Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Wakuu ninaomba nitofautiane na ninyi wengi humu, kuna chanzo kinasema ni marsha aliyelalamikia zoezi hilo kwa pm sasa inakuwaje hapa interest inakuwa kwa kiranja aliyeripoti manung'uniko ya wadau kupitia kwake kwa kiranja mkuu? Tuwe wakweli hapa jf. Masha amekuwa tatizo letu kubwa kiasi hiki cha kumfanya awe target nambari wani kila kukicha au? Kuna nini behind this big machine lawrence marsha? He is young but vita anayopigwa ni kama vile alikuwemo ktk zama akina kingunge na msuya
 
- Masha, Masha x 100 squared...

- Tumeahabarishwa kwamba kila member wa hiyo Bodi ya Tenda ana-kampuni anayoipigia debe (right?), na mimi najiaminisha kuwa hilo ni kweli. Kwa maana hiyo basi swala la mjumbe ku-support kampuni kupata tenda ni kigezo by default. Kila mmoja kwa umoja wake au kwa wingi wao kuna kampuni anayo/wanayo-ipigia debe.

- Binafsi sipendi kick-backs (Rushwa) katika tendering process, BUT, wandungu that is de facto!

- Hoja jangu hapa ni kwamba, tusimrushie makombora Masha peke yake kwa maana wajumbe wote wanafanya vile vile (i.e. kupendelea kampuni X kupata tenda), na WOTE ni MAFISADI kwa kigezo hicho. Na kwa hiyo basi hicho kigezo ni batili!!!!

- Naamini kuna vigezo vingine katika zoezi hili!

- Mheshimiwa Dr. Slaa, Heshima Mbele, tumwagie vielelezo vinyoonyesha kuwa Waziri Masha amekwaza zoezi hili na pia vinavyoonyesha ni jinsi gani wajumbe wengine wanavyoendesha zoezi hili kwa misingi sahihi ya tenda/manunuzi.

- Nawakilisha
 
Jana nilimsikia Mhe. Waziri Mkuu akisema kuna karatisi zilizochomolewa kwenye baadhi ya failes zihusiano na mchakato wa Tender hiyo ya serikali na kuwa hiyo ndio sababu ya kusambaa kwa taarifa hizo. Inasikitisha sana kusikia kuwa Serikali iko so vulnerable.

Lakini kwa upande mwingine, nadhani kuna watu watakaoumia sana kama wataendelea kufanya mambo hayo (kuchomoa karatasi za siri za serikali). Najua kuna sheria inayokataza mambo hayo kufanyika na adhabu endapo mhusika akikamatwa. Naomba wanasiasa wetu wawe waangalifu sana katika mambo haya. Maana itafika siku wakaanza kupata matatizo makubwa.
 
Na Boniface Luhanga, Dodoma

1.Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, majibu ya wazabuni walioingia hatua ya pili ya mchakato wa kupata kazi ya kutengeneza vitambulisho vya taifa hayajatolewa kwa wahusika Je, kampuni ya Sagem Securite ilijua vipi imeenguliwa hadi kulalamika kwa Waziri Masha?

2.Hadi sasa taarifa zinasema si Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wala Bodi ya Zabuni, waliopewa nakala ya barua ya malalamiko ya Sagem Securite, kwa hali hii ni Waziri pekee mwenye barua hiyo, Je, ni halali kukalia barua na kulalamika tu bila kuonyesha vyombo husika?

3.Kwa nini Sagem Securite walilalamika kwa Waziri tu na si kwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani na nakala ya malalamiko kupelekwa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) kama maelekezo ya zabuni yalivyoonyesha?

4. Kwa nini hata pale Waziri Masha ambaye ni mwanasheria mahiri alipopata malalamiko ya Sagem Securite hakuwaelekeza pa kwenda kwa mujibu wa sheria ya PPRA, badala yake aliamua kuchukua jukumu hilo kwa niaba ya mzabuni?

