Wazanzibari ni jamii yenye asili na ustaarabu mseto (cosmopolitan) na sio jamii ya kibantu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
WAZANZIBARI NI JAMII YENYE ASILI NA USTAARABU MSETO (COSMOPOLITAN SOCIETY) NA SIO JAMII YA KIBANTU (KIAFRIKA)

Written by Ahmed Omar Khamis| 04/08/2012

Kabla ya kuja mkoloni wa kiingereza Zanzibar, wazanzibari wa asili mbali mbali kama walivyo hivi sasa walikuwa wakiishi kwa mapenzi makubwa bila ya chuki za ukabila na urangi, au kwa lugha nyengine, waliishi bila ya mimi ni nani na wewe na nani.

Muingereza alikuja kuwaundia wazanzibari vyama vya kikabila na urangi. Vyama hivyo yaani jumuiya za kikabila ni kamavile Arab association, Shirazi association, African association, Indian association na jumuiya nyengine.

Wazanzibari nao wakavishabikia vyama hivi vya kikabila na kila mmoja akawacha kupigania maslahi ya uzanzibari na akapigania maslahi ya kabila lake. Lakini hayo yalikuwa ni mafanikio makubwa kwa Muengereza, kwani ni sera yake muhimu ya ukoloni ya wagawe uwatawale (divide and rule).


Kuanzia harakati za kutafuta uhuru chama cha ASP na viongozi wake akiwemo kiongozi mkuu Karume waliukejeli na kuupiga vita ukweli kwamba wazanzibari ni watu wa asili na ustaarabu mseto na kujaribu kuyatenga makundi yote ya kizanzibari yalio na asili zake kutoka nje ya bara la Afrika kama vile waarabu, wahindi, magoa nk. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba hata washirazi wenye asili zao kutokeaIranambao ndio wanaofanya asilimia kubwa ya wazanzibari nao walipigwa vita.

Kama hilo halitoshi hata wakomoro wenye ngozi nyeupe lakini wenye asili zao kutokea katika bara la Afrika nao walikejeliwa na kukataliwa. Kwa viongozi wa ASP mzanzibari namba moja au mzanzibari asilia na mwenye hadhi kubwa ni lazima awe mwafrika mwenye ngozi nyeusi. ASP iliupigia kelele, kuunadi na kuutukuza uafrika pamoja na ngozi nyeusi na kuzidharau jamii zote za kizanzibari zilizobaki.

Kabla ya mapinduzi ASP na viongozi wake walijaribu kuwaheshimu washirazi wakifahamu bila ya wao na wingi wao ushindi kwa ASP ingelikuwa ndoto. Mara tu baada ya mapinduzi na ASP kushika hatamu chuki dhidi ya ushirazi na washirazi zikadhihirika.

Serikali ya Karume ilipambwa na viongozi wenye asili zao kutokea bara hususanTanganyika. Hii inajionyesha hata kwa majemedari wa mapinduzi na wajumbe wa baraza la mapinduzi la mwanzo lilikuwa na watu wengi zaidi wenye asili zao kutokea bara. Hii iliwafanya wafikirie kwamba serikali ya mapinduzi ni ya wazanzibari wa asili za bara na waliobaki ni watu wa daraja la pili. Baada ya mapinduzi Karume aliwataka watu wote wenye asili ya kikomoro kuomba uzanzibari (Burgess 2009:204). Kwa kuwa Karume mwenyewe alikuwa na asili yake kutokeaMalawialiwaogopasanawashirazi. Katika akili yake Karume aliwaona washirazi ni watu wanaoringa na kujidaikamawazanzibari halisi. Hivyo basi aliwalazimisha washirazi nao kubadilisha makabilayao.

Washirazi wengi walilikataa agizohilola Karume hususan wapemba. Wengi wa washiraziPembawalisema wao hawana kabila jengine mbadala mpaka Karume atakapowapatia baba wengine. Hivyo basi hali halisi ya ugozi na ukabila ilipamba moto zaidi baada ya mapinduzi kuliko kabla.

Wapigaji na wachezaji wa ngoma hiyo chafu ya ukabila baada ya mapinduzi walikuwa viongozi wa serikali ya mapinduzi na wajumbe wa baraza la mapinduzi la mwanzokamavile Karume mwenyewe, Seif Bakari na Abdalla Said Natepe, Mungu awarehemu.


