Waziri Makamba atangaza Serikali kununua umeme kwa wawekezaji Njombe

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Serikali imetangaza kununua umeme kwa wawekezaji

Chanzo: ITV Tanzania/ facebook

--------

Waziri wa Nishati, January Makamba na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wametumia jukwaa moja kutoa majibu ya wananchi wa Lugalawa, wilayani Ludewa mkoani hapa, kuhusu upatikanaji wa umeme na mbolea kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo.

Juzi, Waziri January aliwasiliana na Bashe kwa simu akiwa eneo la Lugarawa na kumpa nafasi ili azungumze na wananchi hao katika mkutano wa hadhara waliotaka kujua mkakati wa Serikali kuhusu upatikanaji uhakika wa mbolea katika msimu ujao wa kilimo.

Katika maelezo yake, Waziri Bashe alisema Agosti 8, mwaka huu katika maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) Rais Samia Suluhu Hassan atazindua mpango wa kutoa ruzuku kwenye mbolea na wananchi hao hawatanunua mbolea kwa bei ilivyo sasa.

Katika maelezo yake kwenye mkutano huo, Waziri January alisema Serikali ipo tayari kununua umeme unaozalishwa na mwekezaji binafsi wa kampuni ya kufua umeme ya Madope ili kuboresha mazingira ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wakazi wa Ludewa.

Alisema kilichotokea ni mkandarasi aliyejenga mtambo huo kushindwa kujua mahitaji halisi ya watu wa vijiji 20 vya Ludewa.

Alitolea mfano umeme uliokuwa ukizalisha na kampuni hiyo, haikuzingatia mahitaji halisi ya wananchi wa vijiji hivyo ndio maana kunajitokeza changamoto za kukatika kwa nishati hiyo.

“Mtambo ulipokuwa ukiwashwa kule, hizi nyaya ndogo zinazopeleka umeme kwenye baadhi ya maeneo nishati hii inazimika au transfoma inalipuka.Kwa hiyo ule mradi ulitengenezwa kiswahili sio kitaalamu, fedha zimepotea lakini malengo hayakutimia na mchakato huu ulifanywa na waendesha mradi siyo Serikali.

“Serikali haiwezi kuwaacha na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) iuchukue mradi huu na kuundesha. Pale kwenye kituo unazalishwa umeme megawati 1.7 na matumizi ya hapa 0.3, sasa tutauingiza kwenye gridi ya Taifa hilo lina uhakika,” alisema.

Alisema Serikali itanunua umeme huo ili kuokoa wanaLudewa na italazimika kuilipa Madope, lakini tathimini iliyofanyika mwaka 2019 kuhusu kuirekebisha miundombinu ili kuondoa changamoto za sasa ili kutoa huduma ilikuwa Sh 4.5 bilioni hata hivyo sasa hivi hali imebadilika huenda gharama hizo zimepanda.

Waziri January, hatua hiyo itafanikiwa endapo wanaendeshaji wa mradi huo ikiwemo kanisa katoliki Njombe wataridhia mchakato huo.

Alisema endapo wakiridhia wataalamu wake watakwenda Ludewa kwa ajili ya kukamilisha taratibu.

Ombi hilo lilikubaliwa na wadau hao akiwemo Mkurugenzi wa Madope, Kulwa Masanja aliyesema Serikali ina uwezo wa kuundesha mradi huo kutokana na rasilimali watu na itauendesha kwa ufanisi hivyo wananchi watanufaika.

Mwananchi
 
Oyoooo, naona watz wakipigwa za uso tena kama kipindi kileee.

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom