Waziri mkuu mwanataaluma wa sheria kama fani uliyoisomea utatuambia nini juu ya hili?

Kagemro

JF-Expert Member
Jan 11, 2010
1,433
633
Watanzania wenzangu,

Siyokwamba nayaandika haya nikiwa napenda,lakini ninaona jinsi Nchii hii inavyoongozwa na Wanataaluma wasiojua kutumi fani zao pale inapotakika.

Najua Waziri Mkuu ni mwanasheria Mzuri kama Fani aliyoisomea,na tukirudi nyuma na kukumbuka swali alilouliza Mhe Mboye lilijikita juu ya Mauwaji ya raia kwa kutumia risasi na akasisitiza mifano ya Arusha na Mbarari.Mwisho aliomba Kauli ya serikali.

Lakini katika maelezo ya waziri Mkuu alipokuwa akijibu swali alisisitiza kuwa Chadema ndio wa kulaumiwa kwa kufanya maandamano na ndiyo yaliyopelekea vifo vya ndugu zetu.

Waziri Mkuu kesi ya viongozi wa Chadema iliyoko mahakamani ni kesi ya KUfanya maandamano kinyume na sheria,makubaliano.

Nachoshangaa Mwanasheria huyu kwa kauli yake hakutambua kama amewahukumu viongozi wa Chadema tayari kwa taarifa yake?

Na jambo hili limefanyika kwa mara tatu mfululizo.


  1. Taarifa ya Habari Maelezo iliyoonyesha picha za video na kusisitiza Chadema ndiyo wakulaaumiwa.
  2. Jakaya Mrisho kikwete wakati akiwahutubia wanachama wa CCM tarehe 5/02/2011.Sherehe zilizorushwa mojakwamoja katika runinga ya TBC
  3. Waziri Mkuu Wakati anajibu swali la Mhe Mboye.
Hukumu hizi zilizotolewa nje ya mahakama zinaukweli gani iliwa (Proscutor) Mpelelezi wa kesi inayowahusu viongozi wa Chadema juu ya swala zima la Arusha amekiri mara mbili mahakamani Uchunguzi bado haujakamilika.

Serikali (wakiwamo viongozi wa juu Pinda na Kikwete) hii imetoa wapi taarifa ambazo zinaonyesha moja kwa moja kuwa Chadema ndio wa kutuhumiwa?

Mhe Pinda kulingana na maelezo yako kama kiongozi Mkubwa wa Serikali,Mahakama haipaswi tena kuendelea kuidanganya umma kuwa Upelelezi bado unafanyika na badala yake hukumu itolewe.

NI KWANINI UMEWEZA KULIZUNGUMZIA HILI LILILOKO MAHAKAMANI NDANI YA BUNGE NA KULITOLEA HUKUMU NAWAKATI HUOHUO MMEWEZA KUZUIA HOJA YA DOWANS ISIZUNGUMZIKE NDANI YA BUNGE.
 
siasa za ccm hatuangalii unyeti wa jambo linalozungumziwa tunazingatia ni jinsi gani tutajisafisha na uovu unaotuhusu. "pale muheshimiwa Pinda hakujibu kama serikali amejibu kiccm"
 
Back
Top Bottom