5.Sheria ya PPRA haitoi fursa ya kulalamika kuhusu zabuni kama vyombo vyote vinavyohusika katika kupitia mchakato wa zabuni ya umma vitakubaliana kwa mujibu wa sheria je, ni kwa nini Waziri Masha alijitokeza na kumtaka Katibu Mkuu wake aombe maelekezo PPRA wakati bodi ya zabuni hakutofautina?

6.Uchunguzi wetu umeonyesha wazi kwamba vyombo kadhaa vya usalama wa nchi vilishiriki katika mchakato wa zabuni hiyo ambavyo ni Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) tangu hatua ya awali, je, malalamiko ya Masha ya kutokukubalina na maamuzi ya bodi ni kielelezo cha kukosa imani na vyombo hivyo na kwamba yeye peke yake ndiye anayeona hitilafu katika mchakato huu?

7.Waziri Masha anadai kulalamikiwa na Sergen Securite, inakuwaje anataka hata makampuni ambayo hayajalalamika rasmi kwake yarejeshwe kwenye mchakato wa zabuni?

8. Kwa nini Waziri Masha hakumweleza Waziri Mkuu ukweli wote kuhusu kampuni ya Sagem Securite hata baada ya kuelezwa na bodi ya zabuni, ni kwa nini pia hakuwa na ujasiri wa kumwona Katibu Mkuu Kiongozi kujua sababu za kumwagiza Katibu Mkuu wake aendelee na mchakato wa zabuni, ni nguvu gani inamsukuma kushindwa kuona yote haya?

9. Kwa nini Waziri Masha ameamua kumpuuza Katibu Mkuu wake, kwa nini hataki afanye kazi kama mtendaji na anamshinikiza kisiasa, je, anataka kuwa msimamizi wa sera na mtendaji kwa wakati mmoja?

10.Waziri Masha anataka kuwaambia Watanzania kwamba mchakato mzima wa zabuni ya vitambulisho vya taifa una utapeli, rushwa na kwa maana hiyo ufutwe kwa sababu tu kampuni ya Sagem Securite imeenguliwa kwenye zabuni?

Watanzania wangependa kusikia majibu ya Masha ingawa amekwisha kusema kwamba hawezi kuzungumzia barua aliyomwandikia Waziri Mkuu wala uingiliaji wake mchakato wa zabuni ya vitambulisho vya taifa kwa sababu anatekeleza kazi za Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Source: NIPASHE


PM
NB: Folio No. 37!
 
Waziri wa JK matatani
• Hoja yake yaweza kumtia matatizoni

na Charles Mullinda, Dodoma

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, huenda akakumbana na hukumu ya Bunge iwapo itathibitika kuwa wizara anayoiongoza iliingilia madaraka ya Bunge.

Mwangunga yuko katika hatari hiyo baada ya wizara yake kutoa maamuzi ya kuwaongezea muda wa kuendelea na uwindaji wamiliki wa vitalu vya uwindaji kutoka nje, huku Bunge likiwa halijapitisha uamuzi wa hoja binafsi iliyowasilishwa na Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya (CCM).

Jana muda mfupi baada ya Waziri Mwangunga kuwasilisha bungeni taarifa ya utekelezaji wa Azimio la Bunge la ugawaji wa vitalu vya uwindaji na bei zake, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alilitangazia bunge kuwa Mzindakaya amewasilisha barua kwake ya kuomba awasilishe hoja kuhusu hadhi ya bunge kutokana na hatua ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuingilia madaraka ya Bunge.

Spika Sitta alisema uamuzi wa Mzindakaya wa kuwasilisha au kutowasilisha hoja hiyo ya haki na madaraka ya Bunge kuingiliwa, atautoa leo saa nne asubuhi bungeni.

Wanasheria kadhaa waliozungumza na Tanzania Daima jana baada ya tamko hilo, walisema iwapo itathibitika Waziri Mwangunga ameingilia madaraka na haki ya Bunge, anaweza kukabiliwa na kifungo cha siku saba gerezani.

