Waziri Dkt. Ndumbaro akabidhi Mifuko ya Saruji 50 Ujenzi Ofisi za CCM Tawi la Mahenge

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo na Mbunge wa JImbo la Songea Mjini, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameambatana na Komredi Alhaji Mwinyi Msolomi, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea kutoa msaada wa mifuko 50 ya Saruji ili kuwezesha ujenzi wa Ofisi ya Tawi la Mahenge Kata ya Songea Mjini.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara wa Kilele cha Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata ya Mfaranyaki, Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema kuwa watu wa Mfaranyaki hawana budi kumchagua kwa kishindo Ndugu Kayombo kwani amekuwa na uzoefu ndani ya CCM kwa miaka 15

"Christopher Kayombo amekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Tawi kwa muda wa miaka 10, mpaka anachukua fomu ya Udiwani alikuwa ni Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa. Uzoefu wake wa miaka 15 ni dhahiri kwamba anakijua Chama Cha Mapinduzi na Kata ya Mfaranyaki" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

WhatsApp Image 2023-09-19 at 22.31.22.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-19 at 22.31.20.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-19 at 22.31.25.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-19 at 22.31.25(1).jpeg
 
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo na Mbunge wa JImbo la Songea Mjini, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameambatana na Komredi Alhaji Mwinyi Msolomi, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea kutoa msaada wa mifuko 50 ya Saruji ili kuwezesha ujenzi wa Ofisi ya Tawi la Mahenge Kata ya Songea Mjini.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara wa Kilele cha Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata ya Mfaranyaki, Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema kuwa watu wa Mfaranyaki hawana budi kumchagua kwa kishindo Ndugu Kayombo kwani amekuwa na uzoefu ndani ya CCM kwa miaka 15

"Christopher Kayombo amekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Tawi kwa muda wa miaka 10, mpaka anachukua fomu ya Udiwani alikuwa ni Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa. Uzoefu wake wa miaka 15 ni dhahiri kwamba anakijua Chama Cha Mapinduzi na Kata ya Mfaranyaki" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Ubarikiwe Mh Ndumbaro
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom