Waziri Membe aitabiria ushindi CHADEMA uchaguzi mkuu ujao

Mh, lakini huyu Membe si ndo anatarajiwa kuwa mgombea uraisi kwa magamba 2015? Au kashaona hana lake! Anway tunamkaribisha.

Tunategemea maneno kama hayayenye busara na upeo mkubwa wa kuchambua mambo kutoka kwa Ndugu yetu Bwana Nape.
 
Chelewa chelewa utamkuta mwana si wako, wapi naweza kupata kadi ya CDM kabla hazijaisha? wana jamii nisidieni mi ni mkeleketwa wa CDM lkn si mwanachama.

Nawakilisha.
 
Bila kung'ata maneno hii habari ni uwongo uliotungwa na gazeti la akina Lowasa ili kumchonganisha Membe na chama chake cha MAGAMBA. Nasema hii habari ni ya UWONGO....
kweli bana,hata mie nilimsikia kwenye taarifa ya itv na nilimuona ni yeye kabisa.ila uso wa aibu alikuwa nao maana hali ya jimboni kwake ni tete,ahadi lukuki,utekelezaji 0.
 
Hizo ndo siasa. Ni ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa Membe. Kweli wewe ni mwanadiplomasia. Hakika kwa hili umenikuna. Kuna wanasiasa kama Wassira na Nape ambao wanadhani siasa ni ugomvi

Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe amekitabiria ushindi chama cha Demokrasia na maendeleo-CDM katika uchaguzi mkuu unaokuja.

Waziri Membe amesema chama cha CDM kimetokea kupendwa na wananchi katika kila kona ya nchi na hata operesheni yao ya kusini imekitikisa chama tawala.

Waziri Membe aliyasema hayo katika chakula cha mchana alichowaandalia viongozi wa CDM nyumbani kwake waliokuwa katika jimbo lake la Mtama.

Viongozi hao ni mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema,kamanda James Millya na viongozi wakuu waandamizi.

Waziri Membe aliwaambia viongozi hao ameishi nchi mbalimbali duniani zenye demokrasia ya hali ya juu hivyo hatashangazwa hata kidogo CDM kuingia Ikulu.

Kuhusu kesi iliyotengua ubunge Lema waziri Membe amedai kushtushwa na kusema kwa vile amekata rufaa anaamini mahakama ya rufaa itamrejeshea ubunge wake.

Source:
Mtanzania Jumapili.

Updates......
Katika taarifa ya habari ITV saa mbili usiku waziri Membe ameonyeshwa akiwakaribisha viongozi wa CDM nyumbani kwake kijijini Jimboni Mtama na kukaririwa akiwashutumu wabunge wanaolalamika kuvamiwa na CDM majimboni mwao katika vuguvugu la M4C.

Membe amesema wabunge hao hawajui ni nini maana ya siasa ya vyama vingi.
 
Umenikumbusha mbali...1928 alipozaliwa Ernesto Che Guevara, katika kitongoji cha na mji mkongwe wa Rosario kule Argentina....dahhh safi sana
 
Mh.Membe mejiandaa kweli kwa haya unayoyafanya...? maana najua hujatumwa na chama chako.
 
Kama kweli kam afanya kwa dhamira safi basi abarikiwe sana maana ni kiongozi wa kwanza kwa upande wangu kusikia amewakaribisha wapinzani ndani ya jimbo lake na kuwandalia chakula na kuzungumnza nao.Siasa safi na yakuigwa iliyo onyeshwa na Membe.Mungu akukirimie upendo ukarimu na utendaji mzuri siku zote za maisha yako Mh.
 
Mnafiki, mzabizabina, nyoka wa mdimu......!

Kwa hiyo we Mwalimu Mkuu, huamini kama CDM watashinda? Basi utabaki na matusi yako ifikapo 2015! Watu wanaona mbali bana, membe kashayaona haya, sasa kama unafikri ni unafiki ila alishawamaliza nguvu wapambe wake kwa kutamka hivyo na wananchi waliomchagua nao wamemsikia so na wao wanajua kuwa 2015 CDM itashinda kwa hiyo hawataenda kupiga kura kwa CCM
 
Membe ameongea yaliyo moyoni kwake. Pia, ameonyesha busara. Hata Maige ameshatoa kauli kama hii zaidi ya mara 1. Mwendawazimu Nepi ndio amebaki kichwa ngumu.

Please please when you want to be serious with issues never mention these names:
1) Nape (Nepi)
2) Mukama
These two figures are always dreaming and they are on a very rubbish/foolish slip.
Their vivid stupidity is so bright.
 
Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe amekitabiria ushindi chama cha Demokrasia na maendeleo-CDM katika uchaguzi mkuu unaokuja.

Waziri Membe amesema chama cha CDM kimetokea kupendwa na wananchi katika kila kona ya nchi na hata operesheni yao ya kusini imekitikisa chama tawala.

Waziri Membe aliyasema hayo katika chakula cha mchana alichowaandalia viongozi wa CDM nyumbani kwake waliokuwa katika jimbo lake la Mtama.

Viongozi hao ni mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema,kamanda James Millya na viongozi wakuu waandamizi.

Waziri Membe aliwaambia viongozi hao ameishi nchi mbalimbali duniani zenye demokrasia ya hali ya juu hivyo hatashangazwa hata kidogo CDM kuingia Ikulu.

Kuhusu kesi iliyotengua ubunge Lema waziri Membe amedai kushtushwa na kusema kwa vile amekata rufaa anaamini mahakama ya rufaa itamrejeshea ubunge wake.

Source:
Mtanzania Jumapili.

Updates......
Katika taarifa ya habari ITV saa mbili usiku waziri Membe ameonyeshwa akiwakaribisha viongozi wa CDM nyumbani kwake kijijini Jimboni Mtama na kukaririwa akiwashutumu wabunge wanaolalamika kuvamiwa na CDM majimboni mwao katika vuguvugu la M4C.

Membe amesema wabunge hao hawajui ni nini maana ya siasa ya vyama vingi.

anajitahidi kusoma alama za nyakati anatakiwa kuangaliwa kwa macho mawili asije kuwa anawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa
 
Angalau Mh. Membe amefunguka kwa kauli iliyojaa busara na si kama mzee wa Gombe anayeamka na kuropoka mf. CDM kitakufa 2013! Lol!!
 
kwangu mimi hizi kauli na kitendo cha kuwakaribisha wahasimu wako wa kisiasa nyumbani kwako pasipo kificho wala vijembe, ni ukomavu wa kisiasa! Ni kama shabiki mkubwa wa simba kumkaribisha mwenzake wa yanga huku akisifu usajili wao (yanga) kuwa msimu ujao timu yao itafanya vizuri na huenda ikachukua ubingwa! For once, hongera Membe kwa ukweli wako.
 
Back
Top Bottom