Katika hoja binafsi aliyoitoa Mzindakaya Aprili 24 mwaka jana katika mkutano wa 11 wa Bunge, baadhi ya mambo aliyotaka yaangaliwe upya au kurekebishwa ni kuondoa kasoro zilizojitokeza katika mkataba wa serikali na TAHOA, aliodai wamekuwa wakiutumia vibaya kwa maslahi ya wamiliki wachache wenye vitalu vya uwindaji.

Mzindakaya (CCM) aliishutumu Idara ya Wanyamapori kwa kuzikumbatia kampuni za nje katika umilikaji wa vitalu vya uwindaji huku za kizalendo zikinyimwa fursa.

Hoja ya Mzindakaya wakati huo iliungwa mkono na wabunge wengine akiwamo Mbunge wa Iramba Mashariki, Mgana Msindai (CCM), aliyeshauri mtindo wa uwindaji wa kitalii ubadilishwe na ikiwezekana ufutwe kutokana na kile alichosema wageni ndiyo wanaoendesha sekta hiyo badala ya wazalendo.

Katika hoja yake hiyo binafsi, Mzindakaya aliyekuwa akilalamikia ugawaji wa vitalu vya uwindaji na bei zake ambavyo muda wake kisheria unamalizika mwaka huu, aliliambia Bunge kuwa zaidi ya Sh bilioni 60 zinapotea kwa mwaka kutokana na utaratibu mbaya wa ugawaji wa vitalu hivyo.

Alisema wawindaji wa nje wana usumbufu na kwamba wamekuwa wakitamba kuwa kila waziri anayehamishwa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wao ndiyo waliomwondoa na akaongeza kuwa, wawindaji hao waliwahi pia kumtishia Katibu Mkuu.

Naye Msindai akimuunga mkono Mzindakaya alisema, pamoja na kampuni za wazalendo kupewa maeneo yasiyo na wanyama, bado kuna viongozi wengi serikalini na wengine wa Idara ya Misitu, wenye kumiliki vitalu kupitia kampuni nyingine.

“Idara ya Wanyamapori haijasafishwa. Wanashirikiana na kampuni kuhujumu nchi. Nchi inaliwa na wenye kampuni za uwindaji,” alisema Msindai na kushauri kuwa kama ambavyo serikali imefanya katika sekta ya madini, iingie pia katika wizara hiyo kubaini hali inavyokwenda.

Akisoma maazimio yake, Mzindakaya alisema masharti yanayotumiwa na Idara ya Wanyamapori kugawa vitalu yanawanyima fursa waombaji wapya huku yakitoa fursa kwa kampuni zenye uwezo wa fedha.

Alisema pia ugawaji huo, umekuwa ni siri ya Mkurugenzi wa Wanyamapori kutokana na kutokuwapo uwazi. Kwa mujibu wake, mkataba wa maelewano kati ya TAHOA na Serikali, umeendelea kutumiwa vibaya kwa maslahi ya wamiliki wachache wa vitalu.

Alisema akiwa kama Mbunge wa CCM, amewahi kupeleka mapendekezo kama haya kutokana na ushirikiano wake na wizara, lakini kutokana na watu wachache wanaojali maslahi yao hayatekelezwi.

Akiipokea hoja hiyo binafsi ya Mzindakaya wakati huo, Waziri Mwangunga alisema serikali imeyapokea na itayafanyia kazi yaliyoelezwa.

