Waziri Mkuu asikitishwa na maazimio ya madaktari

Tatizo Madaktari nao wanajichanganya dai lao kuu halieleweki, maslahi yao au Mawaziri wajiuzulu?
sikiliza wewe

chanzo cha mgomo ni mponda na Lucy na Blandina.... bado wapo, serikali ilijicommit, haijafanya

sasa unategemea nini, kama umezoea kupigwa fix, basi kakojoe ulale
 
Tatizo Madaktari nao wanajichanganya dai lao kuu halieleweki, maslahi yao au Mawaziri wajiuzulu?
Nadhani wewe ndiye uliyechanganyikiwa! Ili uweze kuchangia vizuri ulitakuwa kujua background ya mgogoro mzima na siyo kudandia!
 
Hahusiki vipi? huona kwamba hili suala lina "concern" ya watanzania wote?

ni kweli kk hili suala ni la watz wote, lakini je mtazamo wako unautoa kuanzia wapi?? usidandie mada kama hujui chanzo chake na kama hutaki mabadiliko ya sera zetu za nchi na uwajibikaji, basi kaa pembeni ili walio tayari kupambana wapambane kwa ajili yako!!!!
 
Hata hivyo, wakati Pinda akieleza kusikitishwa na hatua hiyo mpya ya madaktari, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya alisema hawezi kujiuzulu kama madaktari hao wanavyotaka kwa kuwa suala hilo liko nje ya uwezo wake."Hivi sasa siwezi kuzungumza chochote kwa kuwa suala hilo liko juu yangu na siwezi kujiuzulu," alisema Dk Nkya.
Source:Pinda: Madaktari wananisikitisha paragraph ya saba.

MY TAKE:

Nilidhani kujiuzulu ni kitu personal kuonesha kama umekerwa na umeguswa na tukio Fulani.Sasa huyu mama kujiuzuru anataka aaambiwe jiuzuru badala ya yeye kupeleka barua JK aendorse.
Ama kweli mawaziri tunao au JK atakuwa kamwambia komaa mama nguvu ya soda iyo!
Viongozi maslahi hawa!
 
Pinda unasikitika kweli au ni unafiki, makubaliano mloafikiana na madaktari kwanini hadi leo hayajatekelezwa, na nyie mawaziri wa afya kwanini hamjiudhuru au mnaona nyie wasamani sana kuliko maelfu ya madaktari na wagonjwa mahospitalini. Chukueni hatua haraka kabla ya mgomo kuanza, kwani madhara yake ni makubwa hivyo yaepusheni kwa kujiudhuru
 
eeh mungu tunusuru na hawa kina pinda, maana sielewi ni vilaza, mafedhuli, wavivu au uwezo wao kufikiri umefikia ukomo. unasikitikaje wakati hujatimiza makubaliano, hebu tuwe siriasi kidogo ndugu pinda, mzaha wako unaumiza wazee wako mpanda kijijini.
 
It stands to reason that health sector grievances will not abruptly come to a halt by merely getting rid of Mponda and Nkya at the Ministry. There exists separate assortment of issues demanding solutions with regard to problems facing the sector and that has got nothing to do with those two officials. Sadly, this crisis has apparently been usurped by special interests people who attempt to spin the issue to make it look like something political and therefore fulfilling their desire for setting the government against its own citizens.
 
What happen to Mwita 25 id? doesn't sound good for a male to use a Female ID.
 
wanashughulikia kwa muda gani? Na walikubaliana watatue matatizo kwa muda gani? Na yasipotekelezwa walikubaliana wafanye nini?
 
Tatizo Madaktari nao wanajichanganya dai lao kuu halieleweki, maslahi yao au Mawaziri wajiuzulu?

madai yote yapo, na mengine hayatatekelezwa na waziri ambaye amekataliwa. Kutakuwa na ulipaji wa visasi katika utekelezaji.
 
Madaktari watangulize uzalendo mbele waache papara na tamaa.
OK umenena, UZALENDO. Sina uhakika kama umeconsult kamusi yako ujue maana ya neno UZALENDO

Je, madaktari kudai uboreshwaji wa mazingira ya kazi na vifaa tiba kwako wewe si uzalendo?

Je, madaktari kukataa kuwa mashuhuda wa vifo vinavyozuilika na kutibika (mf vifo vya kinamama vitokanavyo na ujauzito/uzazi )kwa serikali kuwajibika ktk kuweka vitendea kazi kwako wewe huo si uzalendo?

Je serikali kupitia WM Pinda kuahidi madaktari na umma kwa ujumla kwamba viongozi wa kisiasa na watendaji wa wizara watawajibisha and then hatuoni utekezaji wake ndani ya muda walokubaliana kwako wewe madaktari watakuwa hawana uzalendo?

