Mahojiano ya mwisho ya Membe akieleza sababu za kutoelewana na Magufuli

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
CL9IMpaW8AE0mmX.jpg

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (68), hatimaye amefichua mambo yaliyomfanya asielewane na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli.

Membe ambaye ni mmoja wa mashushusu hodari nchini, amesema Rais Magufuli, pamoja na mambo mengine, alimfitini hadi akakosa nafasi ya kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola. Jumuiya hiyo ni ya nchi 53 wanachama zilizokuwa makoloni ya Uingereza.

Membe anasema hajui hasa kisa za Magufuli kumfitini, lakini anadhani chanzo ni roho aliyokuwa nayo kiongozi huyo. Rais Magufuli, alifariki dunia Machi 17, mwaka 2021

Membe ambaye amekuwa mbunge wa Mtama kuanzia mwaka 2000 hadi 2015, anasema baada ya Rais Magufuli kukataa kumuidhinisha kuwa katibu mkuu wa jumuiya hiyo ndipo mashambulizi yalipoanza dhidi yake na anamtuhumu mtangazaji Cyprian Musiba, kama mmoja wa watu waliopewa kazi hiyo.

Mahakama Kuu ilimpa ushindi Membe, na kumtaka Musiba amlipe Sh bilioni 7 kama fidia kwa kumchafua. “Musiba alikuwa anafanya hiyo kazi ya kunichafua na kunisingizia uongo wa uhaini kwa maelekezo.”

“Jibu lake ni rahisi kabisa, uongozi wa juu wa nchi na uongozi wa juu wa Chama, hapo kuna Dk. Bashiru Ally (aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM) na Humphrey Polepole (aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.”

“Wote huo ulikuwa ni wasiwasi tu wa uchaguzi wa urais wa mwaka 2020, walidhani kwamba kichwani mwao kabisa ikifika mwaka huo wa 2020 Membe angekuwa tishio la kuchukua urais,” Alisema.

Membe alisema hakunuia kugombea urais mwaka jana kama ilivyodhaniwa, lakini akalazimika kufanya hivyo kutokana na yaliyojiri wakati huo. “Sikuwa nimenuia kugombea urais, mbona mwaka 2015 sikuwa nimenuia? I was provoked,”

“Nilistaafu vizuri nikawa na shughuli zangu vizuri na nilikuwa niwe Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, ndiyo kazi niliyokuwa nataka kuifanya tangu Novemba 2015, lakini yeye Magufuli akakataa.”

“Kwa sababu ili upate nafasi hiyo lazima uidhinishwe na rais wa nchi yako, lakini alikataa tu,” alisema na kuongeza:

“Septemba 2015 tulikwenda UN (Umoja wa Mataifa) katika mkutano wa General Assembly. Tulipofika pale kikafanyika kikao cha Mawaziri wa Jumuiya Madola na moja ya ajenda ni kupendekeza kwa viongozi wakuu kuteua jina la kupendekeza la mtu atakayeshika nafasi ya ukatibu mkuu… kwa sababu aliyekuwapo alikuwa anamaliza muda wake wakati huo.”

“Miongoni mwa mawaziri pale UN wakaamua kumchagua mtu aliyekuwa Mwenyekiti wa Commonwealth Ministiries Action Group (Kamati ya Kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri) atakayeshughulikia migogoro yote ya Jumuiya ya Madola katika kipindi cha miaka miwili.”

“Na huyo atatufaa, na mtu huyo alikuwa ni Bernard Kamillius Membe. Kikao kile kilifanyika nikiwa safarini kwenda India kumuangalia kaka yangu aliyekuwa mahututi wakati ule, alifariki dunia na kikao kile nilikikosa kwa wiki moja tu.”

Nilimuagiza Balozi Peter Kallaghe ahudhurie kwa niaba yangu, wakati huo ni balozi wetu pale Uingereza na kwa kuwa Jumuiya ya Madola inakutana na makao makuu yake ni London, Kallaghe akaenda kuniwakilisha wakinisubiri mimi.”

Alisema wakati huo hata Rais Jakaya Kikwete alitaarifiwa na akasema hana pingamizi na baada ya pale wakarudi nchini na wakaanza maandalizi.

Sektratieti ya Jumuiya ya Madola ikaja kumuona na Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo wakati huo, Waziri Mkuu wa Malta, Josephat Muscat, akamuita kwenda kumuona kabla ya mkutano huo.

Membe alisema alipoenda Malta kumuona akapewa baraka zote na wakamweleza kuwa anapaswa kuunda sera mpya, na hapa nchini wakatengeneza kamati iliyokuwa chini ya Balozi Liberata Mulamula wakati huo akiwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mulamula ambaye kwa sasa ni Waziri wa wizara hiyo, naye mapema mwaka 2021, na Likwelile Servasius majina yao yalikatwa na Rais Magufuli, wasigombee nafasi nyeti za kimataifa.

