Wazee wa East Africa wazua tafrani jijini Dar

hivi lakini kwa nini hawawapi hawa wazee kilicho chao wakamalizie maisha yao na waende bila kinyongo? kwa nini nchi hii ina dhuluma kiasi hiki?

Ninahisi hii pesa ya hawa wazee imeshafisadiwa zamani saaaaana, na inawezekana aliyewafisadi keshakufa zamaaaaani sana.
 
Hiki ndicho kipindi muafaka cha kudai haki yao, kwa njisi CCM ilivyobanwa katika kampeni basi watalipwa fasta fasta ili wasiathiri zaidi kampeni. Tatizo ndani ya hili kundi kuna wengine wasaliti njaa ni adui wa kila kitu, kwenye njaa hakuna haki bali Rushwa hutamba.

Hapa ukimwaga elfu 50 tu kwa wale viongozi wao mchezo umekwisha hadi mwakanii.
 
Wazee wetu waliofanya kazi kipindi sisi hatujaweza kusimama na kujitegemea ndiyo wanaadhirika sasa.
Naamini kama serikali inaendelea kubeza madai yao tunajitafutia laana walah.

Vita dhidi ya rushwa inashindikana kwa elements kama hizi ambapo tunashuhudia wastaafu wanateseka ilhali unajua kamshahara kadogo, basi unaamua kujitwalia pensheni yako mapemaaaa kabla jua halijatua. Serikali ijayo ya CHADEMA iweke mazingira ya kuwaenzi wastaafu kwa kuwahakikishia maisha nafuu baada ya kustaafu. pia wazee walipwe mafao yao kwa wakati na stahili.

Mungu awasaidie hawa wazee wetu ambao wanafia njiani ktk kudai haki zao za lifetime.
 
...Ndio maana kuna wakati unajisikia kutowaonea huruma wazee wetu hawa. Wameishahatarisha maisha yao kwa kukaka barabarani wakidai haki yao lakini hawakupewa lakini mwisho wa siku ndio hawa hawa wanaovaa fulana za njano na kijani na kupiga makofi pale Mheshimiwa anapokataa kura za Wafanyakazi. labda watatia akili. kama kuna muda mzuri wa kudai haki zao na wakalipwa basi ni sasa. lakini wana ujasiri huo????
 
kweli inanishangaza, kisha hawa wazee hawaelewi kua Kikwete ni kitisho cha wao kupata maslahi Bora, Dr Slaa anauwezo wa kuwalipa hawa wazee, anazombinu maridhawa
 
Nimesikia kuwa leo wale wazee wastaafu wa EAC ya mwanzo wamefunga barabara ya kivukoni pale mahakama kuu wakidai haki zao na kusema hawataondoka mpaka JK au Pinda aende kuonana nao.

Mwenye habari zaidi atuletee na picha vilevile!!!!!!
 
Kusema ukweli watu wetu wanaoonewa na utawala huu hawastahili kuonewa huruma. Kuna watu vijiji wanachangia maji ya kunywa na fisi, miaka 50 baada ya uhuru, na wengi wao huyafuata maji hayo hadi kilometre 20 lakini wapi bwana.

Especially huko usukumani yaani wananiboa hakuna mfano
 
Nimesikia kuwa leo wale wazee wastaafu wa EAC ya mwanzo wamefunga barabara ya kivukoni pale mahakama kuu wakidai haki zao na kusema hawataondoka mpaka JK au Pinda aende kuonana nao.

Mwenye habari zaidi atuletee na picha vilevile!!!!!!
Hapo wamemshika pabaya, lazima hiyo hela ataitema, apende asipende.
Wenye madai halali wote huu ni muda muafaka kumtoza hiyo hela, maana akiapishwa tu ndo imekula kwenu!
 
Nimefikishiwa taarifa na jamaa yangu aliyepo maeneo ya mahakama kuu, DSM kwamba wazee wa iliyokua Jumuiya ya Afrika Mashariki wamezua kasheshe baada ya JAJI kujitoa katika kesi yao....kilichoshangaza zaidi ni kwamba wamefunga barabara na FFU wameshindwa kabisa kuwatoa.....mwenye info zaidi azimwage hapa...
 
jamani inauma mwisho wengine watafia hapo kotini kwa kusubiri mafao yao!!!:A S 13:

Ukiweka siasa pembeni, 'burden of proof' iko mikononi mwa hawa wazee. wafanyakazi wa kudumu na wengi ya wale wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyokufa karibu wote walikwisha lipwa. waliokuwa wamebakia wanadai ni wale waliokuwa vibarua kule bandarini ambao walikuwa hawafanyi kwa mkataba na wala hawakuwepo kwenye ajira ya kudumu na baada ya kuvunjika Jumuiya wengine wakajitokeza kudai haki zao bila taratibu kamili kuwa zimefuatwa. Waliowengi waliokuwa na ajira za kudumu au wanauthibitisho kamili wa barua zao za ajira, salary slips na kupandishwa vyeo walikwisha lipwa fedha zao.

