zitawashirikisha kikamilifu.

Nakutakia kazi njema.
Izengo P. Pin&a (Mb.) WAZIRI MKUU
Nakala:
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, IKULU,
DAR-ES-SALAAM.
Mheshimiwa Balozi Khamis S. Kagasheki (Mb.), Waziri wa Maliasili na Utalii, BUNGENI - DODOMA.
Balozi Ombeni Y. Sefue,
Katibu Mkuu Kiongozi,
IKULU,
DAR-ES-SALAAM.
Bw. Peniel M. Lyimo, Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu, S. L. P. 3021,
DAR-ES-SALAAM.
Mheshimiwa Elias Lali, Mkuu wa Wilaya, Wilaya ya Ngorongoro,
NGORONGORO.
Mheshimiwa Kaika Saning'o Telele (Mb.), Mbunge wa Ngorongoro, BUNGENI - DODOMA.
Mheshimiwa Elias Ngorisa,
Mwenyekiti,
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro,
NGORONGORO.
 
Attachments

  • Barua ya Waziri Mkuu.pdf
    4 MB · Views: 9
Serikali imebatilisha msimamo huu??.

Na nini kimepelekea yote haya??

Je ndio tuseme rupia zimebadili msimamo huu wa serikali??
 
Ninachomshukru zaidi MUNGU, siku zetu sote si nyingi hapa duniani. Ukitenda wema utavuna mema na ukitenda mabaya kiyama kinakuja. Tupendane ndugu zangu huku tukiishi maisha ya kumpendeza MUNGU na wanadamu.

MUNGU ibariki Tanzania, MUNGU tubariki wapenda amani, upendo na kuwasaidia wahitaji.
 
Ifahamike pia kuwa, Roliondo Si Ngorongoro.

Roliondo Mzee wa ruksa, Ngorongoro ni huyu Chui Jike.
 
Ninachomshukru zaidi MUNGU, siku zetu sote si nyingi hapa duniani. Ukitenda wema utavuna mema na ukitenda mabaya kiyama kinakuja. Tupendane ndugu zangu huku tukiishi maisha ya kumpendeza MUNGU na wanadamu.

MUNGU ibariki Tanzania, MUNGU tubariki wapenda amani, upendo na kuwasaidia wahitaji.
Mwarabu wana-enjoy balaa huku sisi tunapigana
 
We boya njoo huku joto la jiwe
 
Barua iko vizuri, na katika uamuzi uliofikiwa sijaona kilichobadilishwa. Eneo la hifadhi lilikuwa 4,000 sq km, serikali ikalipunguza hadi 1,500 sq km kwahiyo hizo 2,500 sq km zimebaki kwa wananchi, ni zaidi ya win-win situation kwa upande wa wananchi.
 
Mungu ibariki JF
 
Back
Top Bottom