Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe amekitabiria ushindi chama cha Demokrasia na maendeleo-CDM katika uchaguzi mkuu unaokuja.
Waziri Membe amesema chama cha CDM kimetokea kupendwa na wananchi katika kila kona ya nchi na hata operesheni yao ya kusini imekitikisa chama tawala.
Waziri Membe aliyasema hayo katika chakula cha mchana alichowaandalia viongozi wa CDM nyumbani kwake waliokuwa katika jimbo lake la Mtama.
Viongozi hao ni mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema,kamanda James Millya na viongozi wakuu waandamizi.
Waziri Membe aliwaambia viongozi hao ameishi nchi mbalimbali duniani zenye demokrasia ya hali ya juu hivyo hatashangazwa hata kidogo CDM kuingia Ikulu.
Kuhusu kesi iliyotengua ubunge Lema waziri Membe amedai kushtushwa na kusema kwa vile amekata rufaa anaamini mahakama ya rufaa itamrejeshea ubunge wake.
Source: Mtanzania Jumapili.
Updates......
Katika taarifa ya habari ITV saa mbili usiku waziri Membe ameonyeshwa akiwakaribisha viongozi wa CDM nyumbani kwake kijijini Jimboni Mtama na kukaririwa akiwashutumu wabunge wanaolalamika kuvamiwa na CDM majimboni mwao katika vuguvugu la M4C.
Membe amesema wabunge hao hawajui ni nini maana ya siasa ya vyama vingi.