Hata hivyo, alisema kuanzia mwaka 2000, hakuna kampuni ya nje iliyopewa kitalu na kwamba kampuni za Kitanzania zimeongezeka kutoka 17 hadi 32.
Chanzo: Tanzania Daima
 
Kampuni anayoibeba Masha ni balaa tupu


2009-01-30 10:49:51

Na Waandishi Wetu


Kampuni ya Sagem Securite ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha anadaiwa kuibeba katika mchakato wa kupata mzabuni wa kutekeleza Mradi wa Vitambulisho vya Taifa ambao utaigharimu serikali kiasi cha Sh. bilioni 200, kama ni sawa na iliyoomba kazi ya aina hiyo nchini Nigeria mwaka 2003 ni ya hatari.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, kampuni hiyo, ikijiita Sagem Securite iliwatia matatani mawaziri watatu wa serikali ya Nigeria wakati huo ikiongozwa na Rais Olusegun Obasanjo, kutokana na kudaiwa kuwahonga mawaziri hao kiasi cha Dola za Marekani milioni 2.

Hongo hiyo ilidaiwa kutolewa kama kishawishi kwa viongozi hao ili waibebe katika zabuni ya kutengeneza vitambulisho vya kitaifa vilivyokuwa viliigharimu nchi hiyo kiasi cha Dola za Marekani milioni 214.

Mradi huo unafanana na ambao serikali ya Tanzania inataka kuanzisha wa kutengeneza vitambulisho vya taifa ambao utagharimu taifa Sh. bilioni 200 (sawa na Dola za Marekani milioni 150).

Rais Obasanjo kwa kukasirishwa na uroho wa wasaidizi wake, alimfuta kazi Waziri wa Kazi na Uzalishaji wa nchi hiyo, Hussaini Akwanga.

Akwanga alidaiwa kutenda kosa hilo akishikilia wadhifa wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Nchi ya Nigeria.

Chanzo hicho kilisema kuwa Rais Obasanjo alichukua hatua hiyo wakati uchunguzi wa kashfa hiyo ukiendelea, lengo likiwa ni kupiga vita rushwa kwa watumishi wa umma.
Wakati akimfukuza kazi Akwanga, Rais Obasanjo alisema Waziri huyo, alilidhalilisha taifa.

Waziri huyo na wenzake watano walifunguliwa mashtaka mahakamani kwa makosa 16 yanayohusiana na sakata hilo, linalokadiriwa kusababisha hasara ya Dola za Marekani milioni 214 sawa na Sh. 300 bilioni. Waliofikishwa kortini walidaiwa kula rushwa ya Dola za Marekani milioni mbili.

Walioshtakiwa pamoja na Akwanga, na nyadhifa walizokuwa nazo kwenye mabano ni Turi Akerele (Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani), Dk. Okwesilieze Nwodo (Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Peoples Democratic Party), Dk. Mohammed Shatta (Waziri wa Nchi wa Mambo ya Ndani) na Sunday Afolabi aliyweahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini humo.

Afolab alishtakiwa kwa kupokea Dola za Marekani 330,000, Akwanga alimuwezesha binti yake kupokea Dola za Marekani 30,000 kwa niaba yake.

Mwakilishi wa kampuni hiyo nchini Nigeria ndiye aliyedaiwa kutoa rushwa hiyo akishirikiana na Nwodo na Akerele alipokea Dola za Marekani 500,000.

Kampuni hiyo ikielezwa kuhusika na kashfa hiyo kuhusu vitambulisho vya taifa nchini Nigeria, jana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alithibitishia Bunge kwamba Waziri Masha alimwandikia barua pamoja na mambo mengine akimtuhumu Katibu Mkuu Kiongozi kuingilia wizara yake bila kumuhusisha katika mchakato wa zabuni ya vitambulisho hivyo.

Akijibu mwaswali ya papo kwa papo bungeni, Pinda alisema taarifa hizo ni kweli kwa kuwa kuna nyaraka zimenyofolewa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.

``Hilo ni kweli kabisa, maana kuna watu wamenyofoa folio pale Wizara ya Mambo ya Ndani,`` alisema Pinda alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, aliyetaka kujua sababu za Waziri Masha kuingilia mchakato wa zabuni ya vitambulisho vya taifa kinyume cha sheria ya Manunuzi ya Umma (PPRA).

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwataka watu wavute subira ili mchakato huo ukamilike kwanza ndipo mwenye kutaka kuhoji afanye hivyo.

``Mheshimiwa Slaa umetuwahi, lakini jambo hili linafanyiwa kazi. Ingekuwa ni vizuri ukasubiri mpaka mchakato umalize ulete madai kama haya ingesaidia sana,`` alisema Pinda, na kuongeza:

``Mchakato huu haujafika mwisho. Tusubiri halafu tutamhukumu Waziri ukikamilika.``

Hata hivyo, ilibidi Spika, Samuel Sitta, alilazimika kuingilia kati kwa kuyakataa baadhi ya maswali yaliyoelekezwa kwa Waziri Mkuu na Dk Slaa kutokana na kuonekana kwamba baadhi ya wabunge walionekana kuleta malumbano na Pinda.

``Nadhani tukitumia kipindi hiki kulumbana na Waziri Mkuu, si sahihi Ukipata `facts` na we uliza ufafanuliwe `facts` na siyo kuleta malumbano na kung`ang`ani kile unachodhani wewe ni sahihi,`` alisema Spika Sitta.

Alimshauri Dk. Slaa kutumia njia nyingine ya kuwasilisha bungeni hoja binafsi kama hakuridhika na majibu aliyopewa na Waziri Mkuu ili kutoa fursa ya kujadiliwa na wabunge wengi zaidi.

Naye Joseph Mwendapole anaripoti kuwa Dk Slaa, amesema anaandaa hoja binafsi kwa ajili ya kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, awajibishwe kwa kuingilia mchakato wa kumpata mzabuni wa kutengeneza vitambulisho vya taifa.

Akizungumza na Nipashe jana, Dk. Slaa alisema anashangaa kuona Waziri Masha akiingilia shughuli ambayo anajua fika kuwa hana mamlaka nayo kisheria.

Alisema anashangazwa na hatua ya Waziri Masha kuandika barua ya malalamiko kwa Waziri Mkuu kutetea kampuni ya Sagem Securite iliyoomba zabuni ya kutengeneza vitambulisho hivyo.

Waziri Masha anadaiwa kuitetea kampuni hiyo baada ya Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo kuiengua katika mchakato wa kuwania zabuni hiyo.

Dk. Slaa alisema Masha kama angeona kuna taratibu zimekiukwa alipaswa kumwelekeza mlalamikaji (Sagem Securite), hatua za kuchukua kuwasilisha malalamiko badala ya yeye (Masha) kulalamika kwa niaba ya kampuni hiyo.

``Mchakato wa zabuni hii una usiri na mashaka sana...na mashaka haya yanadhihirishwa na waziri ndani ya serikali kulalamika kwa niaba ya kampuni iliyoomba zabuni,`` alisema na kuongeza kuwa Waziri hana mamlaka ya kuingilia mamlaka zinazoshughulikia masuala ya zabuni.

Aidha, alisema kama Waziri alikuwa na mashaka na maamuzi yaliyotolewa na kamati ya zabuni, alipaswa kuielekeza kampuni ya Sagem kwenda kulalamika kwenye Mamlaka ya Usimamizi wa Zabuni (PPRA) na si yeye kulalamika.

``Kama kulikuwa na malalamiko, PPRA ndiyo ilipaswa kuchunguza na kutoa jibu kama kuna sheria au taratibu imekiukwa au la, sasa yeye anakimbilia kwa Waziri Mkuu kufanya nini na ana maslahi gani na kampuni hiyo?`` alihoji Dk. Slaa na kuongeza kuwa Masha ni mwanasheria na alijua fika kuwa anachokifanya ni kinyume cha sheria.

Alisema atakapokamilisha hoja yake hiyo ataiwasilisha kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ambayo ndiyo ina mamlaka ya kupanga siku ya kusikilizwa kwa hoja hiyo.

