Waziri Mkuu asikitishwa na maazimio ya madaktari

Lyimo

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,826
2,017
Kufuatia kikao cha madaktari kilichoazimia kuendelea na mgomo waliousitisha ifikapo jumatano (7/03/2012) kwa kutotekelezwa baadhi ya makubalionao walioafikiana na serikali chini ya Waziri mkuu Mizengo Pinda.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema amesikitishwa na tishio hilo akisema kwa sasa Serikali ipo katika mchakato wa utekelezaji wa makubaliano mbalimbali na wanataaluma hao.

Source: Mwananchi 5/03/2012

Swali la msingi:

Ni kweli serikali imeshindwa kuendelea na mchakato huo wakati ikiwa imewawajibisha Mawaziri husika kama walivyokubaliana? Kwananmna hiyo basi, mawaziri hawa waliopelekea matatizo yaliyo pita watakuwa wanashiriki katika mchakato huo ambapo Madaktari na sisi wananchi tukiwa hatuna imani na viongozi hao. Inatuwia vigumu sana kuona Mh. Pinda unasikitishwa na maazimio ya Madaktari mlioafikiana awali.
 
ahadi za uongo kwa madokta ili kuzima moto,lakini madokta wameligundua hilo,..misimamo ya madokta sio ya walimi.pinda get that to your zero head.
 
pinda amepinda, na hata maneno yake yamepinda,
jana nilicheka nilivyocheki kibonzo cha wiki mlimani TV, pinda anahutubia kuhusu matumizi bora ya lugha ya kiswahili bila hata aibu anaongea kiswanglish, PINDA KAPINDA NA KAULI ZAKE ZIMEPINDA. nchi inaongozwa na magazeti siku nyingi, hatuna viongozi wenye kauli mda mrefu sana.
 
Mzee wangu Pinda kinachokusikitisha nini sasa kama makubaliano mliyo afikiana nao hayajatimizwa na muda mliopeana umefika?lawama lazima ziwaangukie serikali kwa kushindwa ku play role yenu na wala si madaktari!epukeni kuwalinda watu wabovu
 
Maamuzi magumu yenye manufaa kwa wananchi hayawezwi fanywa na viongozi wetu ktk serikali legelege km yetu ambayo uongozi upewa kiswahiba. Pinda hamuumizi alijua ni enzi za kudanganya watu na kupotea sasa ni kipindi cha mabadiliko na wananchi wamechoka na utawala wa uswahiba na viburi vya watawala wao.
 
Kufuatia kikao cha madaktari kilichoazimia kuendelea na mgomo waliousitisha ifikapo jumatano (7/03/2012) kwa kutotekelezwa baadhi ya makubalionao walioafikiana na serikali chini ya Waziri mkuu Mizengo Pinda.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema amesikitishwa na tishio hilo akisema kwa sasa Serikali ipo katika mchakato wa utekelezaji wa makubaliano mbalimbali na wanataaluma hao.

Source: Mwananchi 5/03/2012

Swali la msingi:

Ni kweli serikali imeshindwa kuendelea na mchakato huo wakati ikiwa imewawajibisha Mawaziri husika kama walivyokubaliana? Kwananmna hiyo basi, mawaziri hawa waliopelekea matatizo yaliyo pita watakuwa wanashiriki katika mchakato huo ambapo Madaktari na sisi wananchi tukiwa hatuna imani na viongozi hao. Inatuwia vigumu sana kuona Mh. Pinda unasikitishwa na maazimio ya Madaktari mlioafikiana awali.

kwani madaktari wanadai maslahi yao au wanachodai ni Mawaziri wajiuzulu? Mbona hawaeleweki, wamekuwa wanasiasa?
 
Pinda ameshaanza kujenga mazingira ya serikali kuonewa huruma, wakati serikali haitaki kutekeleza sehemu yake ya wajibu!
Tatizo Madaktari nao wanajichanganya dai lao kuu halieleweki, maslahi yao au Mawaziri wajiuzulu?
 
Hata hivyo, wakati Pinda akieleza kusikitishwa na hatua hiyo mpya ya madaktari, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya alisema hawezi kujiuzulu kama madaktari hao wanavyotaka kwa kuwa suala hilo liko nje ya uwezo wake.“Hivi sasa siwezi kuzungumza chochote kwa kuwa suala hilo liko juu yangu na siwezi kujiuzulu,” alisema Dk Nkya.
Source:Pinda: Madaktari wananisikitisha paragraph ya saba.

MY TAKE:

Nilidhani kujiuzulu ni kitu personal kuonesha kama umekerwa na umeguswa na tukio Fulani.Sasa huyu mama kujiuzuru anataka aaambiwe jiuzuru badala ya yeye kupeleka barua JK aendorse.
Ama kweli mawaziri tunao au JK atakuwa kamwambia komaa mama nguvu ya soda iyo!
 
kwani madaktari wanadai maslahi yao au wanachodai ni Mawaziri wajiuzulu? Mbona hawaeleweki, wamekuwa wanasiasa?
Mkuu kasome maazimio yaliyofikiwa kwenye mkutano kati ya Madaktari na Waziri mkuu vinginevyo hutaweza kuelewa kama huungi matukio!!
Haki ya nani hii serikali kweli ni kimtandao, na iko kulindana hadi presha izidi ndiyo inafanya cha maana.
 
Haya ni matokeo ya kufuja rasilimali za nchi. Sasa wakati umefika wa kulipia ile ziada ya mrahaba wa asilimia 3% kwenye madini. Mnawafanya watu wajinga mno, lakini njia ya uongo ni fupi.
 
kwani madaktari wanadai maslahi yao au wanachodai ni Mawaziri wajiuzulu? Mbona hawaeleweki, wamekuwa wanasiasa?

Ni wewe tu (na wenye malengo kama yako) ndio mnajifanya hamuelewi. And in any case haikuhusu, waache wenye madai yao wayadai Muda wa propaganda ulishaisha kitambo, sijui nyie watu ni lini mtaukubali ukweli huu?
 
Hahusiki vipi? huona kwamba hili suala lina "concern" ya watanzania wote?
 
Tatizo Madaktari nao wanajichanganya dai lao kuu halieleweki, maslahi yao au Mawaziri wajiuzulu?
Wewe ndio hueleweki, binadamu wote wanaotumia ubongo kufikiri tunayafahamu vyema madai ya madaktari, wasioyafahamu madai ya madaktari ni wale tu wanaotumia viungo vingine kufikiri.

420512_10150575550606156_687191155_9648383_353347232_n.jpg
 
ngeleja bado ni waziri mpaka leo,nchi hii kulindana kisa mnacheza wote disco diomond jubilee
 
Ni muhimu hao mawaziri waondoke kwanza ndipo majadiliano yaendelee. Tokea mwanzo wizara haikuwa tayari kuyashughulikia matatizo ya madaktari na ushahidi ni taarifa ya Mponda Bungeni. HAKUWA NA NIA YA KUHANGAIKIA MADAI YAO. Hivyo ni vigumu kujadiliana na mtu asiye na nia ya kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom