Wazee wa East Africa wazua tafrani jijini Dar

hivi lakini kwa nini hawawapi hawa wazee kilicho chao wakamalizie maisha yao na waende bila kinyongo? kwa nini nchi hii ina dhuluma kiasi hiki?

Siyo kwamba tatizo ni moja, yako mengi mfano; tumesimamisha wanafunzi wote wa vyuo vikuu zaidi ya 60,000 wasifungue vyuo mpaka tumalize uchaguzi maana nao wanataka mikopo! Serikali yetu haina fedha kwa sasa sababu fedha zote tumezielekeza kwenye uchaguzi. Gharama ni kubwa mno. Ebu fikiria kuwanunulia wananchi zaidi ya milioni 15 kanga, t-shet, kofia, skaf, mashati, vitenge n.k. Hapo bado mabango, helkopta n.k.
 
mojawapo ya mambo ambayo yananishangaza hadi sasa; miaka 30 baadaye wameshindwa kutatua tatizo hili!!!!
 
Last edited by a moderator:
You can not solve the problem at the same level it was created. Tatizo limewashinda maana hawana new ideas za kulimaliza. Inawezekana wamekuwa wanalipa hao wastaafu ila hela zinaishia kwa watu wasiokuwa wastaafu halali wa EA.
Hata hivyo kwa upande wa pili, hawa wazee miaka yote hii si wangelifanya kazi nyingine na kupata zaidi ya hela hizo wanazodai?
 
Ndahani.. hiilo ni kweli na nina uhakika wazee hao hao ndio waenda kuwachagua watu wale wale walioshindwa! Ila jiji la Dar nalo ni mishen town over the years yawezekana wapo wengine wamedandia mbele ya safari LOL
 
Nafikiri mwaka huu kuna kila sababu ya watu kwenda kupiga kura.Tuwachague wawakilishi watakaokwenda kutusaidia kumaliza matatizo kama haya yasiyo isha miaka nenda miaka rudi. Tusipofanya hivyo, regardless ya nini yatakuwa matokeo( kuheshimiwa ama kutoheshimiwa), itabidi tujifunze kufunga midomo yetu na kukaa kimya.
 
mojawapo ya mambo ambayo yananishangaza hadi sasa; miaka 30 baadaye wameshindwa kutatua tatizo hili!!!!

Simple being said than done!!!! NB Kesi hii iko mahakamani... hicho ndio chombo ambacho kinahusika kutoa haki, lets wait!!!
 
Last edited by a moderator:
Kasheshe.. miaka karibu 30 kweli? mnawaambia "lets wait".. kwelimnasubiri mahakama ya duniani au ya mbinguni hadi wote waishe ndiyo mje kutoa hukumu?
 
Hii kali kweli kweli! halafu mbona kawa wengi wao wana bagarashia na kujifunga shungi ama ni kujikinga na jua?

..sheikh hilo ni vazi tu.....,wazee wetu wameona kunakuchwa.......its so sad kama bilioni at least 10 zingetosha kuwafanya hawa wazee .......wakae kimya kabisa........wakati CCM wanatumia zaidi ya Bilioni 50[bajeti rasmi]......acha bajeti za pembeni zisizo rasmi na za wagombea ubunge wao wanaochangisha wafanyabiashara....SIONI KAMA SERIKALI INASHINDWA KUWALIPA...wangejiminya kidogo bajeti yao ya mabango wangewalipa wazee hawa..ambao waliwaahidi kuwalipa baada ya kulala pale salender......wamewasahau!!

halafu siri nyingine ya kutofungua vyuo ni kuwa CCM wamekomba pesa zote hazina..na wameogopa wangeruhusu tu wanachuo 60,000 nchini warudi vyuoni ......kungezuka migomo ya kila pembe ,ukichangannya na hii ya wstaafu...hapo hapo ishu ya watumishi na waalimu [aliowaangukia songea] haijatulia....CCM wangekuwa wanajichimbia kaburi.......

Ni wazi kuwa kazi ya kwanza ya bunge la kwanza mwezi ujao ni kujadili na kupitisha bajeti ndogo ili nchi iendee.....maaana serikali imebanwa kila engo!!!
 
Hizi ni laana kabisa wanajitengenezea hawa mafisadi. Yote haya yana mwisho (Chonya wa Chilonwa)
Labda umesahau kidogo hapo kwenye red, aliyesema hivyo alikuwa ni character Rashid katika kitabu cha KULI, na mwandishi alikuwa Shafi Adam Shafi wa huko Zenji!
 
Labda umesahau kidogo hapo kwenye red, aliyesema hivyo alikuwa ni character Rashid katika kitabu cha KULI, na mwandishi alikuwa Shafi Adam Shafi wa huko Zenji!

Sahihisho...ni kitabu kilichotungwa na marehemu Ndyanao Materu(nee Balisidya) sikumbuki title yake na sio Kuli
 
Fedha za kununua maelfu ya tshirts, kapelo , hongo , helikopta na Mabango zipo, lakini za kuwalipa wastaafu hakuna!...Lakini Mungu anaona haya, na yatalipwa kwa wakati!
 
Katika CCM ya sasa viongizi wengi wa juu ni wachumia tumbo tu ukianza na mwenyekiti wao. Hii inajidhilihili wanapotumia pesa nyingi kwenye kampeni wakati mwanzoni alishinda by more than 80%. Baada ya uchaguzi yatafumka mengi tu.
 
Watanzania hawatambuai kuwa maamuzi yako mikononi mwetu. Kwani hujaona wakipewa tisheti na kofia, na wengine miguuni hamna hata yebo, wako wanaishangilia ccm. CCM IMETUMIA MTAJI WA UJINGA KUENDELEA KUTAWALA NDO MAANA HATA SERA ZAO ELIMU HAIPO!

Naipenda nchi ya Chile ilivo okoa watu wao wote 33. Japo mtoto mmoja wa kitanzania alianguka kwenye bwawa karibu na chuo kikuu cha mlimani, pamoja na kushindwa kumwokoa akiwa hai, hata maiti yake walishindwa! HIVI HII NI NCHI? AU NI USANII.
 
Hii ni nchi yenye AMANI, UTULIVU NA MSHIKAMANO na watu wa nje wanatuangalia kwa jicho la husuda.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom