Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,967
- 12,430
Niaje waungwana
Huyu Mhe. Innocent Bashungwa, alikuwa ni miongoni mwa mawaziri wachache sana niliowaheshimu sana katika baraza hili la mawaziri wa raisi Samia.
Kila alipopelekwa alionesha kupamudu vizuri kiutendaji, na kiusimamiaji lakini sasa huku alipoletwa sasa hivi (wizara ya ujenzi) kunaonekana wazi kumshinda, na hii ni baada ya waziri huyo kutembelea maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam na kujionea ubovu wa barabara zetu, kisha kuahidi ahadi hewa na baadae kutoweka bila kutekeleza ahadi zake alizoahidi.
Kila mtu anakumbuka jinsi alivyoahidi kuishughulikia haraka iwezekanavyo barabara ya Mbezi - kuelekea Msumi lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika na hajarudi tena kuwaambiwa wananchi wa maeneo hayo kwamba nini kinafanyika ili mradi huo wa ujenzi uanze, na sio barabara hiyo tu, ni nyingi mno amekuwa akiahidi bila utekelezaji.
Sasa kwa maana hiyo, huyu waziri ashaanza kuonekana kuwa hafai kuendelea na wizara hiyo, ni bora tu ajiuzulu, ahamishwe au apambane tena kuikamilisha. Hawezi kuendelea kutupiga changa la macho watu wazima na akili zetu kama vile mzee awadanganyae wajukuu zake. No.. no.. no again.