Kwa bahati mbaya wengine walikuwa hawajuwi haki zao, na wengine walikuwa hawajuwi jinsi ya kudai haki zao ndiyo sasa unakuta baadhi ya watu kama hao wanadai mafao lakini pesa ya serikali kwa bahati mbaya haitoki kiholela na kama wakilipwa kienyeji, nina amini kabisa kuwa humu humu ndani siku moja tutakuja kusema ufisadi ulifanyika katika malipo yao.

Tuwachie Mahakama ifanye kazi yake:tonguez:
 
Nimefikishiwa taarifa na jamaa yangu aliyepo maeneo ya mahakama kuu, DSM kwamba wazee wa iliyokua Jumuiya ya Afrika Mashariki wamezua kasheshe baada ya JAJI kujitoa katika kesi yao....kilichoshangaza zaidi ni kwamba wamefunga barabara na FFU wameshindwa kabisa kuwatoa.....mwenye info zaidi azimwage hapa...

....hii ya leo ni hatari hatari kabisa.....leo mjini kuna foleni ya kufa mtu ..wazee wameesema wamechoka na ahadi ....wameamua bora wamuharibie..wakose wote...tangu saa tatu asubuhi barabara ya mahakama kuu haipitiki,,,,FFU wametanda ..na bado wamegoma kabisa ......nimetoka maeneo hayo sasa hivi na imenichukua masaa mawili kufika upanga ...just from Kilimanjaro hOtel
 
Ukiweka siasa pembeni, 'burden of proof' iko mikononi mwa hawa wazee. wafanyakazi wa kudumu na wengi ya wale wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyokufa karibu wote walikwisha lipwa. waliokuwa wamebakia wanadai ni wale waliokuwa vibarua kule bandarini ambao walikuwa hawafanyi kwa mkataba na wala hawakuwepo kwenye ajira ya kudumu na baada ya kuvunjika Jumuiya wengine wakajitokeza kudai haki zao bila taratibu kamili kuwa zimefuatwa. Waliowengi waliokuwa na ajira za kudumu au wanauthibitisho kamili wa barua zao za ajira, salary slips na kupandishwa vyeo walikwisha lipwa fedha zao.

Kwa bahati mbaya wengine walikuwa hawajuwi haki zao, na wengine walikuwa hawajuwi jinsi ya kudai haki zao ndiyo sasa unakuta baadhi ya watu kama hao wanadai mafao lakini pesa ya serikali kwa bahati mbaya haitoki kiholela na kama wakilipwa kienyeji, nina amini kabisa kuwa humu humu ndani siku moja tutakuja kusema ufisadi ulifanyika katika malipo yao.

Tuwachie Mahakama ifanye kazi yake:tonguez:

...Are you really?? Pesa ya Serikali haitoki kiholela?? Puliizi! So why do we have EPA, Meremeta, RichMonduli etc etc...????
 
Laana...laana....laana...laana...CCM hapo hamtoki kwenye tope la laana..
 
Leo katika mahakama ya kisutu, wazee wagoma kuondoka na kusimamisha shughuli za mahakama kwa muda..wataka Kikwete aje kutoa majibu yanayoeleweka.
 
Laana...laana....laana...laana...CCM hapo hamtoki kwenye tope la laana..

WAZEE WA EAST AFRICA YA ZAMANI WACHARUKA DAR; NI BAADA YA JAJI KUJITOA KESI YAO Y MADAI YA MALIPO

Baadhi wakijilaza mbele ya gari la polisi wa kutuliza ghasia la maj ya muwasho

Wakisali swala ya Dhuhuri poapo hapo barabarani mbele ya mahakama kuu

MSAJILI wa Mahakama, Francis Mutungi, akiwatanabahisha wadai hao wa iliyokuwa Afrika Mashariki, kipi kitafuatia baada ya Jaji wa Mahakama Kuu, Njengafibili Mwaikugile kujitoa kesi yao.

BAADHI ya wafanyakazi wa Mahakama Kuu wakiwa ndani ya geti wakati vurumai za wadai hao zilipokuwa zikiendelea nje ya jengo kwenye barabara ya Kivukoni

WAZEE waliomo katika madai hayo, wakila chakula cha mchana
 
Ni warithi wa warithi hao....yaani mfanyakazi alikufa bila kulipwa...mwanae akarithi madai nae akafa...sasa hao ni wajukuu wa mdai mwenyewe....kumbuka ni toka 1977 wanadai

Hii kali kweli kweli! halafu mbona kawa wengi wao wana bagarashia na kujifunga shungi ama ni kujikinga na jua?
 
Back
Top Bottom