Baada ya mapinduzi vitabu vyote vya historia vilivyofundisha ukweli kuhusuZanzibar, maisha ya masultani, na urithi wa ustaarabu mseto vilichomwa moto (Burgess 2009). Tukio moja la uchomaji huo lilifanyika eneo la Lumumba Unguja mbele ya macho ya maelfu ya watu. Badala yake mwenyekiti wa Youth league, Seif Bakari aliandika kitabu kipya kilichokua kikisomeshewa watoto mashuleni. Katika kitabu chake hicho, Seif Bakari anadai kuwa yote yaliopita kabla ya mapinduzi yalikuwa si chochote bali ni dhiki na dhuluma.

Katika kuzidi kuchonga chuki miongoni mwa wazanzibari weusi dhidi ya wenye ngozi nyeupe, Abdalla Said Natepe ambae ni mjumbe wa mwanzo wa baraza la mapinduzi na mjumbe wa kamati ya watu 14 alikuwa akifanya mikutano ya hadhara kuwaaambia watu hadithi za uzushi. Miongoni mwa hadiuthi hizo ni kuwa waarabu waliwalazimisha waafrika kupanda minazi kisha wakawa wanajifundishia shabaha kwa kuwatungua kwa risasi.

Hadithi nyingine ni kuwa waarabu waliwalazimisha wanawake wa kiafrika kufyagia barabara kwa maziwayaona waja wazito wa kiafrika walip[asuliwa ili bibi wa kiarabu ajue mtoto amekaaje tumboni. Mafundisho haya yamekuwa yakitolewa mashuleni kwa muda mrefu ili kutia sumu katika akili za watoto wakishirazi na kifrika dhidi ya waarabu.


Nyimbo za uafrika dhidi ya asili nyengine zote ziliendelea kuimbwa ndani serikali ya mapinduzi kupitia warithi wake wenye misimamo mikali ya uhafidhina wa ugozi na umapinduzi kwa lengo la kulinda malengo na uhalali wa mapinduzi hayo.

Kuthibitisha kasi na nguvu za uhafidhina huu na chuki dhidi ya watu wasiokuwa na asili ya kiafrika ndani ya Zanzibarni maneno ya Omar Ramadhani Mapuri, ambae yeye mwenyewe ana asili yake kutoka Tanzaniabara, aliyekuwa Waziri wa elimu na Naibu waziri kiongozi katika awamu ya nne ya Rais Salmin Amour. Kupitia kitabu chake, Zanzibar Revolution, Achievements and Prospects, kitabu ambacho kinazungumzia kiwango cha juu cha ukabila katika enzi za ustaarabu duniani, Mapuri ameweka wazi hisia zake kali dhidi ya watu wasiokua waafrika ndani yaZanzibar.

Lengo kuu la Mapuri katika kitabu chake ni kuwataka wazanzibari wenye asili za kiafrika kuungana dhidi ya kile anachokiita chokochoko na uchokozi wa nchi za magharibi na waarabu ambao chini kwa chini kwa mujibu wa Mapuri wanataka kurudisha tena ushawishi waoZanzibarkama ilivyokuwa kabla ya mapinduzi. Umoja huu ambao Mapuri anawaasa wazanzibari ndio ule ule uliotumika katika harakati za uhuru na mapinduizi ya 1964.


Katika kitabu chake pia Mapuri anakana kwa nguvu zote mauwaji yaliyofanywa na mapinduzi ya 1964 na kwa mujibu wa mawazo yake yale yanayoripotiwa kuwa ni upotezaji wa roho za watu kwa mgongo wa mapinduzi ya 1964 ni uongo mtupu na kusisitiza kwamba watu waliokufa kutokana na mapinduzi hayo ni wachache mno. Hata hivyo katika kitabu chake anadai kuwepo kwa nyaraka zinazobainisha azma ya serikali ya Shamte na Sultani iliyopinduliwa ya kutaka kuuwa raia wengi wa kiafrikakamani kulipiza kisasi kwa mauwaji ya waarabu waliouliwa kufuatia uchaguzi wa juni 1961 ijapokuwa hakubainisha katika kitabu chake nyaraka hizo zilipo.

