Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afika Kariakoo. Aagiza task force za TRA kusitisha shughuli zake haraka

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameamua kukutana na kuongea na Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo leo ambapo tayari amefika Kariakoo muda huu badala ya Jumatano May 17,2023 ambayo ilitangazwa hapo wali hii ni kutokana na uzito wa suala hilo.

Awali mkutano kati ya Waziri Mkuu na Kamati ya Wafanyabiashara hao pamoja na TRA na Mawaziri wa Sekta husika ulitarajiwa kufanyika saa 8 Mchana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni-Ikulu Dar es salaam Jumatano May 17, 2023 kwa uratibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala, lakini Waziri Mkuu ameamua aende leoleo Kariakoo.
---
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kusikiliza kero za Wafanyabiashara wa Kariakoo leo ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufuta Vikosi Kazi (Task Forces) ambavyo amesema vinatumika kufanya kamatakamata na wakati mwingine kuchukua rushwa.

Waziri Mkuu Majaliwa akiwa Kariakoo jioni hii amesema “Tuna taarifa kuwa kuna kikosi kazi kimeundwa kinazunguka huko, Rais alikemea Vikosi Kazi (Task Forces) kwasababu vinatumika kuwasumbua Wafanyabishara na kuomba pia rushwa, naagiza hiyo Task Force isitishwe mara moja”.

“Task force hii ndio inaendesha kamatakamata kila siku, Kamishna wa Mapato ya Ndani TRA naagiza isitishwe, kanuni zipo sheria zipo zinatuelekeza namna ya kulipa kodi, kamatakamata hii inafukuza Wafanyabiashara Kariakoo na mbaya zaidi mnawakamata hadi Wageni kutoka nje”.

AWASHANGAA TRA kukaidi maagizo ya Rais
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshangazwa na Watumishi wa ngazi za chini wakiwemo wa TRA kukaidi maagizo ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, wakisema ni maagizo ya kisiasa tu ambapo amesema wakimbaini anayetoa majibu hayo atachukuliwa hatua.

Akiongea na Wafanyabiashara wa Kariako leo Waziri Mkuu ameshangazwa na wanaodharau kauli za Viongozi Wakuu wa Kitaifa “Akitokea Mtu anasema lazima ulete barua ya agizo lililotolewa na Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu, mtuletee huyo Mtu, Rais,Makamu wa Rais na Waziri Mkuu hawaandiki barua, wataandika barua ngapi?”

“Rais na Makamu wa Rais wanapoagiza sisi wa chini tunatekeleza, leo TRA Rais amesema kodi za miaka mitano mziache, nyie mnadai barua kwa Watu wa Kariakoo hivi Mfanyabiashara wa Kariakoo atapata wapi barua ya Rais? halafu unamwambia Mfanyabiashara hilo ni agizo tu la kisiasa, yaani agizo lililotolewa na Rais unasema ni la kisiasa hiyo ni dharau na natamani ningemjua aliyesema hivyo tumchukulie hatua”.

Awaomba wafanyabiashara kufungua maduka yao

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba Wafanyabiashara wa Kariakoo kusitisha mgomo na kufungua maduka yao huku akiagiza TRA kuacha kuwaonea Wafanyabiashara.

Akiongea na Wafanyabiashara wa Kariakoo leo, PM Majaliwa amesema “Nimeacha Bunge nimewafuata kuja kujua kuna nini!? Soko la Kariakoo tunalitegemea kutuingizia mapato ni lazima tulitulinze , nimesoma mabango yenu moja baada ya moja, kuna linalosema “TRA mmefukuza Wageni’ , mmeongelea EFD n.k, hakuna jambo mtalifanya tutalichukulia rahisirahisi”

“Tabia ya kuonea Wafanyabiashara ikome mara moja, hii ya kukusanya tu mnakusanya tu mpaka damu itoke hii sio sawa, wengine mnawazidishia kodi ili mkae nao chini muwaombe rushwa na hii rushwa inafanya Wafanyabiashara watoe hadi pesa zao za mauzo”

“Wafanyabiashara sikieni ombi la Serikali fungueni maduka yenu na matatizo yote keshokutwa tunayajadili keshokutwa, ningeweza kusema kesho lakini Mh.Rais amenituma kumwakilisha kwenye maziko ya Mh. Membe acha niende kesho asubuhi, ilitakiwa niende leo nimeghairi naenda asubuhi kesho nazika narudi tutatue matatizo”.

Pia Soma:
- News Alert: - Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023
 
Biashara kkoo ndo UTI wa mgongo wa uchumi wote bila hivyo hatupati posho so serikali hatuwezi kufanya mchezo hapo lazima tuwe wapole tuyajenge lakini pia TRA HAWATAKUBALI KULEGEZA KIHIVO MAANA LAZIMA UCHUMI UYUMBE..LIPENI KODI NYIE MATAJIRI ACHENI HIZO
 
Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa muda huu anaelekea Kariakoo kukutana na wafanyabiashara. Tukio litakuwa live TBC
FB_IMG_1684142099561.jpg
 
Biashara kkoo ndo UTI wa mgongo wa uchumi wote bila hivyo hatupati posho so serikali hatuwezi kufanya mchezo hapo lazima tuwe wapole tuyajenge lakini pia TRA HAWATAKUBALI KULEGEZA KIHIVO MAANA LAZIMA UCHUMI UYUMBE..LIPENI KODI NYIE MATAJIRI ACHENI HIZO
Una mavi kichwani wewe sio bure

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom