Wazanzibari ni jamii yenye asili na ustaarabu mseto (cosmopolitan) na sio jamii ya kibantu

Unataka kusema watanganyika?

Unapiga ramli chonganishi?

Ninachojua ni kuwa washirazi na waarabu walitokea mashariki ya mbali wakaja kwenye visiwa hivyo na pwani ya afrika mashariki. Akili ya kawaida tu inaonesha kuwa hawakukuta visiwa hivyo vikiwa vitupu bila watu. Walikuwepo watu na bila shaka walikuwa ni watu weusi wenye asili ya Bara la Afrika. Washirazi ni wakuja, waarabu ni wakuja, wahindi, wabulushi wote ni wakuja. Ukweli ndio huo hata kama unawauma waarabu koko ambao hawapokelewi uarabuni na sasa wanalazimisha kuwa wao Waliumbiwa na Mungu hapo visiwani.
 
hawa ni watumwa kutoka tanganyika wakipelekwa super market ya utumwa znz,
hakuna mtu wa znz aliefanywa mtumwa kwa sababu biashara ya utumwa ilipo anza zanzibar watu wake tayari walikua na serikali inayo jiendesha
tanganyika, malawi na kwengi neko hakukua na serikali yoyote, ma chief walikua wakiwauza watu wao kwa kupewa vioo!! ama wanawake !!!
hivyo hizi picha za kuchora hazia shirii kuwa hawa ni wa znz bali ni wa bara ambao wanapelekwa znz kuuzwa
hawana uhusiano na znz nz hawakuwa na haki ya kiraia huko,
tusichanganye mambo!!
hawa uta waona kule marekani ,na ulaya amabo pengine ndio kina Ophrah ama Tyson, na wengine wapo Kule salala Oman, ukienda kule utawaona 'waarabu' weusi kuliko mnyachusa

hawa hawakukuta znz haina watu bali walikuwapo,,,, na wao walikua wapita njia tu ..wakinunuliwa haya hawooo ulaya...
Waarabu ndio walioiita nch yenu Zenjbar, nchi ya watu weusi (ref wikipedia). Baada ya hapo ni uongo tu. Ukipora je ni mmiliki asilia. Let Zanzibar remain cosmopolitan, a land of allaces. It has never happened in this world that one race has annihilated another completely from the face of the earth. As long as you believe in cosmopolitanism, then your view of Bantus not being part of modern Zanzibar makes you a non cosmopolitan.
 
WAZANZIBARI NI JAMII YENYE ASILI NA USTAARABU MSETO (COSMOPOLITAN SOCIETY) NA SIO JAMII YA KIBANTU (KIAFRIKA)

Written by Ahmed Omar Khamis| 04/08/2012

Kabla ya kuja mkoloni wa kiingereza Zanzibar, wazanzibari wa asili mbali mbali kama walivyo hivi sasa walikuwa wakiishi kwa mapenzi makubwa bila ya chuki za ukabila na urangi, au kwa lugha nyengine, waliishi bila ya mimi ni nani na wewe na nani.

Muingereza alikuja kuwaundia wazanzibari vyama vya kikabila na urangi. Vyama hivyo yaani jumuiya za kikabila ni kamavile Arab association, Shirazi association, African association, Indian association na jumuiya nyengine.

Wazanzibari nao wakavishabikia vyama hivi vya kikabila na kila mmoja akawacha kupigania maslahi ya uzanzibari na akapigania maslahi ya kabila lake. Lakini hayo yalikuwa ni mafanikio makubwa kwa Muengereza, kwani ni sera yake muhimu ya ukoloni ya wagawe uwatawale (divide and rule).

Kuanzia harakati za kutafuta uhuru chama cha ASP na viongozi wake akiwemo kiongozi mkuu Karume waliukejeli na kuupiga vita ukweli kwamba wazanzibari ni watu wa asili na ustaarabu mseto na kujaribu kuyatenga makundi yote ya kizanzibari yalio na asili zake kutoka nje ya bara la Afrika kama vile waarabu, wahindi, magoa nk. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba hata washirazi wenye asili zao kutokeaIranambao ndio wanaofanya asilimia kubwa ya wazanzibari nao walipigwa vita.

Kama hilo halitoshi hata wakomoro wenye ngozi nyeupe lakini wenye asili zao kutokea katika bara la Afrika nao walikejeliwa na kukataliwa. Kwa viongozi wa ASP mzanzibari namba moja au mzanzibari asilia na mwenye hadhi kubwa ni lazima awe mwafrika mwenye ngozi nyeusi. ASP iliupigia kelele, kuunadi na kuutukuza uafrika pamoja na ngozi nyeusi na kuzidharau jamii zote za kizanzibari zilizobaki.

Kabla ya mapinduzi ASP na viongozi wake walijaribu kuwaheshimu washirazi wakifahamu bila ya wao na wingi wao ushindi kwa ASP ingelikuwa ndoto. Mara tu baada ya mapinduzi na ASP kushika hatamu chuki dhidi ya ushirazi na washirazi zikadhihirika.

Serikali ya Karume ilipambwa na viongozi wenye asili zao kutokea bara hususanTanganyika. Hii inajionyesha hata kwa majemedari wa mapinduzi na wajumbe wa baraza la mapinduzi la mwanzo lilikuwa na watu wengi zaidi wenye asili zao kutokea bara. Hii iliwafanya wafikirie kwamba serikali ya mapinduzi ni ya wazanzibari wa asili za bara na waliobaki ni watu wa daraja la pili. Baada ya mapinduzi Karume aliwataka watu wote wenye asili ya kikomoro kuomba uzanzibari (Burgess 2009:204). Kwa kuwa Karume mwenyewe alikuwa na asili yake kutokeaMalawialiwaogopasanawashirazi. Katika akili yake Karume aliwaona washirazi ni watu wanaoringa na kujidaikamawazanzibari halisi. Hivyo basi aliwalazimisha washirazi nao kubadilisha makabilayao.

Washirazi wengi walilikataa agizohilola Karume hususan wapemba. Wengi wa washiraziPembawalisema wao hawana kabila jengine mbadala mpaka Karume atakapowapatia baba wengine. Hivyo basi hali halisi ya ugozi na ukabila ilipamba moto zaidi baada ya mapinduzi kuliko kabla.

Wapigaji na wachezaji wa ngoma hiyo chafu ya ukabila baada ya mapinduzi walikuwa viongozi wa serikali ya mapinduzi na wajumbe wa baraza la mapinduzi la mwanzokamavile Karume mwenyewe, Seif Bakari na Abdalla Said Natepe, Mungu awarehemu.


Baada ya mapinduzi vitabu vyote vya historia vilivyofundisha ukweli kuhusuZanzibar, maisha ya masultani, na urithi wa ustaarabu mseto vilichomwa moto (Burgess 2009). Tukio moja la uchomaji huo lilifanyika eneo la Lumumba Unguja mbele ya macho ya maelfu ya watu. Badala yake mwenyekiti wa Youth league, Seif Bakari aliandika kitabu kipya kilichokua kikisomeshewa watoto mashuleni. Katika kitabu chake hicho, Seif Bakari anadai kuwa yote yaliopita kabla ya mapinduzi yalikuwa si chochote bali ni dhiki na dhuluma.

Katika kuzidi kuchonga chuki miongoni mwa wazanzibari weusi dhidi ya wenye ngozi nyeupe, Abdalla Said Natepe ambae ni mjumbe wa mwanzo wa baraza la mapinduzi na mjumbe wa kamati ya watu 14 alikuwa akifanya mikutano ya hadhara kuwaaambia watu hadithi za uzushi. Miongoni mwa hadiuthi hizo ni kuwa waarabu waliwalazimisha waafrika kupanda minazi kisha wakawa wanajifundishia shabaha kwa kuwatungua kwa risasi.

Hadithi nyingine ni kuwa waarabu waliwalazimisha wanawake wa kiafrika kufyagia barabara kwa maziwayaona waja wazito wa kiafrika walip[asuliwa ili bibi wa kiarabu ajue mtoto amekaaje tumboni. Mafundisho haya yamekuwa yakitolewa mashuleni kwa muda mrefu ili kutia sumu katika akili za watoto wakishirazi na kifrika dhidi ya waarabu.

Nyimbo za uafrika dhidi ya asili nyengine zote ziliendelea kuimbwa ndani serikali ya mapinduzi kupitia warithi wake wenye misimamo mikali ya uhafidhina wa ugozi na umapinduzi kwa lengo la kulinda malengo na uhalali wa mapinduzi hayo.

Kuthibitisha kasi na nguvu za uhafidhina huu na chuki dhidi ya watu wasiokuwa na asili ya kiafrika ndani ya Zanzibarni maneno ya Omar Ramadhani Mapuri, ambae yeye mwenyewe ana asili yake kutoka Tanzaniabara, aliyekuwa Waziri wa elimu na Naibu waziri kiongozi katika awamu ya nne ya Rais Salmin Amour. Kupitia kitabu chake, Zanzibar Revolution, Achievements and Prospects, kitabu ambacho kinazungumzia kiwango cha juu cha ukabila katika enzi za ustaarabu duniani, Mapuri ameweka wazi hisia zake kali dhidi ya watu wasiokua waafrika ndani yaZanzibar.

Lengo kuu la Mapuri katika kitabu chake ni kuwataka wazanzibari wenye asili za kiafrika kuungana dhidi ya kile anachokiita chokochoko na uchokozi wa nchi za magharibi na waarabu ambao chini kwa chini kwa mujibu wa Mapuri wanataka kurudisha tena ushawishi waoZanzibarkama ilivyokuwa kabla ya mapinduzi. Umoja huu ambao Mapuri anawaasa wazanzibari ndio ule ule uliotumika katika harakati za uhuru na mapinduizi ya 1964.

Katika kitabu chake pia Mapuri anakana kwa nguvu zote mauwaji yaliyofanywa na mapinduzi ya 1964 na kwa mujibu wa mawazo yake yale yanayoripotiwa kuwa ni upotezaji wa roho za watu kwa mgongo wa mapinduzi ya 1964 ni uongo mtupu na kusisitiza kwamba watu waliokufa kutokana na mapinduzi hayo ni wachache mno. Hata hivyo katika kitabu chake anadai kuwepo kwa nyaraka zinazobainisha azma ya serikali ya Shamte na Sultani iliyopinduliwa ya kutaka kuuwa raia wengi wa kiafrikakamani kulipiza kisasi kwa mauwaji ya waarabu waliouliwa kufuatia uchaguzi wa juni 1961 ijapokuwa hakubainisha katika kitabu chake nyaraka hizo zilipo.

Mapuri anadai nyaraka hizo zinathibitisha kwamba serikali ilipanga kuuwa waafrika sitini (60) kwa kila mwarabu mmoja aliyeuliwa Juni 1961. Mapuri pia anadai nyaraka hizo zinathitisha azma ya serikali ya Shamte na Sultani kuzitaifishamalizote za waafrika wasio na asili za kizanzibari. Hakumalizia hapo Mapuri pia ameandika kwamba Serikali ya Shamte ilikuwa na lengo la kuwafanya watumwa wazanzibari wote wenye asili ya kiafrika na hatimae Zanzibar kutangazwa kama ardhi ya waarabu.

Kikubwa zaidi ambacho pia Mapuri amewatanabahisha wazanzibari katika kitabu chake ni azma ya Serikali ya Shamte iliyopinduliwa kuwauwa watoto wote wa asili ya kiafrika na wanawake wenye asili ya kiafrika kulazimishwa kuolewa na waarabu kwa malengo ya kutokomeza ngozi nyeusiZanzibar.

Alichokifanya Mapuri bila shaka lilikuwa si jambo geni katika historia yaZanzibar. Ni marudio tu ya yale yalioanzia miaka ya 1960 ya mapambano ya makabila katika kugombania kumezwa, kufunikwa au kutokomezwa na makabila mengine.

Ni jambo la kushangaza mno kwa enzi ambayo vuguvugu la kihistoria la ukabila na uasili tayari limeshasahaulika, kiongozi wa ngazi za juu katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibaranapika upya migawanyiko ya wazanzibari kwa misingi ya rangi, ngozi na wanakotokea mababu zao.

Kiongozi kama huyu bila shaka ana dhima kubwa ya kuwaunganisha wazanzibari walio na asili na utamaduni wa kila namna karibu kutoka pembe zote za dunia lakini badala yake anashajihisha na kuhimiza umoja na muungano wa baadhi ya wazanzibari dhidi ya wenzao. Hata hivyo sio Mapuri peke yake katika viongozi wa leo wanaopiga kelele za ukabila na uasili ndani ya Zanzibarya kisasa.

Wapo wenzake Mapuri ambao wao wamefika mbali zaidi kwa kudai kwamba vijukuu na vinying'inya vya waarabu hawapaswi kupewa madaraka ya Zanzibarkwa kunasibika kwao na kabila la wapinga mapinduzi ya 1964. Katika kitabu chake, Kwaheri ukoloni kwaheri uhuru, Harith Ghassany analizungumzia hivi suala hili.

"Fikra ya uzalendo ya Pan-Africanism ambayo ilikuwa ikipigiwa kelele na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa na misingi kwamba kila asiye "Muafrika" ni mgeni (wakuja) Afrika na kwa maana hiyo pia ni mgeni Zanzibar hata kama alizaliwa na alikuwa na mizizi mirefu na mipana ndani ya Zanzibar.

Kinyume chake kila aliyekuwa ana asili ya Kiafrika (kibantu) na hata kama hakuzaliwa na wala hana mizizi mirefu ndani ya Zanzibar basi ana haki zaidi juu ya kuweza kutawala kwa sababu tu ni "Muafrika." Hapa sharti ifahamike kwanza kuwa neno "Afrika" linatokana na neno Ifriqiya, ambayo wanahistoria wanathibitisha ilikuwa ni jimbo la Kaskazini ya Afrika katika nchi ambayo kwa sasa inajulikana kwa jina la Tunisia.