Mapuri anadai nyaraka hizo zinathibitisha kwamba serikali ilipanga kuuwa waafrika sitini (60) kwa kila mwarabu mmoja aliyeuliwa Juni 1961. Mapuri pia anadai nyaraka hizo zinathitisha azma ya serikali ya Shamte na Sultani kuzitaifishamalizote za waafrika wasio na asili za kizanzibari. Hakumalizia hapo Mapuri pia ameandika kwamba Serikali ya Shamte ilikuwa na lengo la kuwafanya watumwa wazanzibari wote wenye asili ya kiafrika na hatimae Zanzibar kutangazwa kama ardhi ya waarabu.

Kikubwa zaidi ambacho pia Mapuri amewatanabahisha wazanzibari katika kitabu chake ni azma ya Serikali ya Shamte iliyopinduliwa kuwauwa watoto wote wa asili ya kiafrika na wanawake wenye asili ya kiafrika kulazimishwa kuolewa na waarabu kwa malengo ya kutokomeza ngozi nyeusiZanzibar.

Alichokifanya Mapuri bila shaka lilikuwa si jambo geni katika historia yaZanzibar. Ni marudio tu ya yale yalioanzia miaka ya 1960 ya mapambano ya makabila katika kugombania kumezwa, kufunikwa au kutokomezwa na makabila mengine.


Ni jambo la kushangaza mno kwa enzi ambayo vuguvugu la kihistoria la ukabila na uasili tayari limeshasahaulika, kiongozi wa ngazi za juu katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibaranapika upya migawanyiko ya wazanzibari kwa misingi ya rangi, ngozi na wanakotokea mababu zao.

Kiongozi kama huyu bila shaka ana dhima kubwa ya kuwaunganisha wazanzibari walio na asili na utamaduni wa kila namna karibu kutoka pembe zote za dunia lakini badala yake anashajihisha na kuhimiza umoja na muungano wa baadhi ya wazanzibari dhidi ya wenzao. Hata hivyo sio Mapuri peke yake katika viongozi wa leo wanaopiga kelele za ukabila na uasili ndani ya Zanzibarya kisasa.

Wapo wenzake Mapuri ambao wao wamefika mbali zaidi kwa kudai kwamba vijukuu na vinying'inya vya waarabu hawapaswi kupewa madaraka ya Zanzibarkwa kunasibika kwao na kabila la wapinga mapinduzi ya 1964. Katika kitabu chake, Kwaheri ukoloni kwaheri uhuru, Harith Ghassany analizungumzia hivi suala hili.


"Fikra ya uzalendo ya Pan-Africanism ambayo ilikuwa ikipigiwa kelele na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa na misingi kwamba kila asiye "Muafrika" ni mgeni (wakuja) Afrika na kwa maana hiyo pia ni mgeni Zanzibar hata kama alizaliwa na alikuwa na mizizi mirefu na mipana ndani ya Zanzibar.

Kinyume chake kila aliyekuwa ana asili ya Kiafrika (kibantu) na hata kama hakuzaliwa na wala hana mizizi mirefu ndani ya Zanzibar basi ana haki zaidi juu ya kuweza kutawala kwa sababu tu ni "Muafrika." Hapa sharti ifahamike kwanza kuwa neno "Afrika" linatokana na neno
Ifriqiya, ambayo wanahistoria wanathibitisha ilikuwa ni jimbo la Kaskazini ya Afrika katika nchi ambayo kwa sasa inajulikana kwa jina la Tunisia.

Ibn Khaldun, mwanafalsafa wa historia maarufu duniani na baba wa sayansi ya jamii (sociologist) aliyeishi miaka 676 nyuma, amemzungumza katika kitabu chake Mfalme wa zamani wa Yemen Afriqus Bin Qays Bin Sayfi. Kwa mujibu wa Ibn Khaldum Mfalme huyu aliishi wakati wa Nabii Musa au labda kidogo kabla yake. Ibn Khaldum anathibitisha kuwepo kwa mfalme huyo kutoka Yemen ambaye jina lake hilo inawezekana sana likawa moja wapo wa asili ya jina "Afrika".

Mawazo yaliyoenezwa kila upande ni kwamba Zanzibar ni ya Muafrika mweusi mwenye asili ya bara peke yake kuliko Muafrika mwingine yeyote hata kama amezalika huko Zanzibar kwa dahari nyingi. Mawazo haya yanatokana na fikra kuwa "Bara la Waafrika" ni Bara la watu weusi tu. Watu weusi hao tena ni wale wanaotokana na asili ya Kibantu na Wabantu hao bila shaka wawe hawana kabisa asili au uhusiano wowote na Waarabu.

Wenye mawazo haya bila shaka walisahau kuwa wanalitenga kundi kubwa la Waafrika wa Kaskazani katika nchi za Ethiopia, Somalia, Djibouti, Eritrea na Mauritius. Halkadhalika mawazo hayo yamewatenga wazungu wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Kenya. Pia mawazo hayo yamewatenga Mayahudi na Wahindi wazalendo wa Afrika, na makabila yote ya watu ambayo yana chimbuko lake katika bara hili
" (Gassany 2010).


Wazanzibari ni watu walio na asili zao nyingi na ustaarabu mchanganyiko ulizoanzia mbali. Asili za kiarabu, ki-pashia, kihindi, kitanganyika, kiganda, kikenya, kimsumbiji, kikomoro, kinyasa, kisumeri, kiassiri, kisomali, kiabisini, kifoniki, kidiba, kidebule, kireno, kibaluchi, kikurdi, kijojia, kichina, kisrilanka nk Wengi wao ni machotara, hakuna awezae kukaza mdomo akamtukana mbantu, akija akitanabahi kumbe kamtukana babu yake, au akakaza mdomo akamtukana mwarabu, akitanabahi kamtukana mama yake.

Uarabu, ubantu, uhindi, na asili nyengine zote za wazanzibari zilizopo kamwe hazibandukani na uzanzibari na bila ya kundi moja tu katika hayo ni sawa na mwanadamu asivyokamilika akikosa baadhi ya viungo vyake.


Tunaishukuru sana serikali ya ya Dr Shein ya Umoja wa kitaifa kwani imefanikiwa kufuta madoadoa ya kibaguzi baina ya wazanzibari wenyewe kwa wenyewe na kuusimika ule ustaarabu mseto (cosmopolitanism) unaomtambua kila mzanzibari kua ni mzanzibari bila ya kuangalia rangi yake, nywele zake pua yake.

Wazanzibari tusurudi nyuma haya ya kufunzwa kubaguana ndio yaliyotufikisha hapa na kuipoteza nchi yetu na hatimae kuingia mikononi mwa Tanganyika. Tuungane kwa umoja wetu turudishe heshma ya Zanzibar yetu yenye mamlaka kamili kama ilivyowahi kutamalaki hapo kabla ya 1964.


Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza
 
Ukisoma kwa makini kuna mahali imesemwa 'washirazi ambao ni wengi' ili kuanza kujenga hoja kuwa Washirazi ndio wengi ZNZ. Kuna element za kuonyesha kuwa ukatili haukufanywa na waarabu bali waafrika chini ya Karume.

Anachokusudia mwandishi ni kutaka kuwafanya wznz wajione hawana tofauti lakini anajisahau kwa kuanza kuwanyooshea mkono Waafrika.

Ukweli ni kuwa Wzn wengi wenye asili ya ZNZ ni wakazi wa Afrika hasa Tanganyika. Hawa wengine ni Wzn wenye asili zingine kama ilivyo kwa Tanganyika yenye watu wa asili nyingine lakini bado ni Watanzania.

Hii habari ya kupindisha ukweli kuwa Washirazi ni wengi ni dalili za kwanini hawa watu wanaita Watanganyika Makafir. Nje ya muungano MZNZ mwenye nywele za kipili pili ndiye atakuwa Kafir kwasababu asili yake ni kutoka ukafirin.

Lakini pia utaona jinsi gani wznz wanavyojitahidi kuhusisha matatizo yao na Nyerere. Wanasema dhana ya Nyerere ya Pana Africanism ilikuwa na lengo la kuwatenga watu wa mataifa mengine. Ujinga na upuuzi wa hali ya juu wa waandishi wa Zanzibar hasa wenye nywele za 'katani'.

Dhana ya Pan Africanism haikuwa ya Nyerere ingawa alikuwa mshiriki.

Ni lazima hawa wamanga wasome vitabu na waelimike, huyu Ghassany ndiye jamii ya A.Rajab na M. Said, ambao wanadhani wanaweza kuupotosha umma kwa hoja nyepesi za kipuuzi zilizojikita katika fikra za uarabu na tamaduni za kiarabu. Wanafanya hivyo kwa kutumia dini.