Alisema inashangaza kuona mabilioni ya fedha za umma zikizidi kuyeyuka katika mchakato usio na mwisho, lakini hakuna anayewajibishwa.

Dk. Slaa alipinga kauli ya Waziri Mkuu aliyoitoa jana bungeni kuwa mchakato wa zabuni hiyo unaendelea kwa kuwa sasa umesimama.

``Nitaomba kama haya yanayosemwa juu ya Masha ni kweli basi awajibishwe kwa kuwa kila anayekiuka Sheria lazima achukuliwe hatua za kisheria,`` alisema.

Masha anadaiwa kufanya hivyo akidai kutoridhishwa na hali halisi ya mchakato huo kabla hata matokeo ya kupatikana mzabuni hayajatangazwa.

Kampuni hiyo, ni kati ya makampuni 54 yaliyoomba kupewa zabuni hiyo. Ilienguliwa katika mchujo wa tatu, baada ya mchujo wa kwanza kuyaengua makampuni 33 na kubaki 21 na mchujo wa pili, kuyaengua makampuni 13 na kubaki manane.

Wajumbe wanaounda bodi hiyo, ni wanatoka Magereza, Uhamiaji, Jeshi la Polisi, Zimamoto na Uokoaji, Usalama wa Taifa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru).


SOURCE: Nipashe
 
Nakumbuka kwenye nyuzi mojahuko nyuma niliwahi kusema mh Masha ametukatisha tamaa baada ya kujiingiza kwenye old school politics. Badala ya kuja na mtazamo mpya kwenye siasa zetu, amemezwa na kuingia kwenye mkondo ule ulewa siasa za mipasho, blackmail, na kuanza mambo ya kitoto ambayo yameondoa kabisa credibility yake. He has gone completely native, and is now lacking newness we expected of him. ama tetesi zina ukweli basi zina msingi fulani.
 
mhn, siyo Masha peke yake, wako wengine pia sijui hao wawili walio bakia ni akina nani, ila kwa ujumla viongozi wa leo wana tumaliza kabisaa na ni kwa makusudi, hapa ni kuomba Mungu tu, Ujasiri na kujizira ndiyo dawa pekee, mtu asicheleweshwe mbona Msumbiji Raisi alifukuza mawaziri na hata jenerali wake mkuu!!! sisi bado tunaendekeza uswahili tu !! tutajie hao waliobakia tujazie minofu
 
Siyo tu kuwa na elimu ndiyo unafaa kuwa kiongozi lahasha,itakiwa vilevile uonyeshe kuwa kazi inafanyika na watu wajivunie kuwepo kwako hapo na kuona kuwa elimu yako ulionayo inaisaidia jamii katika kutatua matatizo ya kila siku.

Lakini hapa, ninachokiona ni sawasawa na mtu mzima hovyo; yaani unafanya vitu ambavyo hata mtoto mdogo haamini kama unastahili hata kuigwa (role model) na hii nafikiri ndiyo inayopelekea JK kubadili baraza la mawaziri kila mara. Kwasababu, anateuliwa mtu kufanya kazi kwa manufaa ya umma lakini akienda pale unashangaa hivi ilikuaje mpaka akapewa hii nafasi!?
 
Una maana kati ya watu milioni 40 hakuna angalau watu 4,000 wenye uwezo wa kuongoza? Au wapo lakini hawapati nafasi? Na kama hawapati nafasi ni kwa nini hawapati nafasi?

Hawapati nafasi sio kana kwamba hawana uwezo bali sio WANAMTANDAO; sio maswahiba wa Jakaya
 
Inaezekana Mengi akawa hana kosa ila Mie Personally simpendi Mengi.Hivyo ndivyo nilivyo

Sasa wewe Gembe wewe ni nani hata kudiriki kuchukia mtu na kusema kwenye forum au kwa sababu una masters!
 
Naona Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda (MB), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atalia sana mwaka huu na huu ni mwezi wa kwanza tu - bado mingine kumi na moja.
 
