Waziri Mkuu amelidanganya bunge na watanzania wote

...nimepitia hiyo taarifa ya kilichotokea huko Arusha, kwa kweli inatia huzuni sana kwa ''ubakaji'' wa madaraka uliofanywa na hao CCM! On the other hand sielewi huyu Pinda kama taarifa za kintelijensia huwa zinamfikia au la na kama huwa zinamfikia kama zilivyo (bila uchakachuaji), naamini hata hizi zilimfikia.....the real ones! Ivi haoni aibu kusema uwongo kwa watanzania mchana kweupe?

Huyu jamaa atakuwa mnafiki sana, wakati wa sakata la maalbino kuuwa aliropoka ''kwa uchungu'' kuwa yeyote atakayekamatwa kwa kuua albino na yeye auawe, baadaye baada ya kupewa kibano bungeni kuhusu maneno haya, alitoa machozi.......akidai eti kuuawa albino kunamtia huzuni sana! Sasa je, albino ni binadamu na wale waliouawa Arusha ni nini? wanyama? kama ni binadamu, na kama asingekuwa mnafiki na mwongo ningetegemea angekuwa na at least consistent katika kukerwa na mauaji ya binadamu......! na hivyo kulieleza bunge ukweli wa kile kilichotokea Arusha!

Inakera na kuudhi sana, mtu mzima na kiongozi mzito kama yeye anapoamua kusimama mbele ya chombo kikubwa kama Bunge na kutamka maneno ya kisanii na uwongo kama alivyofanya huyu MP! Anaweza kuwa amefanikiwa kuwadanganya wabunge, lakini sisi wananchi tuliowapeleka huko we have nothing to loose, tunajua kuchambua mchele na chuya.....! One day this will end!

Kaka pole sana nadhani huoni kuwa pm anaelia bungeni badala ya kuwa imara ni pm gani huyo?
Mie pinda simkubali at all. Pm hajui kukemea, muda mwingi hulalamika tu kama wakulima. Kweli tz hatukujaliwa viongozi imara.
 
Pinda ni muhuni asiyestahili heshima. Nawashangaa watu wanaomuita mtoto wa mkulima. Kajamaa kabaya sana kale usikaone kanalialia ovyo. Niliacha kukaheshimu baada ya mkutano wa Bunge uliosababisha Lowasa na wengine kujiuzulu. Pinda alienda moja kwa moja mpaka Igunga na katika mkutano pale ambao ulihudhuriwa na mbunge wa Igunga Rostam Aziz, Pinda alisema na ninamnukuu, "ROSTAM NI MTU MUADILIFU SANA, MAMBO YA BUNGENI NI MENGI SANA, NAWASHAURI MUYAACHE HUKO HUKO". Kauli kama hii hawezi kuitoa mtu muadilifu. Ni huyu huyu Pinda anayesadikika kushurutisha matokeo ya ubunge na urais katika mkoa Rukwa kuchakachuliwa. Anajiita mkatoliki lakini yeye alikuwa namba moja kuutukana ukatoliki kwa kumfananisha kikwete na Mungu, wabunge , Yesu na madiwani wa CCM Roho Mtakatifu. Huyu jamaa ni kinyaa na matapishi. Na hakuna kinachoniudhi kama anavyojifanya mwema wakati ni adui wa haki. Si afadhali Lowasa alikuwa akichakachua waziwazi? Sasa huyu nungunungu kazi ya uwaziri nkuu hawezi, na ukweli hana. KAzi kulia lia tu kama yule feki Dokta anayejiita rais anavyo cheka chekaovyo wakati watanzania wanaangamia na umaskini. Aisee naichukia CCM we acha tu
Punguza hasira Mkuu.
 
hivi jf ni ya chadema? mbona hamna usawa kosa kuongea kuhusu mabaya ya chadema,

Ongelea lolote kaka/dada liwe CCM, TADEA, NCCR, CUF, TLP, NK ili mradi uwe na uwezo wa kujenga hoja na source ya uhakika wa thread yako lasivyo utapata wakati mgumu sana hapa jamvini... ukileta habari za kusimuliwa na suala la kusema JF ni ya CHADEMA si kweli ni mawazo na fikra zako tu... Pamoja tujenge nchi
 
Watu wamepoteza maisha Arusha. Waziri Mkuu makini angeaagiza uchunguzi huru wa kina kujua nani alimuua nani na kwa nini. Huwezi kukaa kulaumu CDM bila kuchukua hatua madhubuti kubaini ukweli na kufikisha mbele ya sheria wauaji. Kama ni CDM ndio waliohusika huwezi kushtaki chama kizima kwa mauaji. Uchunguzi huru ungeonyesha ushahidi ni nani hasa katika CDM "aliyeua". Kama ni Mbowe, au Slaa, au Lema, kamata weka ndani shtaki kwa mauaji! Kama ni polisi ndio waliaoua, bila sababu, vivyo hivyo. Ikukumbukwe kwamba kesi iliyopo mahakamani haihusiani na mauaji ya watu, inahusiana na maandamano bila kibali. Kesi hii haitatuambia ni nani aliuua Arusha. Mimi ningependa kuona wauaji wanashtakiwa kwa mauaji, na kama Pinda yuko sure kwamba akina Mbowe ndio walioua Arusha awafungulie mashtaka ya mauaji mara moja. Aache porojo za akina Makamba na Tambwe kwenye mauaji ya watu.
 
Nimekuelewa vizuri, na nakupongeza kwa ujasiri na kutufungua macho, Kuna kitu kimoja wana CCM na Viongozi wao hawaelewi, kwamba walioathirika ARUSHA si wanachadema tu, ni watanzania wa kawaida tena wapo wana CCM wengi ambao hawakubaliani na hali ya mambo ya chama ndani ya chama chao.

Kikubwa ni haki itendeke, kwani hatutegemei kwa wanayoyafanya CCM hata sasa inaiongezea CDM wafuasi, kwa hiyo mzee pinda aseme ukweli kwani muda wake wa kukaa madarakani ndio unaishia ukilinganisha na vijana kama mnyika, Lema, Mdee na wengine wengi kwa hiyo tunamuomba aachane na hizi propaganda afanye kama alivyokuwa TAMISEMI na kuwadanganya waTZ.
 
Mbaya zaidi inasemekana hizo barua za kikao (Kiambatanisho D nanukuu .....mkutano ulioahirishwa utafanyika tarehe 18/12/2010 saa 4.00 asubuhi) barua hizo zilipelekwa kwenye ofisi za CHADEMA saa sita usiku na kuachwa kwa mlinzi, hivyo madiwani wengi wa CHADEMA hawakujua kinachoendelea zaidi ya kujua ratiba ya awali ambayo ilikuwa ni semina na sio muendelezo wa kikao kilichovunjika tar 17. Nafikiri ushahidi wa dispatch utaeleza ukweli wa ni wakati gani madiwani walipata hizo taarifa za muendelezo wa kikao kilichoshindikana kwisha tarehe 17 hivyo muendelezo wake kuwa tar. 18
 
hii kitu iliishia wapi? watanzania na kasumba yetu ya kusahau

Inawezekana siku alizopewa kamanda lema za kuwasilisha hazijafika. Lakini ki ukweli serilikali ilishikwa pabaya, na kwasababu spika amepewa madaraka makubwa yakiwemo na ya kukalia mambo yanayoaibisha serikali, basi ndo imetoka hiyo. ripoti imesha kaliwa.
 
Back
Top Bottom