“Wakati kamati hiyo inafanya kazi yake Magufuli tayari akawa ni Rais. Ndipo Mulamula akaitwa na Magufuli na kupigwa marufuku kuandaa hiyo kamati kwa ajili ya kunifanya mimi niwe Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo,”

Membe alisema si hilo tu, bali ili Katibu Mkuu wa achaguliwe anahitaji Rais wa nchi husika akamwelezee katika vikao vya vya viongozi wakuu wenzake. Ananukuliwa marehemu Membe

“Wanakwenda huko wanakaa siku nzima na moja kati ya shughuli wanazozifanya ni kuteua Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola. Kwa hiyo rais wangu alitakiwa aende pale akasome CV (wasifu) yangu na kuwaambia wenzake waniunge mkono,”

“Hadi wanakwenda Commonwealth nilikuwa na nchi 32 zinaniunga mkono kati ya 53, na hata kabla ya kule nilikuwa nimeshavuka asilimia 50. Wakati Magufuli akiwa hapa akakataa kwenda Malta; na rais wako asipokwenda basi kazi imeshaisha.”

Akakataa kwenda kwa maelezo yuko bize kutengeneza baraza lake la mawaziri - kama mnakumbuka ilimchukua zaidi ya mwezi mmoja kutengeneza baraza.” “Akakataa, kwa hiyo aliua Kamati ya Jumuiya ya Madola pia akakataa kwenda Malta.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alinipigia, akaniambia nimeongea na Abdulrahman Kinana (wakati huo akiwa Katibu Mkuu wa CCM) na naongea na wewe - kama rais wako haendi anitume mimi kwa sababu mimi ni Mwenyekiti wa EAC (Jumuiya ya Afrika Mashariki) nikazungumze kwa niaba yake.”

“Rais wetu akakataa, sasa unataka ushahidi gani zaidi wa kuonyesha Rais alikataa?” Membe alisema Kinana akasaidia kwa kumfuata Rais Magufuli na kumwambia kama haendi amruhusu Kenyatta aende kwa sababu kule kuna fedha nyingi.”

“Kule commonwealth kuna fedha, wewe fikiria nilikuwa nakabidhiwa Paundi bilioni saba za commonwealth fund. Sekretarieti ilipokuja hapa kuni-brief. Nilikuwa nakabadhiwa fedha hizo kwa ajili ya technical fund kwa ajili kusomesha watu nje ya nchi, fedha za maafa, kuwawezesha wanawake, kupambana na magonjwa, tukakiacha kiti kikaenda Trinidad na Tobago, ujinga mkubwa,”

Membe alisema baada hayo kutokea hakuzungumza na Magufuli na hakupenda kabisa kumuona. “Sasa after the facts iweje? Na alishaonyesha wazi mimi kutopata nafasi hiyo, wala sikumtafuta na sikutaka kujidogosha kiasi hicho. “Wakati huo sikufanya ubaya wowote ndani ya chama (CCM) kwa sababu tuliteuliwa watu watano yeye akapita tatu bora na nilishiriki kwa mkoa wangu wa Lindi kumfanyia kampeni huku nikibembeleza nikijua kuna commonwealth position,”

“Tulikwenda vizuri hadi Novemba alipovunja ile kamati ya Commonwealth, akakataa kwenda Malta, akakataa kumruhusu Kenyatta, common sense inasema ni ushindani wa nafasi ya urais ndani ya chama.”

Sasa baada ya hapo yakaanza mashambulizi from no where katika vyombo vya habari ndipo akazuka Musiba.”

Alisema baada ya ushindi wa Magufuli yeye Membe alihojiwa na gazeti moja la kila siku na akaulizwa ushauri wake kwa rais kujenga uhusiano na dunia.

Membe anasema akajibu haiwezekani kutosafiri kwa sababu rais lazima aende nje kwa kuwa Tanzania haiwezi kujitenga pia akienda nje atajenga uhusiano.

“Kupitia vyanzo vyangu, nikasikia anasema unaona, mimi nimesema siendi nje huyu ananipinga. Mara sasa ikanza katika gazeti inatoka mara huyu ni mhujumu mara anafanya hivi, nikajiuliza hiki kitu inatoka wapi?”

“Inakwenda… inakua na wala mimi sikujibu, inakua inakua hadi likatengenezwa gazeti mahsusi kwa ajili ya kunishambulia, kila toleo lilikuwa linanishambulia, picha yangu inakuwa kubwa hata kama tuko wanne, Membe ni mtu hatari katika nchi hii, Membe apagawa,…

“.. Membe kumhujumu Rais, ala fedha za Libya. “Sasa mimi nimetoka katika intelligence, nina network, there is no doubt at all kwamba Magufuli, Bashiru na Polepole ndiyo walikuwa wanahusika.”

“Kwa hiyo nikavumilia, lakini kilichoniuma ni pale Bashiru alipojitokeza rasmi kumuunga mkono Musiba na kunipiga vita mimi. Nikiwa Zimbabwe katika uchaguzi nikasema kumbe ndiyo tumefikia katika pointi hiyo.
 
Kweli Membe alikuwa na confidence anaongea na mtemi huku mguu kapiga 4
 
Nafikiri sasa atakuwa ameshapokelewa na akina Ben Mkapa na Magufuli.
 
Huu Uzi ni wa Kuungwa Ungwa hauna Chanzo wala aliyeandika. Aliyehoji n.k Yaani imekosa taarifa na Maelezo muhimu.
R.I.P J.P.M B.C.M
 
Yaan hata nipige picha na tembo pamoja nyati still kwenye hiyo picha mi ndo naonekana bonge
 
Back
Top Bottom