Nasikia huyu Masha ana uraia wa nchi mbili? Uraia wa Marekani na Tanzania? Inakuwaje hapa wadau!Waziri wa Mambo ya Ndani na Uraia wa Nchi Mbili?Kwa tetesi nilizo pata watoto wake huko kwa Babu mandela shuleni wameandikishwa kama raia wa marekani!?

Bila shaka kuna haja ya kutafuta uhakika wa hili suala ubalozi wa America na kupata ufafanuzi zaidi, maana ni Hatari ya danger kuwa na viongozi wa namna hii.Naomba kama kuna mdau yeyote mwenye nyeti hizi atusaidie kwa maslahi ya nchi na wala si kwa maslai ya mtu au chama.mna uchungu na nchi yangu, Tanzania nakupenda inaniuma sana ninapo ona unachezewa.
 
No wonder mauaji ya maalbino yameendelea kupeta kipindi chote hiki... Waziri alikua bize , ekchuale vere bize na mambo mengine nyeti... Ya Sagem.

After all kwani kwenye maalbino kuna dili la mshiko???... Ndio viongozi wetu hao.
 
Naufahamu utendaji kazi wa Lau (Masha),ni mmoja kati ya watendaji waliokuwa wazuri,nimeshtuka na hili lililomkuta toka awe Waziri,(nimefikiri kuwa labda ni ulimbukeni lakini si kweli)nimefikia hatima ya kuona kuwa Siasa sio nafasi yake...Ni vyema ajiuzulu tu..nafasi hizi za kisiasa na arudi Immma kuendeleza Taaluma yake ya Sheria.Kuna shutuma nyingi zinaelekezwa moja kwa moja kwake...na ni shutuma nzito.....Huwezi kuwa kiongozi mzuri kama una mzigo wa lawama mgongoni mwako!!!Uongozi ni trust,kama watu hawakuamini huwezi kuwaongoza!!
 
Naufahamu utendaji kazi wa Lau (Masha),ni mmoja kati ya watendaji waliokuwa wazuri,nimeshtuka na hili lililomkuta toka awe Waziri,(nimefikiri kuwa labda ni ulimbukeni lakini si kweli)nimefikia hatima ya kuona kuwa Siasa sio nafasi yake...Ni vyema ajiuzulu tu..nafasi hizi za kisiasa na arudi Immma kuendeleza Taaluma yake ya Sheria.Kuna shutuma nyingi zinaelekezwa moja kwa moja kwake...na ni shutuma nzito.....Huwezi kuwa kiongozi mzuri kama una mzigo wa lawama mgongoni mwako!!!Uongozi ni trust,kama watu hawakuamini huwezi kuwaongoza!!

mwawado... nyota njema huonekana asubuhi. Wengine tulipoonesha dalili tukaonwa tuna "chuki". Tatizo la viongozi wa Tanzania siyo elimu, siyo kabila, siyo wapi wamesoma, na kwa hakika siyo dini zao.. tatizo la viongozi wetu ni uwezo.

Bado tunafanya makosa ya kufikiria msomi=kiongozi bora! au mwenye mvuto=kiongozi bora..!!! Swali ni tunapimaje uwezo kabla hawajapewa madaraka? Maana kama Lau alipewa nafasi (promotion as a matter of fact) hili linasema nini kuhusu uwezo wa yule aliyemteua? au mchakato wa uteuzi wake?
 
1. Naufahamu utendaji kazi wa Lau (Masha),ni mmoja kati ya watendaji waliokuwa wazuri,

2. nimeshtuka na hili lililomkuta toka awe Waziri,(nimefikiri kuwa labda ni ulimbukeni lakini si kweli)

3. nimefikia hatima ya kuona kuwa Siasa sio nafasi yake...Ni vyema ajiuzulu tu..nafasi hizi za kisiasa na arudi Immma kuendeleza Taaluma yake ya Sheria.

