Waziri Aweso aagiza timu ya Wataalamu kuchunguza madai ya maji yenye uchafu Sombetini Arusha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com ambaye ni Mkazi wa Sombetini kusema kuwa kuna changamoto ya maji yasiyo salama kutoka kwenye mabomba ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA), hali ambayo ilikuwepo kwa miezi kadhaa nyuma na sasa imejirudia na kuwasababishia Magonjwa ya Tumbo, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso metoa neno.

Kupitia Ukurasa wa Instagram wa JamiiForums, Mdau mwingine alichangia taarifa hiyo kwa kuandika “Jamani mimi nimeharisha damu wiki nzima maji yanatoka yana Wadudu kabisa nipo Sombetini maji ni machafu mno mnoooooo.” Ndipo Waziri Aweso akasema:

“Ninalifuatilia jambo hili kwa ukaribu sana, nimeagiza timu ya Wataalam na watu wa ubora wa Maji kufika Sombetini haraka, nikuombe pia mawasiliano yako ili tukufikie pia na kuwa na picha halisi ya muathirika wa hali hii kama ipo.”

Baada ya muda Mdau huyo akajibu kuwa ametumia sehemu ya ushahidi wake na mawasiliano yake kupitia ‘inbox’ na Waziri Aweso akamjibu kuwa amepata na anafanyia kazi.

Awali, Mdau aliyeanzisha mada alisema kuna muda maji yamekuwa yakitoka yakiwa na harufu kama ya kinyesi na mengine kuwa na uchafu ambao unaonekana. Anadai walipeleka malalamiko kwa Viongozi wa ngazi mbalimbali, wakapiga kelele hali ikapoa, lakini hivi sasa imerejea kwa mara nyingine huku Viongozi wakiwa kimya

Hoja ya Mdau wa awali soma hapa = Maji ya bomba yanayotoka Sombetini (Arusha) ni machafu na yanatuathiri Wananchi
 
Japo siyo sawa kuwepo kwa maji machafu kwenye mfumo rasmi wa maji mijini na vijijini, Inaonesha huyo mdau anakunywa mamji bila kuchemsha. Hamna maji unayoweza kunywa hapa Tanzania kwa sasa bila kuchemsha labda yaliyo kwenye chupa tu, na uhakikishe hayajachakachuliwa.
 
Back
Top Bottom