hivi lakini kwa nini hawawapi hawa wazee kilicho chao wakamalizie maisha yao na waende bila kinyongo? kwa nini nchi hii ina dhuluma kiasi hiki?
Ndahani.. hiilo ni kweli na nina uhakika wazee hao hao ndio waenda kuwachagua watu wale wale walioshindwa! Ila jiji la Dar nalo ni mishen town over the years yawezekana wapo wengine wamedandia mbele ya safari LOL
mojawapo ya mambo ambayo yananishangaza hadi sasa; miaka 30 baadaye wameshindwa kutatua tatizo hili!!!!
Hii kali kweli kweli! halafu mbona kawa wengi wao wana bagarashia na kujifunga shungi ama ni kujikinga na jua?
Labda umesahau kidogo hapo kwenye red, aliyesema hivyo alikuwa ni character Rashid katika kitabu cha KULI, na mwandishi alikuwa Shafi Adam Shafi wa huko Zenji!Hizi ni laana kabisa wanajitengenezea hawa mafisadi. Yote haya yana mwisho (Chonya wa Chilonwa)
Labda umesahau kidogo hapo kwenye red, aliyesema hivyo alikuwa ni character Rashid katika kitabu cha KULI, na mwandishi alikuwa Shafi Adam Shafi wa huko Zenji!
Hivi hawa wazee baadhi yao sio ndio wale wanaoitwa wazee wa Dar es salaam waliokuwa wakimshangilia JK kwa mbwembwe?
Watanzania hawatambuai kuwa maamuzi yako mikononi mwetu. Kwani hujaona wakipewa tisheti na kofia, na wengine miguuni hamna hata yebo, wako wanaishangilia ccm. CCM IMETUMIA MTAJI WA UJINGA KUENDELEA KUTAWALA NDO MAANA HATA SERA ZAO ELIMU HAIPO!
Naipenda nchi ya Chile ilivo okoa watu wao wote 33. Japo mtoto mmoja wa kitanzania alianguka kwenye bwawa karibu na chuo kikuu cha mlimani, pamoja na kushindwa kumwokoa akiwa hai, hata maiti yake walishindwa! HIVI HII NI NCHI? AU NI USANII.