Ndugu yangu mtanzania mwenzangu funguka. Tuwaunge mkono madaktari ktk kuiwajibisha serikali ambayo inajisahau kupita maelezo

Hiyo J5 kama hao mabwana wakubwa wataendelea kuwepo ofisini na madaktari wakagoma basi mimi na wewe na wananchi wote kwa ujumla popote walipo nchi hii hatutakuwa na namna bali kuingia barabarani na kuandamana kudai haki yetu ya kikatiba ya kupata huduma za Afya na hivyo kuendelea kuishi.

Hatutakuwa tayari kuona even a single life is once again being lost kisa watu 2 wawekataa kuwajibika. That's a BIG NO

Kwangu mimi madaktari na WAZALENDO wa kuigwa mfano
 
pinda amepinda, na hata maneno yake yamepinda,
jana nilicheka nilivyocheki kibonzo cha wiki mlimani TV, pinda anahutubia kuhusu matumizi bora ya lugha ya kiswahili bila hata aibu anaongea kiswanglish, PINDA KAPINDA NA KAULI ZAKE ZIMEPINDA. nchi inaongozwa na magazeti siku nyingi, hatuna viongozi wenye kauli mda mrefu sana.
Mi inasikitisha sana kwamba tunamaliza muongo mmoja bila viongozi hasa rais....ndio hatuna tuna wajanja wajanja flani wanatupeleka peleka tu ili mradi tumalize hii nngwe... basi tuanze upya
 
tatizo nchi hii inaendeshwa kihuni kila kitu ooo tupo kwenye mchakato!!!michakato gani isiyoisha???upuuzi mtupu wanaufanya..ningekuwa pinda ningeanza kujiuzulu
 
huyu pinda naye kapinda kweli, yeye ni mtu wa kusikitika tu kwani kaambiwa watanzania wanataka mtu wakuwasikitikia? Mara alie mara ahuzunike sisi hatutaki ujinga huo tunataka uamuzi wa busara sio kusikitika mimi ananikera sana huyu bwana kusikitika mnafiki sana hana msimamo
 
Jambo moja muhimu ambalo serikali hii na wapambe wake wanatakiwa kuelewa ni kuwa; Ikiwa wakati ule wananchi waliwaelewa madaktari na hawakupumbazwa na propaganda za ccm na serikali yake, wasijidanganye kuwa wakati huu huo upuuzi wanaouita propaganda utafua dafu. Wananchi wameujua ukweli na hakuna atakayedanganyika wakati huu... Mwenye sikio la kusikia huko serikalini na asikie...
 
Wewe ndio hueleweki, binadamu wote wanaotumia ubongo kufikiri tunayafahamu vyema madai ya madaktari, wasioyafahamu madai ya madaktari ni wale tu wanaotumia viungo vingine kufikiri.

420512_10150575550606156_687191155_9648383_353347232_n.jpg
Kauli hii sio kweli sana Matola. Hebu nielimishe kidogo kuhusu yafuatayo:
-Uhusiano wa mojakwamoja wa kikazi kati ya madaktari hawa na waziri wa afya au naibu wake.
-Waziri na naibu wake kwa upande mmoja na madaktari upande mwingine na kati yao kuna wagonjwa wanaohitaji huduma.
-Kama leo hii madaktari wakifanikiwa kushinikiza waziri aondoke au aondolewe kesho watashindwa kufanya hivo kwa WAZIRIMKUU, RAIS?
-Hili shinikizo limekaa KITAALUMA kweli?
-MaDaktari wanatumiwa au kutumika kisiasa? Wanawaumiza WATANZANIA masikini kwa kuwa Dr Mponda hataki kung'oka?
-Ni taaluma hii peke yake iliyonyeti nchi hii? Polisi, DAWASCO, TANESCO, TRA,..., wakigoma kwa staili na mtindo huu je?
Namwomba Rais wetu asiyaendekeze haya. Tuchukue madaktari kutoka Cuba, China au kungineko kwa gharama yoyote ile.
 
Naomba nikujibu tu kwa kifupi, ni kwamba hawa maziri ndio chanzo cha mgogoro huu kufikia hapa ulipo, hili swala lilikuwa ndani ya uwezo wao na kama una kumbukumbu nzuri ni kwamba chokochoko ziliznzia kwa Interns Doctors, swali kwako je ni kweli Serikali haikuwa napesa za kuwalipa posho zao Interns Doctors?
Pili siku zote kuna CONFLICT RESOLUTION je unawezaje kukaa meza moja kusuruhisha tatizo hili meza moja na watu wale wale waliowapuuza Madaktari na kuipotosha Serikari?

Mkuu Waberoya binafsi mimi nilikuwa muhanga wa mgomo ule, Namuuguza mama yangu mzazi huu sasa ni mwezi wa pili, nashukuru Mungu ameshafanyiwa oparesheni pale MOI lakini bado anahudhuria clinic, ni mpumbavu tu peke yake anayeweza kuwapuuza Madaktari, otherwise labda neno hospital uwe unalisoma tu kwenye keyboard.
I strong support our doctors regardless i be will among of victims.
 
Back
Top Bottom