4. Kuna shutuma nyingi zinaelekezwa moja kwa moja kwake...na ni shutuma nzito.....Huwezi kuwa kiongozi mzuri kama una mzigo wa lawama mgongoni mwako!!!Uongozi ni trust,kama watu hawakuamini huwezi kuwaongoza!!

Mkuu Mwawado,

- Heshima mbele sana, watu wa aina yako humu ndani sio wengi, ambao huwa ninawaheshimu sana kwa sababu huwa hamkurupuki na ishus na hata mnapotoa hukumu huwa mnakuwa mmetoa kila aina ya nafasi kwa mhusika au wahusika, na pia huwa mnakuwa na subira ya habari yote na facts zake zote, badala ya mbio mbio za kulilia kujiuzulu.

- Leo asubuhi, nimeongea na waziri mmoja ambaye ni very senior na kiongozi mmoja mkubwa sana wa CCM, kuhusu hatma ya Lau na uwaziri, at this point ninaungana kabisa na maoni yako kwa 100%, kwamba wakati umefika kwa Lau kufikiria tena kama kweli he belongs kwenye siasa hasa za taifa.

- Hili la vitambulisho limenishitua kuliko yote ya negative yanayomuhusu niliyowahi kuyasikia toka awe waziri, maana kama nilivyowahi kusema huko nyuma siyajui sana yanayomuhusu kwenye level ya uwaziri, lakini hili limenishitua sana kwa sababu on the record personally nilimuonya toka day one anapewa uwaziri wa ndani kuwa stay away form this national ID thing maana kuna wanaokutega wakunase kwenye hilo na nikawaomba ndugu zake wa karibu wamkumbushe maneno yangu kuwa awe muangalifu na hili na ikibidi alikalie mbali sana maana ninawajua wote waliokuwa wakimtafuta kwenye hili la national ID,

- sasa leo tena to hear this kwamba Lau na national ID, ina maana moja tu kwamba sikio la kufa halisikiii dawa, ingawa pia nitampa nafasi ya kusikiliza his side of the story maana so far sijampata, mara ya mwisho nilisema naye akiwa Mwanza na Mkulu wangu Margai, wiki mbili zilizopita ambapo hii ishu ilikuwa haijaibuliwa.

- Kwa kumaliza naomba tena kusema hivi, kama haya ya ID ni kweli kama nilivyoambiwa leo asubuhi na wakulu, basi ndugu yangu Lau huenda akawa katika maji ya shingo sana kuliko anavyofikiri.

- Ni kweli mengi sana yamesemwa hapa JF kuhusu Lau, lakini naomba kuwakumbusha wale wote waliokuwa na haraka za kudai kujiuzulu kwa Lau, kuliko Sophia Simba, kwamba wazazi wangu waliponipeleka shule kwa mara ya kwanza, waliniambia kua wanataka nijifunze kufikiri for my own na kujua kusema yes and no at the right time, na sio anything else, to this day they all regret hayo maneno waliyonifundisha maana yamewaumiza wao kuliko anybody else, hasa la mimi kufikiri na kuamua on my own badala ya kusubiri kufikiriwa na kuamuliwa na wengine!

Again, ninajaribu kumtafuta kujua na kusikia his side of this story, kabla sijatoa my final hukumu, lakini kwa machache niliyoyasikia leo, ninakubaliana na wewe Mkuu Mwawado kwamba huenda siasa sio mahali pa Lau, maana najua kwa nafasi yako unajua mengi kuliko uliyoyasema hapa. Na Lau hawezi kumlaumu Mengi kama haya ni ya kweli, wa kujilaumu atakuwa ni yeye mwenyewe, maana nimemuambia hata kabla hajaapishwa kua waziri wa ndani kuwa kaaa mbali na national ID, I mean inasikitisha sana.


Sauti ya umeme - Wazee wa FMES!
 
Back
Top Bottom