Ibn Khaldun, mwanafalsafa wa historia maarufu duniani na baba wa sayansi ya jamii (sociologist) aliyeishi miaka 676 nyuma, amemzungumza katika kitabu chake Mfalme wa zamani wa Yemen Afriqus Bin Qays Bin Sayfi. Kwa mujibu wa Ibn Khaldum Mfalme huyu aliishi wakati wa Nabii Musa au labda kidogo kabla yake. Ibn Khaldum anathibitisha kuwepo kwa mfalme huyo kutoka Yemen ambaye jina lake hilo inawezekana sana likawa moja wapo wa asili ya jina "Afrika".

Mawazo yaliyoenezwa kila upande ni kwamba Zanzibar ni ya Muafrika mweusi mwenye asili ya bara peke yake kuliko Muafrika mwingine yeyote hata kama amezalika huko Zanzibar kwa dahari nyingi. Mawazo haya yanatokana na fikra kuwa "Bara la Waafrika" ni Bara la watu weusi tu. Watu weusi hao tena ni wale wanaotokana na asili ya Kibantu na Wabantu hao bila shaka wawe hawana kabisa asili au uhusiano wowote na Waarabu.

Wenye mawazo haya bila shaka walisahau kuwa wanalitenga kundi kubwa la Waafrika wa Kaskazani katika nchi za Ethiopia, Somalia, Djibouti, Eritrea na Mauritius. Halkadhalika mawazo hayo yamewatenga wazungu wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Kenya. Pia mawazo hayo yamewatenga Mayahudi na Wahindi wazalendo wa Afrika, na makabila yote ya watu ambayo yana chimbuko lake katika bara hili" (Gassany 2010).

Wazanzibari ni watu walio na asili zao nyingi na ustaarabu mchanganyiko ulizoanzia mbali. Asili za kiarabu, ki-pashia, kihindi, kitanganyika, kiganda, kikenya, kimsumbiji, kikomoro, kinyasa, kisumeri, kiassiri, kisomali, kiabisini, kifoniki, kidiba, kidebule, kireno, kibaluchi, kikurdi, kijojia, kichina, kisrilanka nk Wengi wao ni machotara, hakuna awezae kukaza mdomo akamtukana mbantu, akija akitanabahi kumbe kamtukana babu yake, au akakaza mdomo akamtukana mwarabu, akitanabahi kamtukana mama yake.

Uarabu, ubantu, uhindi, na asili nyengine zote za wazanzibari zilizopo kamwe hazibandukani na uzanzibari na bila ya kundi moja tu katika hayo ni sawa na mwanadamu asivyokamilika akikosa baadhi ya viungo vyake.

Tunaishukuru sana serikali ya ya Dr Shein ya Umoja wa kitaifa kwani imefanikiwa kufuta madoadoa ya kibaguzi baina ya wazanzibari wenyewe kwa wenyewe na kuusimika ule ustaarabu mseto (cosmopolitanism) unaomtambua kila mzanzibari kua ni mzanzibari bila ya kuangalia rangi yake, nywele zake pua yake.

Wazanzibari tusurudi nyuma haya ya kufunzwa kubaguana ndio yaliyotufikisha hapa na kuipoteza nchi yetu na hatimae kuingia mikononi mwa Tanganyika. Tuungane kwa umoja wetu turudishe heshma ya Zanzibar yetu yenye mamlaka kamili kama ilivyowahi kutamalaki hapo kabla ya 1964.

Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza
Bwana mtoa mada kabla ya kutoa povu hebu turudi kwenye jina la Zanzibar lenyewe ambalo waarabu ndio waliotowa na asili yake ni zenjbari, nchi ya watu weusi, sasa watu weusi ni wabantu au waarabu? pili wakati mwinyi mkuu anatawala kabla ya ukoloni mkongwe wa abu said, ama sultan seyyid said kuvamia, je wazawa walikuwa na utamaduni gani? na kama utawala wa sultani seyyid said si ukoloni wapi wananchi wa zanzibar chini ya mwinyi mkuu kiongozi wao walikubali kuwapa wageni wa kiarabu nchi yao kutawala? Na jee ni kwa nini kiongozi huyo wa wazalendo mwinyi mkuu aliuwawa ikiwa aliridhia nchi yake kuwapa wavamizi wa kiarabu kutoka Oman, akina sultan seyyid said na vizazi vyake?
Ukweli siku zote hubaki ukweli, zanzibar ni nchi ya watu weusi tiiii, wabantu na waarabu ni wavamizi na ndio maana mapinduzi ya 1964 yakaja kurekebisha hilo.
 
