Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 1,689
- 3,264
Mapinduzi ya Zanzibar yaliendeshwa na bwana John Okello. Hili halina ubishi. Mapinduzi yalianza saa tisa za usiku yakiongozwa na Okello na watu mia kadhaa wakiwa na silaha za jadi.
Walivamia vituo vya polisi na huko ndiko walikopata bunduki. Kufika saa moja asubuhi Okello akatangaza redioni kuhusu mapinduzi huku akijitambulisha kama Field Marshall. Wakati huo wote Karume alikuwa yuko huku Tanganyika.
Kufupisha stori: Baada ya Karume kushika madaraka Okello alifukuzwa Zanzibar kwa kuzuiwa kuingia Zanzibar akitokea Tanganyika. Akaenda Kenya na baadaye Uganda akiwa kapuku.
Naelewa kwa nini Karume alimfukuza Okello, hata mimi ningefanya hivyo. Kwanza alikuwa mtu mkatili sana, mwenye kuongea maneno ya kikatili hasa. Wakati wa mapinduzi alikuwa akipiga kelele watu waue na kuchinja waarabu. Inasemekana waarabu zaidi ya 20,000 waliuawa. Wanawake walibakwa vibaya na kuuawa. Kuwa na mtu mkatili kama kichaa ni hatari sana. Alifaa kufukuzwa.
Waarabu waliochinjwa wakati wa mapinduzi.
Pia jamaa alifaa kufukuzwa sababu hakuendana kabisa na jamii ya wazanzibari, alikuwa ni wa kuja hasa. Alikuwa anapiga kelele akidai ni mkombozi wa kikiristo huku akiwa na lafudhi yake nzito ya Uganda. Kwa Zanzibar ambayo majority ni Waislamu hawakumuelewa kabisa swaga zake.
Sababu za kumfukuza Okello zinakubalika kabisa. Lakini mchango wake kwenye mapinduzi ya Zanzibar ni mkubwa sana. Huyu ndiye aliyewakomboa Wazanzibari kutoka ukandamizwaji wa serikali ya Sultani. Ndiye aliyewatoa unyonge wanahitaji kumshukuru. Serikali ya Zanzibar haioni kuwa inahitajika kuwafanyia kitu watu wa familia ya bwana Okello.