Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,555
- 41,066
Watanzania yaelekea vichwa vyetu ni vizito sana kuelewa!!
Wakati January Makamba akiwa Waziri wa Nishati, aliwahi kunena kuwa kukatika kwa umeme kulikuwa kumesababishwa na mitambo ya TANESCO kutofanyiwa matengenezo wakati wa utawala wa Hayati Magufuli. Akaongeza kuwa baada ya matengenezo, kukatika kwa umeme itakuwa historia.
Sasa, naamini huenda sikumwelewa Makamba. Nilidhani Makamba alikuwa akimaanisha kuwa kukatika kwa umeme kutaisha na watu watabakia kukumbuka tu kuwa hapo awali umeme ulikuwa ukikatika. Ninyi wengine mlielewi nini?
Lakini kwa yanayoendelea sasa, nashawishika kuamini kuwa Makamba alikuwa akimaanisha kuwa baada ya kukamilika zoezi walilokuwa wakilifanya, kukatika kwa umeme kutakuwa ni kwa kiwango cha historia, yaani umeme utakatika kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea. Na naona baada ya kulikamilisha zoezi la kukatika umeme kwenye kiwango cha historia, Rais aliridhika kuwa kazi ameikamilisha vizuri, akazawadiwa wizara ya kimataifa.
Sasa Rais amesema kuwa mwisho wa kukatika umeme ni mwezi March 2024. Hofu yangu ni kuwa isije kuwa nimemwelewa vibaya tena. Isije ikawa baada ya mwezi wa tatu, ikawa mwisho wa umeme kukatika kwa sababu uemme hautakuwepo kabisa. Maana kadiri tunavyoisogelea March 2024, hali ya umeme inazidi kuwa mbaya zaidi.