Waziri Chami amwaga chozi - Awataka watumishi wamuombee asiadhirike

Maskini Chami, kuvuliwa uwaziri sio mwiso wa maisha, before hujawa waziri ulikuwa unaishije?
 
Chezea kupanda V8 wewe na posho za 400k kila safari lazima chozi limwagike
 
Akili za CCM bwana, hivi vijamaa vimekazana 'mimi sikuiba, mimi sikuiba'. Ndio hamkuiba, haya basi mbona vimeibiwa mkiwepo na hamkusema kitu?

Kama hamumuelewi, kinachomliza ni madili yake ambayo yako pending. Pengine kulikuwa na documents ambazo angezisaini angelamba mpunga wa maana sasa anawaza wakati wazungu wanazileta yeye keshamiminwa.

Eti Mungu, Mungu gani na wezi? Na bado, huo uliopoteza ni uwaziri, jiandae kupoteza UBUNGE. CDM wameshaanza kulitathmini jimbo lako
 
Kama waziri hana taarifa za kazi ya Kamati ya Bunge basi hapo hakuna waziri. Alitakiwa atolewe mapema zaidi

Pia kitendo cha kulia hadharani ni udhaifu mkubwa kwa kiongozi. Hivyo nashauri wapiga kura wake waandamane kumng'oa
 
Napata shida sana, mbona Nyalandu na Malima wamerejeshwa kwenye baraza? Nasikia Nyalandu anafadhili WAMA ni kweli? Na huyo Malima je amewezaje kuwa msafi ndani ya wizara chafu kama Nishati na madini? Ninajiuliza sana sipati jibu.

Mkuu wapi pameandikwa kuwa kuna mtu msafi ndani ya CCM? Waliorudishwa hawakurudishwa sababu ya usafi wao, wamerudishwa sababu ya sanda-ka-lawe kuwadondokea. Hamna jipya hata kwa hao wanaoitwa wapya; Kanzu mpya shehe yuleyule
 
Ekelege!!!!!mkongwe kwenye system tunasubiri tuone atafanywaje zaidi kufichwa tu na kurudi kijiweni pale makaburini!!ndio hao hao!!ukiambiwa hizo pesa zilitumika.......utakataa??EPA,Meremeta walisemaje?pesa zimetumika mambo ya usalama........period


Hivi Ekelege bado anakalia kiti chake pale TBS? Nilitarajia angekuwa selo (cell) muda huu
 
,uwaziri wa tz ulitakiwa kuwa kazi nzito ya kutosha kumpa mtu mvi za stress ndani ya miezi miwili, yaani mtu akitolewa inatakiwa avute pumzi ndefu na kushukuru Mungu hasa kama ana uhakika hajaiba....sasa hii ya kulia tena...!!1
 
Dr Chami ameondolewa kwa sababu ya TBS. Lakini inakuwaje Mkuchika anabaki ili hali Halmashauri zimekula mabilioni? Au Prof Maghembe amebakije wakati board ya Pamba inafili wakulima wa pamba, wakulima wa korosho wanalala barabarani, mbolea na mbegu fake zimezagaa?
 
Kanunua nyumba masaki...kaiangusha yote ili ajenge upya.kabla hajakaa sawa kapigwa chini.Wengi tunajua bei ya nyumba ya kawaida masaki haipungui milioni 500...linganisha ubunge na uwaziri kapata lini halafu mtizame tena anavyotoa michozi...mimi naweza kumnyonga hapo hapo
 
Mijizi mingine hata haya haina.. pambav kabisa, kwani madudu ya TBS ndio ilikuwa mara ya kwanza kuyasikia pale bungeni?? bila shaka fangas zitakuwa zinamtafuna...
 
Natabiri kutakuwa na hali ya kutokuaminiana,

Na hiyo hali itafanya wateule waogope hata unyasi wakidhani ni nyoka

Na kwa kufanya hivyo, huenda utendaji ukawa wenye mafanikio.
 
mkuu mi sijaelewa analia kaukosa uwazi au analilia nini Jamani aende zake moshi akaanzi
she kiwanda cha kusindika maparachichi
 
Kama huyu waziri ni Mchagga basi kama kuna wizi anahusika moja kwa moja. Ripoti za Wabunge alizikalia na akawa anatetea, Why? kama hahusiki!

wewe pia unafahamika kwa kuitetea serikali ya ccm, Maige, Mponda na Mkulo wamesabisha hasara kubwa zaidi kwenye wizara zao, ni wachaga pia? Ila tunajua iyo "mchaga" umelenga nini, pole, raisi wa Tanzania atatoka popote, kama akitimiza maitaji ya katiba. Na cdm wakimpitisha yeyote kati ya Mbowe au Silaa, atakua raisi. R.I.P magamba
 
Kanunua nyumba masaki...kaiangusha yote ili ajenge upya.kabla hajakaa sawa kapigwa chini.Wengi tunajua bei ya nyumba ya kawaida masaki haipungui milioni 500...linganisha ubunge na uwaziri kapata lini halafu mtizame tena anavyotoa michozi...mimi naweza kumnyonga hapo hapo


Acha chuki....,kumbuka kuwa Chami kabla ya kuwa waziri alikuwa mshauri wa Rais Mkapa Uchumi, na kabla ya hapo alikuwa Lecturer kwenye vyuo vikuu canada.......,zile qouter alipata kama watumishi wengine ,....na alikopeshwa na hadi kesho anakatwa.....huwezi kufananisha na wanaonunua nyumba cash dola laki 5 hadi 7......,
 
Neno la Mwenyezi Mungu Dr. Chami halijui vizuri. Masahihisho ni kuwa Ayubu hakuadhibiwa kwa makosa ya wengineo bali alijaribiwa na Mwenyezi Mungu kupima ucha Mungu wake kutokana na shetani kumlalamikia Mungu ya kuwa Ayubu alimpenda Mungu kwa sababu ya neema alizopewa na Mwenyezi Mungu.

Pili Chami aache kujipima hiyo ni kazi ya Mungu pekee yake asimwingilie na kujaribu kujisafisha machoni pa wanadamu.

Jingine huyu bwana ni mbinafsi sana hivi. Yeye bado Mbunge bado anataka tumwombee huko aendako kwani anaenda ahera? Mbona hawaombei watanzania wengi ambao wanaishi kwa mlo mmoja kwa kutwa wakati yeye bado ni mbunge?
 
Issue sio yeye kuwa mbadhirifu, amepewa wizara kusimamia, kama hakufanya kazi yake vyema hata kama hakuiba hata sensi tano, basi yeye alikuwa ni mzembe, tena anatakiwa kusimama kizimbani kwa kutofanya kazi yake vyema na kusababisha hasara kwa serikali na taifa kwa ujumla,kafie mbele mzembe mkubwa wewe.
 
Back
Top Bottom