jaribu kupitia post zote za thread hii utapata majibu, fuatilia na thread "jk awekwa kikaangoni na ma dr."Kauli hii sio kweli sana Matola. Hebu nielimishe kidogo kuhusu yafuatayo:
-Uhusiano wa mojakwamoja wa kikazi kati ya madaktari hawa na waziri wa afya au naibu wake.
-Waziri na naibu wake kwa upande mmoja na madaktari upande mwingine na kati yao kuna wagonjwa wanaohitaji huduma.
-Kama leo hii madaktari wakifanikiwa kushinikiza waziri aondoke au aondolewe kesho watashindwa kufanya hivo kwa WAZIRIMKUU, RAIS?
-Hili shinikizo limekaa KITAALUMA kweli?
-MaDaktari wanatumiwa au kutumika kisiasa? Wanawaumiza WATANZANIA masikini kwa kuwa Dr Mponda hataki kung'oka?
-Ni taaluma hii peke yake iliyonyeti nchi hii? Polisi, DAWASCO, TANESCO, TRA,..., wakigoma kwa staili na mtindo huu je?
Namwomba Rais wetu asiyaendekeze haya. Tuchukue madaktari kutoka Cuba, China au kungineko kwa gharama yoyote ile.