CCM haina Shaka na Utendaji wa Waziri Mkuu Majaliwa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakina shaka na utendaji kazi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwakuwa ni kiongozi Mchapakazi na Mtiifu.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi Paul Makonda amesema hayo leo Alhamisi, November 02, 2023 alipokwenda ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema lengo la Chama ni kuhakikisha ndoto ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwatumikia na kuwaletea maendeleo Wananchi wote hususani wanyonge inafikiwa.

Makonda amesema “Katika utendaji wa kazi sisi upande wa Chama tuna matumaini makubwa na uwajibikaji na uaminifu wa Waziri wetu Mkuu Kassim Majaliwa, tumemuona katika maeneo mengi akisimamia shughuli mbalimbali za Serikali na nilipotoa agizo la Chama kwa Waziri Mkuu nilitaka agizo hilo lifike kwa Mtu anayeweza kuleta matokeo chanya kwa Chama.”

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema Serikali imepokea maelekezo ya Chama na kwamba itaendelea kuyafanyia kazi na kuhakikisha migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini inaendelea kushughulikiwa.

#MillardAyoUPDATES
 
CCM haigawanyiki. Lengo ni kuendelea kushika dola. Lengo linafanikiwaje sijui ila majeruhi wa kisiasa watakuwepo na hatimaye tutarudi pale pale kwa wahenga "hakuna rafiki wala adui wa kudumu kwenye siasa." Mh. Waziri Mkuu ana hekima nyingi,amepokea maelekezo ya Chama yaliyopita kwa KIU wa Chama.
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakina shaka na utendaji kazi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwakuwa ni kiongozi Mchapakazi na Mtiifu.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi Paul Makonda amesema hayo leo Alhamisi, November 02, 2023 alipokwenda ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema lengo la Chama ni kuhakikisha ndoto ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwatumikia na kuwaletea maendeleo Wananchi wote hususani wanyonge inafikiwa.

Makonda amesema “Katika utendaji wa kazi sisi upande wa Chama tuna matumaini makubwa na uwajibikaji na uaminifu wa Waziri wetu Mkuu Kassim Majaliwa, tumemuona katika maeneo mengi akisimamia shughuli mbalimbali za Serikali na nilipotoa agizo la Chama kwa Waziri Mkuu nilitaka agizo hilo lifike kwa Mtu anayeweza kuleta matokeo chanya kwa Chama.”

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema Serikali imepokea maelekezo ya Chama na kwamba itaendelea kuyafanyia kazi na kuhakikisha migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini inaendelea kushughulikiwa.

#MillardAyoUPDATES
Hili jamaa ni pumbavu!
 
Hiyo ni kama funika kombe mwanaharamu apite. Jana maagizo yanatoka kwa "boss lady" ofisi ya PM ipewe pia ofisi ya naibu PM, leo tunamsikia muenezi mpya tofauti kabisa na mienendo na matamko ya wale waliomtangulia akithubutu kutoa maagizo hadharani kwa PM na hata kumpa "ultimatum".

Kesho unatarajia nini ambacho kinatarajiwa kutokea!? Wachezaji hawa wawili wa "substitution" ya lala salama, wameletwa kama "game changer" lakini sioni "impact" yoyote ile kubwa tuelekeapo 2024/25.

Nafasi ya PM ndani ya CCM toka wakati wa Kambarage ni ya lawama na dodoki la kumsafishia Rais kwa madudu anayofanya. Katika hili la kutatua migogoro ya ardhi nchini ikiwemo ya ardhi ya Wamaasai litakwenda na Majaliwa.

Madudu yote ambayo yamefanyika katika kupora ardhi na kupewa wawekezaji wa kigeni ikiwemo Ngorongoro atatwishwa PM kwa kisingizio cha kutoa ushauri mbaya mpaka hayo yote yakatokea. Leo mwenezi anamuita mchapa kazi na mtiifu, lakini anakwepa kwa makusudi kuitaja sifa ya uadilifu.
 
Hili tukio la Katibu wa Itikadi na Uenezi Comrade Makonda kwenda kuonana na Waziri Mkuu ni Maagizo toka ngazi ya juu au viongozi wengine wenyewe hekima na busara.
-Maagizo ya CCM hufanywa na vikao au MwenyeKiti wa Chama kwa kushauriana na makamu wake wawili.
-Makonda anaposema Chama kimempa PM miezi 6 kumaliza migogoro ya ardhi,ingependeza kama angetaja ni kikao gani Chama kilichokaa kutoa maagizo hayo (Maagizo hufanywa kwa kurejea vikao-best practice).
  • Wajumbe wa Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wanafahamu kuwa kuna baadhi ya migogoro ya ardhi ipo Mahakamani na suala ambalo lipo Mahakamani haliingiliwi
  • Aidha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM anaposema Chama kimeagiza, anamainisha MwenyeKiti wa Chama na makamu wake wawili ndiyo ambao wametoa Maagizo hayo kwa Waziri Mkuu.
Ushauri
-Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ayaendee Majukumu yake kwa hekima na busara ili kuleta umoja na mshikamano ndani na nje ya Chama.
- Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM afanye kazi kwa mujibu wa Job description zake,na hayo mambo yao ndani kati ya muuza duka na mwenye duka,wayajadili kwenye vikao vyao vya ndani.
-Mambo ya chumbani hayaletwi hadharani.
 
Back
Top Bottom