Cuf ya Maalim ni chama kinachopata pesa toka kwa Sultani aliepinduliwa. (Maalim anakutanishwa na Sultani Jemshid Qatar, na Karume anajua) Kwanini tunachezea shilingi chooni? Pia kinaitwa Hizbu kama chama asilia ya Sultani yaani kwa kiswahili ndio chama cha wananchi. Chama kichafu hichi kwa amani na mustakabali wa nchi yetu. Chama kifutwe mara moja. Migogoro mingine sio ya lazima, tuachwe tufanye kazi, hawa wanaotamani uarabu kama suluhu ya matatizo ya kiuchumi waone Siria, Somalia na Yemen wakigombania kula mizoga ya mbwa na watu. Futeni chama chenye ndoto ya piga ua kuigawa Tanzania.
 
Hivi ngozi nyeusi imewakosea nini kila shemu duniani inasakwa.Hivi mnaenda mbinguni mkakuta Mungu na malaika ni weusi mtajisiaje?
 
Mfalme wa Qatar alipokuja tu Zanzibar tena kwa njia ya baharini hapo hapo Karume na Maalim wakakutana, Maalim akaitambua serikali ya Karume, Karume akamuingiza Maalim katika serikali kama Makamo wake, jaribio likafanywa la Karume kuongezewa muda wa Urais ili azidi kuwaunganisha eti Wazanzibari, chokochoko za kudai mafuta na gesi ya Zanzibar yakaanza yakiongozwa na Mansouri CCM na Jussa kwa CUF (sasa wote cuf) vikundi vya ugaidi UAMSHO vikaanza kazi bila kuficha kuidai Zanzibar kwa kuwachomea Wabara, kuuwa Viongozi wa Kikristo. Meli za kina hao hao nje zenye bendera ya Tanzania zikaanza kusafirisha kila kilicho gharamu. Je nani atapinga kuwa kwenye Meli ya Mfalme wa Qatar hakuwepo pia Mfalme wa Zanzibar? Kwanini baada tu ya Meli ile Zanzibar ikafanya marekebisho ya katiba yake ili ianze kwa kusomeka "Zanzibar ni nchi?" Badala ya Zanzibar ni sehemu ya Tanzania? Asante Mungu Anko Magu yupo, uozo wote utafumuliwa.
 
Wazanzibari wengi sana ni wagonjwa, wanabishana kutwa kujiita Waarabu, mwenye ngozi nyeupe kidooogo tu mfano wa kina Chenge basi wao ni Waarabu asilimia 100 na hadi sauti wanabadili, kubana pua, kujitenga, kudharau weusi, kutembea kwa kujivuta vuta hivi kimlegezo eti kiarabu. Yaani Zanzibar unacheka akili ya kuku.
 
Nguruvi3,

hapana wa znz ni wa znz tu hawana uhusiano na watanganyika, wapo wahamiaji ambao walifika zanzibar kutokana na masalia ya biashara ya utumwa. itakumbukwa kuwa zanzibar ndio ilikua ndio soko lautumwa afrika mashariki , wafanya biashara wa utumwa wa kizungu, kiarabu na washirazi kwa kushirikiana na ma chifu wa tanganyika walifanya biashara hii na znz ndio ilikua ndio super market yao.hakuna mshirazi aliefanywa mtumwa, mara baada kupigwamarufuku biashara ya utumwa kutokana na uvumbuzi wa viwanda hivyo nguvu kazi hii haikutakiwa tena huko ulaya wale masalia ambao hawakupatwa kuuzwa ndio waafrika walio bakia zanzibar na ndio baadhi yao wapo.

kundi la pili la watanganyika ni wale waliokuja znz katika karne ya 20, hawa kufata neema ya uchumi na kazi , hawa wamo kina Ali hassan mwinyi, Aboud Jumbe Mwinyi, Seif Bakari , Edington Kisasi, Sepetu, David WAKATI, Abeid Aman Karume(alitokea Malawi)
hakuna mshirazi aliekubali ku olewa na mtanganyika ama mkenya ama mmalawi ila wachache sana, lakini washirazi,wapemba , na watumbatu walikuwepo znz miaka na miaka na ndio asili yao znz , watanganyika hawana historia yoyote kwamba waliingia znz kabla ya utumwa.

inajulikana wazi hapa dar es salaam na tanga na bagamoyo miaka 300 iliyopita hapajakuwa na mhaya , myachusa,mchaga, ama mhaya aliyerfika maeneo ya pwani, seuze ku - venture safari ya bahari kwenda znz !!! huu ni ukweli, kabla ya kujengwa reli watanganyika wa kati ya tanzania hawakuwahi kuja huku pwani hata siku moja, sasa wa znz walikua ni wa znz na wa tanganyika walikua wa wabara tu, ambao walikua chini ya ma chief wao, na taratibu zao, za kiafrika , huu ndiio ukweli, hakuna historia yoyote inayosema amabyo ina mshiko kama kuna mhaya znz, ama mchaga, ama mhehe,ama mnyachuza, laiti ingekuwa kuna slight intergration ya watu wa bara na znz basi wangeacha atahari japo kidogo,kwenye tanaduni ama lugha.

wareno walifika pemba na kutawala chini ya miaka 100 lakini walia cha athari ya lungha na mitaa. seuze leo iwe jamaii ya znz iwe ina asili ya bara ama tanganyika halafu kusiwe na athari yoyote ya kutoka mrima,!! ila ni ukweli kwamba znz ndio imeacha athari kubwa upande wa tanganyika , kwa dini, uislam. hata ukristo, wazungu walianzia znz, wame acha athari ya lugha ya kiswahili.

watu wa znz ni wa visiwani tu hawakua na asili ya bara tuache siasa za kuwadanganya watu.

znz hakuna watu wenye asili ya kimasai
Kwakuwa hakuna watu wenye asili ya kimasai, kichaga na kihaya, hiyo inadhihirisha kwamba hakukuwa na watu wenye asili ya kizaramo, kimatumbi nknk? Au hoja yako ni kwamba hakuna mwenyeji wa eidha Tanga au Mombasa au Lindi aliyewahi kufika Zanzibar kabla ya Mwarabu kufika hapo?

Historia ya lugha ya kiswahili; lugha kuu izungumzwayo Zanzibar hata kabla ya Muungiliano na wageni toka mataifa ya nje, ni kibantu. Inajinasibisha na lugha zote za kibantu zilizoko hata mbali zaidi ya Zanzibar, ilifikaje huko? Asili ya wazanzibar ni wabantu, hata wageni wa mwanzoni wamelithibitisha hilo.
 
HiLI SOMO PEVU, Maana mabo mengi yamekorogwa na uongo..
akuna anaesema znz ni ya waarabu..hata siku moja...ila wapo waarabu wahamiaji .warabu walifika znz 1628 baada ya "WAZANZIBARI HALISI AMBAO HAWANA UUSIANO NA TANGANYIKA WALA WARABU" chini ya kiongozi wao Mwinyi mkuu wa unguja na pemba kupata dhiki ya utawala wa kishenzi wa wa Wareno, walipeleka ujumbe Oman kuomba msaada wa kijeshi kuja kuwasaidia kuwatoa wareno katika ardhi yao.
(wa oman wao waliwatoa wareno huko kwao)
hapa ndipo wa Oman kuja kwao Znz , lakini haikua rahisi kwani wareno walikuwa tayari wapo coast yote mpaka lamu mombasa kilwa hadi chini maputo.

wa oman hawa waliweza kuwatoa wareno katika pwani hizi na ikabaki kule msumbiji tu.
wengi walifariki na kuteswa na wareno lakini waliwatoa ndugu zao kutoka katika mateso ya wareno. vita hii ilichukua zaidi ya miaka 50 na hapa askari kwa askari wa ki oman walikua wakija huku na ndio mwnzo wa wao kuhamia pwni ya afrika mashariki.

sasa utaona ile jamii ya znz ya kina mwinyi mkuu walikua ni wa znz wa asili na asili yao ni visiwani.

warabu waliwakuta
watumwa watanganyika na kutoka kwengine nao walikuja wakawakuta
wahindi waliwakuta

na wazungu waliwakuta

visiwa hivi vilikuwa na wenyeji wake na ndio hao washirazi

hakuna anaesema kwamba waraabu ndio wenyeji , wao wanaajujua kwamba wao ni Muhajirun, sawa na wabongo, wote ni walowezi,
walipokuja wa oman znz tayari ni nchi ya kiislam, kulikuwa tayari kuna misikiti, mingi sana, nao hao wa oman walijenga yao ya madhehebu yao ya kiibadhi.

ndio maana znz wenyeji wote ni wa madheheb ya sunni mabyo si madhehebu ya watawala wa ki oman.

