JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,321
- 5,493
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Elikana Balandya awasimamishe kazi watumishi wawili wa Jiji la Mwanza huku akiagiza Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa huo arudishwe wizarani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Ameagiza ujenzi wa ghorofa uliositishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Amos Makalla uendelee kwenye viwanja namba 194 & 195 kitalu ‘U’ Rwagasore, jijini Mwanza na wamiliki wa viwanja hivyo wakabidhiwe hati zao kama alivyokuwa ameelekeza awali.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Oktoba 3, 2023) kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma cha viongozi wa majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Tanga na Dodoma ili kujadili migogoro ya ardhi iliyokithiri kwenye majiji hayo.
“Ninaagiza Katibu Tawala wa Mkoa wasimamishe kazi Mkuu wa Idara ya MipangoMiji, Bw. Robert Phares na Afisa Mteule na Mkuu wa Kitengo cha Ardhi katika Jiji la Mwanza, Bi. Halima Iddi Nasoro. Na Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi (Mwanza), Bw. Elia Kamihanda arudishwe makao makuu na achukuliwe hatua za kinidhamu.’’
Chanzo: Ofisi ya Waziri Mkuu