Kama Nyerere angekuwa anachukia watu wa mataifa mengine, asingeweza kuwa na Waziri Leader Sterling wa Uingereza, Amir Jamal (Mhindi), Alnoor Kassam (Mhindi), Mbunge D.Bryceson (mzungu), Genereal Wladen n.k.

Hata kwenye serikali ya muungano akina Hassan Diria, M. Abouud na wengine wasingeonekana basi!

Hakuna mtu wa taifa lingine aliyewahi kufukuzwa au kunyanyaswa hapa Tanzania. Kinyume chake Mwalimu alikemea sana ukabila na udini. Ushahidi ni jinsi tubavyoona upuuzi uliopo na nyakati zake.

Kwahiyo WZN washughulikie matatizo yao bila kutafuta mchawi, haya tunayoyaona ni mwanzo tu, nje ya muungano ni disaster. Washirazi wameshaanza kudai shea yao. Kama una nywele za kipili pili na ngozi yako si ya 'dhahab', huna madevu basi jiandae maana Washirazi wanaidai nchi yao.
 
Nafikiri sasa wadau mmwanza kuona nini kitafuata baada ya muungano kutoweka. Wataanza kubaguana kwa kwa misingi ya WASTAARABU na WABANTU n.k.
 
Mi naona si kweli. Sababu ni maamuzi ya chaguo la itikadi mliyoamua kuichukua ndiyo inawapa utumwa na mateso makubwa.

Mambo mengi walituletea wakoloni hivyo kama ulifuata rafiki mwenye akili ndogo na wewe utakuwa finyu kimawazo pia. Mzungu na Mwarabu walikuwa ndio wageni wetu hasa waliotuletea itikadi. Na waliofuata Mwarabu kazi kwao, mfano mzuri, Siria na nchi nyingine za Kiarabu jinsi ambavyo migogoro haishi na mwishowe NO MAENDELEO.

Kazi kwenu, muungano ukivunjika lazima mtaanza kubaguana Wapemba, Watumbatu, Waunguja n.k.
 
Zanzibar iligunduliwa na watu watatu, Msambaa anayeitwa Kombo, Mzigua anayeitwa Makame na Mwarabu anayeitwa Halfan. Walianzisha makazi na kuzaliana kabla ya wangazija na wengine kulowea huko.

Kinasaba, wazanzibar ni wasambaa, wazigua, wangazija, waarabu, wamakonde, wanyamwezi to name a few. Talk about Cosmopolitan society.

Simo.
 
Hhahahah, Munakasirika kweli mukiambiwa ukweli. Waacheni wazanzibari wanede zao. Nyinyi muna jiinchi kubwa kweli kweli, munashindana na kajisehemu kadogo. Watu hawafiki millioni moja wanawasumbuanini?. Vunjeni muungano.
 
nani jamaa anakuonewa donge na kwa lipi zaidi watu wa bara wanatafakari jinsi watakavyokumbatia mzigo sababu mwisho wa yote na maneno yenu mengi mtatuomba hifadhi.
 
ELIMU YA MADRASSA BALAA
1Kumbe kwako wakoloni ni waingereza sio seyyid said na said barghash?
2,mgawanyiko haukwepo kabla ya waingereza kuja?????!!!!! wakat warabu waliendesha biashara za utumwa? eg tipu tip
3,zanzibar watu weusi walikwepo kabla ya wajinga kama wewe waliokubali uislam na mbaya uarabu (jina lako)
4,je kama ni hivo kwanini karume alimpindua jamsheed kama hakuwa na udaraja na ukabila? tangu lini mwarabu akajiona sawa na kiumbe duni (mutu nyeusi) kama wewe?
5 soma elim dunia kaka hyo ya madrasa itakupeleka kusiko
 
Ahmed ahsante sana huo ndio ukweli anayepinga anajipa shida tu! ati tumechanganyikiwa ! kwa bahati nzur sisi hatukeshi vilabu kunywa pombe! watanganyika musione choyo andikeni na nyinyi hiyo historia yenu ,iliyobuniwa na huyo baba yenu wa taifa! tokeni na husda zenu !

Kwa Ukweli Wazanzibari sio WABANTU?
 