ukweli utabaki znz ina wenyewe tangu enzi na enzi...
kabla ya mwarabu wa oman
kabla ya kuja wa tanganyika kwa njia ya utumwa
na tanganyika ina wenyeji wake
kila nchi ina wenyeji wake
watumwa walioplekwa marekani ni zaidi ya 20,000,0000 na hawa hawafanyi kuwa wao ndio asili yao ni marekani asili yao ni afrika, wenyeji ni red indians hata kama wazungu wahamiaji wa huko wali wachinja chinja
kule Burma kuna issue sasa hivi wenyeji MA BUDA wanawatoa kwa nguvu wahamiaji waislam, asili ya Rongyia, na hawa walihamia Burma miaka zaidi ya 200.
siasa za uongo ambazo ndio hizo zinazowataka kuwafanya wazanzibar waamini kuwa asili yao ni bara ili kuhalalisha muungano , lakini wao wenyewe sasa wamengamua kuwa wao ni wazanzibar na waislam na wana asili yao ambayo haina uhisiano na uwarabu wala utanganyika sasa kuna wanaosappurt dhana hii na wanaopinga...wana pinga kuoogopa aumoja wa znz
Kuna kosa moja kubwa unalifanya mkuu, la kuamini kwamba Zanzibar haikuwahi kukaliwa na watu kabla ya watu toka bara arabu kuja, (waoman waliwakuta na misikiti yao ya kiislamu), labda kama una uthibitisho kwamba uislam ulianzia Zanzibar na kuenea bara la Arabia.

Jina "Mwinyi" si jina lenye asili ya kiarabu wala jamii nyingine yoyote ile nje ya jamii za Pwani, wazaramo, Wakwele, Wakutu nknk, akna Mwinyimvua na mengineyo yametamalaki tangu enzi za mababu huko.

Vitabu vya kihistoria vya akina Ibin Batuta, ambao wao walikuwa ni waislam, wanakiri kuwakuta wenyeji hapo, waliokuwa na tawala zao, taratibu zao, lugha yao, na Mungu na dini yao. Misingi ya lugha ya kiswahili ni ya kibantu, na sitakosea nikisema tofauti baina ya kiswahili na kizaramo, ukiondoa maneno ya lugha za kigeni ni ndogo sana.
 
Kwa mwenye busara toka jamii ya wajitiao waarabu koko, busara ndogo kama ile imuwezeshayo paka kufunika kinyesi chake tu, angeshauri njia mbadala za kuishi kwa amani ktk Zanzibar na si kuandika utumbo kama huu wenye kufufua chuki za asili. Eti anasema jamii iliishi vizuri enzi za utawala wa mwarabu, Sijui mwandishi anaweza kulithibitishia ni mtawala yupi mweusi aliyetokelezea Zanzibar, tangu mkoloni mwarabu aitwae hii nchi?

Vipi kuhusiana na nyanja nyingine kama za kiuchumi, je walikuwepo wazanzibar weusi wenye kumiliki mali nyingi hata kuwazidi baadhi ya waarabu na washirazi ktk utawala wa waarabu? Kisiasa, je ktk ngazi za juu, weusi walishirikishwa kama viongozi pia?

Hawa ni watu wa ajabu sana, ndio maana duniani kote hawatafanikiwa kwa unafiki wao uliowajaa. Unadhani muizrael angemnyima chakula na mavazi na ujakazi mpalestina ktk utawala wake? Je kufanya hivyo kungetosha kuitwa ubora na ustaarabu? Unafiki haujawahi kumuacha mnafiki salama.
 
Bwana mtoa mada kabla ya kutoa povu hebu turudi kwenye jina la Zanzibar lenyewe ambalo waarabu ndio waliotowa na asili yake ni zenjbari, nchi ya watu weusi, sasa watu weusi ni wabantu au waarabu? pili wakati mwinyi mkuu anatawala kabla ya ukoloni mkongwe wa abu said, ama sultan seyyid said kuvamia, je wazawa walikuwa na utamaduni gani? na kama utawala wa sultani seyyid said si ukoloni wapi wananchi wa zanzibar chini ya mwinyi mkuu kiongozi wao walikubali kuwapa wageni wa kiarabu nchi yao kutawala? Na jee ni kwa nini kiongozi huyo wa wazalendo mwinyi mkuu aliuwawa ikiwa aliridhia nchi yake kuwapa wavamizi wa kiarabu kutoka Oman, akina sultan seyyid said na vizazi vyake?
Ukweli siku zote hubaki ukweli, zanzibar ni nchi ya watu weusi tiiii, wabantu na waarabu ni wavamizi na ndio maana mapinduzi ya 1964 yakaja kurekebisha hilo.

Upo mbali sana mkuu, kwanza punguza jazba.
Tunaomba ututhibitishie kama Winyiwakuu walikua ni waBANTU.

Mapinduzi ya 1964 yamekuja kurekebisha unavosema, lakini unafahamu kama Karume, Aboud Jumbe, Ali hassan Mwinyi, Seif Bakari, Natepe, Kaujore, Okello, Mfaranyaki, Yussuf Himid, Washoto, wanaitwa wanamapinduzi na watawala baada ya mapinduzi wote hawa hawajazaliwa Zanzibar?
 
