Mbunge Juliana Shonza Akabidhi Mifuko 30 ya Saruji (690,000) Ujenzi Ofisi ya UWT Kata ya Ibaba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza ameendelea na ziara yake katika Wilaya ya Ileje Kata ya Ibaba kwa lengo la kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero za wananchi na kuwapa mrejesho wananchi kuhusu utendaji kazi wa Serikali.

Katika ziara yake, Mhe. Juliana Shonza aliambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka TANESCO, RUWASA ili wajionee wao wenyewe kutoka kwa wananchi changamoto wanazopitia na kutoa majibu sahihi.

Mhe. Juliana Shonza alimtaka afisa kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Songwe kueleza kwanini Watu wanalala giza wakati Rais Samia Suluhu ameshatoa maagizo kwani Mmeweka alama lakini hakuna nguzo wala hakuna umeme. Mna mpango gani?

Vilevile, Mhe. Juliana Shonza alimuomba Meneja wa RUWASA Mkoa wa Songwe kuzungumza kuhusu maji kwani haiwezekani wananchi wakakosa maji kwasababu ya kukosa Pampu tu.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza akizungumza na Wanawake wa UWT Ileje amepongeza ujenzi wa Ofisi za Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Ibaba

Aidha, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza amefurahishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 na kusema kuwa wao kama viongozi wanatembea vifua mbele. Miaka ya nyuma CCM Tunduma tulinyanyasika sana, hata kuvaa nguo ya CCM ilikuwa ni mwiko.

"Kuna muda najiuliza hivi Rais Samia hizi fedha zote anayatoa wapi, kwasababu hakuna Jimbo au Kata ambayo utaenda usikutane na miradi ya Shule. Mbozi kuna shule ya msingi imejengwa, tumesema iitwe Mama Samia, utajua ni Chuo lakini ni shule ya msingi ya kisasa" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

Mhe. Juliana Daniel Shonza amemshukuru Diwani wa Kata ya Ibaba usimamizi mzuri wa ujenzi wa barabara kwani barabara zinapitika tofauti na Mwanzoni Barabara zilikuwa hazipitiki kirahisi.
 
Attachments

  • pongezi za ujenzi wa uwt ofisi.mp4
    29 MB
  • majibu ya fidia mkurugenzi mkoa.mp4
    50.2 MB

Mifuko 30 ndio kusifia hivyo? Punguza siasa nyepesi
 
Wewe umetoa mifuko mingapi hapo mtaani kwenu? Unajuwa inahitajika mifuko mingapi mpaka yeye kutoa hiyo? Unafahamu namna Mheshimiwa Juliana shonza alivyo fanya kazi kubwa katika mkoa wa Songwe na wilaya zake?

Hakuna mahali unapoweza kwenda usikute alama za Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza. Hata uchaguzi ujao atapita kwa kishindo maana hana wa kunyima kura katika mkoa wa Songwe.

Alishawapa kila aina ya mahitaji wanayohitaji wanawake katika kuwainua kiuchumi na kupata mitaji. Amegawa hadi mitungi ya gesi kuwapa wanawake .

Sasa wewe eleza umefanya nini kusaidia watu na kugusa maisha ya watu.
 
🤣🤣🤣 mifuko 30 ya saruji ndiyo inaandikwa kwa mbwembwe namna hii??

Mbona hii hela mm naitumia kwa chai tu??
Huna lolote wewe. Unaelewa ilikuwa inahitajika mifuko mingapi mpaka yeye akatoa hiyo? Hivi kwa akili yako unafikiri ametia ni hapo tu? Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza anatoa na kujitolea sana katika kusaidia wananchi na mambo mbalimbali ya kimaendeleo.ukienda shuleni ,zahana,vituo vya afya n.k.utakuta kaweka mikono yake .
 
Wewe umetoa mifuko mingapi hapo mtaani kwenu? Unajuwa inahitajika mifuko mingapi mpaka yeye kutoa hiyo? Unafahamu namna Mheshimiwa Juliana shonza alivyo fanya kazi kubwa katika mkoa wa Songwe na wilaya zake?

Hakuna mahali unapoweza kwenda usikute alama za Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza. Hata uchaguzi ujao atapita kwa kishindo maana hana wa kunyima kura katika mkoa wa Songwe.

Alishawapa kila aina ya mahitaji wanayohitaji wanawake katika kuwainua kiuchumi na kupata mitaji. Amegawa hadi mitungi ya gesi kuwapa wanawake .

Sasa wewe eleza umefanya nini kusaidia watu na kugusa maisha ya watu.
Mwambie na pale Kinyerezi anapoishi ile shule ya msingi ambayo yupo jirani nayo wanafunzi wanahitaji madawati.
 
mifuko 30 ya saruji ndiyo inaandikwa kwa mbwembwe namna hii??

Mbona hii hela mm naitumia kwa chai tu??
Halacu angalia msafara alio fuatana nao na magari kibaoooo. Kwenda kutoa oesa za kunywa bia kwa masaa mawili.
Difa nyingine ni za kishenzi kabisa
 
Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza anatoa na kujitolea sana katika kusaidia wananchi na mambo mbalimbali ya kimaendeleo.ukienda shuleni ,zahana,vituo vya afya n.k.utakuta kaweka mikono yake .
So what!? Huu ni uzwazwa. Mbunge hapaswi kuwa mfadhili ktk Jimbo lake.

Kwahiyo kama anafanya hivi ili kujiongezea kukubalika kwake ni mpumbavu na hajui wajibu wake.

Mbunge ni mwakiloshi wa wananchi (ni kama messenger). Wabunge wengi akiwemo huyu Shonza (sijui nimepatia jina lake?), ni mbumbumbu.
 
Kwani huko ninyi hamna mbunge wenu. Au mnataka aje agombee na huko. Mpeni barua ya maombi atakuja awasaidie maana hanaga hiyana wala ugumu katika kusaidia watu.
Humu hamna wapiga kura wake, nenda huko alipopeleka cement ukafanye campaign....
 
So what!? Huu ni uzwazwa. Mbunge hapaswi kuwa mfadhili ktk Jimbo lake.

Kwahiyo kama anafanya hivi ili kujiongezea kukubalika kwake ni mpumbavu na hajui wajibu wake.

Mbunge ni mwakiloshi wa wananchi (ni kama messenger). Wabunge wengi akiwemo huyu Shenzi (sijui nimepatia jina lake?), ni mbumbumbu.
Unazifahamu kazi za mbunge
 
690,000÷30 = 23,000

Yani mfuko mmoja huko Songwe unauzwa kwa sh elfu 23?

Samia anafanya nini madarakani sasa?
 
mheshimiwa Juliana shonza hana mpinzani 😍😍😍🙏🏽 Mungu aendelee kukuweka dada yangu nakupenda sana
 
Kwani katoa mifuko 30 ya cement (ambayo haina cement) au katoa cement mifuko 30* (yenye cement)?
 
Back
Top Bottom