Kuna kosa moja kubwa unalifanya mkuu, la kuamini kwamba Zanzibar haikuwahi kukaliwa na watu kabla ya watu toka bara arabu kuja, (waoman waliwakuta na misikiti yao ya kiislamu), labda kama una uthibitisho kwamba uislam ulianzia Zanzibar na kuenea bara la Arabia.

Jina "Mwinyi" si jina lenye asili ya kiarabu wala jamii nyingine yoyote ile nje ya jamii za Pwani, wazaramo, Wakwele, Wakutu nknk, akna Mwinyimvua na mengineyo yametamalaki tangu enzi za mababu huko.

Vitabu vya kihistoria vya akina Ibin Batuta, ambao wao walikuwa ni waislam, wanakiri kuwakuta wenyeji hapo, waliokuwa na tawala zao, taratibu zao, lugha yao, na Mungu na dini yao. Misingi ya lugha ya kiswahili ni ya kibantu, na sitakosea nikisema tofauti baina ya kiswahili na kizaramo, ukiondoa maneno ya lugha za kigeni ni ndogo sana.

Wakati Ibn batuta alipotembelea africa mashariki, Kulikua na utawala wa kisharazi kutoka Persia, Kamsome vizuri uyo ibn batuta mkuu.
 
Wakati Ibn batuta alipotembelea africa mashariki, Kulikua na utawala wa kisharazi kutoka Persia, Kamsome vizuri uyo ibn batuta mkuu.
Persia ni mchambawima ya leo au Comoro? Usitoke nje ya mada?
 
Wakati Ibn batuta alipotembelea africa mashariki, Kulikua na utawala wa kisharazi kutoka Persia, Kamsome vizuri uyo ibn batuta mkuu.
Inshu ilikuwa je Zanzibar ilikuwa empty wakati hao wanakuja hata wakawa wao ndo wenye asili? Ibn Batuta alikuwa ni raia wa nchi gani na aliabudu dini ipi? Zanzibar aliikuta ni nchi yenye watu wake wenye kumuuamini Mungu wao na dini yao na wenye kuongea lugha yao?
 
Kumbe yale Mapinduzi yalihitajika. Bila hivyo leo tungeambiwa nchi hiyo haiko Afrika. Cosmopolitanism heterogeneity haiondoi "identity" ya kabila moja moja. Na hiyo ndio sifa moja kuu ya cosmopolitan society. Zinj ambapo tumepata Zanzibar maana yake nyeusi. Wabantu kibso wapo Zanzibar ukiacha Washirazi wengineo. Wabantu asikia wengi tu.
 
Wazanzibari wengi sana ni wagonjwa, wanabishana kutwa kujiita Waarabu, mwenye ngozi nyeupe kidooogo tu mfano wa kina Chenge basi wao ni Waarabu asilimia 100 na hadi sauti wanabadili, kubana pua, kujitenga, kudharau weusi, kutembea kwa kujivuta vuta hivi kimlegezo eti kiarabu. Yaani Zanzibar unacheka akili ya kuku.
Hahaha
 
ELIMU YA MADRASSA BALAA
1Kumbe kwako wakoloni ni waingereza sio seyyid said na said barghash?
2,mgawanyiko haukwepo kabla ya waingereza kuja?????!!!!! wakat warabu waliendesha biashara za utumwa? eg tipu tip
3,zanzibar watu weusi walikwepo kabla ya wajinga kama wewe waliokubali uislam na mbaya uarabu (jina lako)
4,je kama ni hivo kwanini karume alimpindua jamsheed kama hakuwa na udaraja na ukabila? tangu lini mwarabu akajiona sawa na kiumbe duni (mutu nyeusi) kama wewe?
5 soma elim dunia kaka hyo ya madrasa itakupeleka kusiko
Hauna akili hata mwandiko wako tu unatuthibitishia hilo.
 
Inshu ilikuwa je Zanzibar ilikuwa empty wakati hao wanakuja hata wakawa wao ndo wenye asili? Ibn Batuta alikuwa ni raia wa nchi gani na aliabudu dini ipi? Zanzibar aliikuta ni nchi yenye watu wake wenye kumuuamini Mungu wao na dini yao na wenye kuongea lugha yao?

Tatizo lenu mnazungumza kinadharia na si kihalisia. Hebu twambieni mnakadiria ni kipindi gani wa bantu walianza kufika Zanzibar?
Waarabu na Wapersia tarehe za makadirio zipo sasa hebu tupeni za wabantu.
 
Back
Top Bottom