WAZANZIBARI NI JAMII YENYE ASILI NA USTAARABU MSETO (COSMOPOLITAN SOCIETY) NA SIO JAMII YA KIBANTU (KIAFRIKA)Na pia si jamii ya KIARABU!!
 
Subirini tuipige chini CCM yenu halafu mtaisoma namba vizuri! As far as I am concerned muungano ukifa leo itaniongezea sana miaka ya kuishi! Nyota ya maisha yangu inang'aa zaidi nje ya muungano kuliko inavyochafuliwa sasa na watu wasiobebeka, wasioridhika, mabingwa wa kunung'unika, wachokozi, wachochezi, wavivu, wabaguzi, waongo, wabinafsi......! Labda hiyo ndiyo sifa ya WASTAARABU!

Eti wazanzibari siyo wabantu; so what? Nani kakwambia merit ya kuwa mtanzania ni ubantu?

LET ZANZIBAR GO!
Zanzibaris are very abnormal! Hawautaki muungano yet wanawaunga mkono CCM ambao ndiyo kundi pekee nchini (ambalo after all sasa ni DOGO, linalindwa tu na dola) linaloukumbatia muungano wa namna hii!!!! Very strange indeed!

Nina ushauri mmoja tu kwa wazanzibari: Kama ni kweli walio wengi hawautaki tena muungano huu basi they have only one option: "Kuunga mkonno jitihada za dhati zilizopo sasa za kuipiga chini CCM. Wasiendelee kunung'unika huku wakiendelea kuiunga mkono CCM ambayo ndiyo kundi pekee linalokumbatia muungano uliochokwa sasa na pande zote mbili." Lest they give me more substatial ground to question their rationality!
 
Hii title pekee WAZANZIBARI NI JAMII YENYE ASILI NA USTAARABU MSETO (COSMOPOLITAN SOCIETY) NA SIO JAMII YA KIBANTU (KIAFRIKA inatia kichefuchefu!
Hii ina maana watu wenye asili ya Kibantu (Kiafrika) sio wastaarabu?
Nini maana ya Ustaarabu? Kwako wewe ni nani Mwafrika katika Afrika?
Huyu aliyeandika makala hii anapaswa akili yake ikoshwe kwa jiki.

Mtu mwenye mawazo kama haya, anajulikana kama "Snob," [
A snob believes that some people are inherently inferior to him or her for any one of a variety of reasons, including real or supposed intellect, wealth, education, ancestry, class, taste, beauty, nationality, et cetera.] Asili ya neno hili Kilatini lina maana ya kutotokana na watu wasio na daraja ("sine nobilitate" or "sans noblesse" meaning "without nobility"), lakini ili waonekane wanatokana na daraja ya juu, huwa na tabia ya kujidai kutokana na daraja hilo, kama kinga ya kutojiamini kwao miongoni mwa wenye daraja. Huyu atakuwa ni huyu "mjomba wangu" aliyeandika makala hii.
 
napita tu .. hapa, mi hawa ni ndugu zangu katika iman "waislam" lakini i was disappointed kule mzalendo nakuta comments wanasema waislam wa tanganyika hawajui dini .. sina chuki na wa znz.. ila muache dharau basi at list kwa ndugu zenu katika iman "waislam wenzenu"

kwenye facebook page ya zanzabar - nakuta comments kwenye picha ya mfanya biashara tiputipu yule mshenzi aliyefanya biashara ya kuuza bin adamu wenzake wao wana comments kumsifia na kumuombea dua alale mahala pema peponi na kumfanya as if he was a hero & successful business man na wakazidi kusema hakuwafanya watumwa wazanzibaar bali aliwatoa tanganyika watumwa .. mlikuwa wengi kwenye page yenu mkanizidi kwenye arguments ila ukweli my brothers & sisters katika iman "mtume alipiga vita biashara ya utumwa kipindi uislam unaenea" huyu mnayemuona ni successful business man na kufanya biashara ya utumwa hata mkimuombea dua his place ni HELL ...

ni hayo tu!
 
Ukisoma kwa makini kuna mahali imesemwa 'washirazi ambao ni wengi' ili kuanza kujenga hoja kuwa Washirazi ndio wengi ZNZ. Kuna element za kuonyesha kuwa ukatili haukufanywa na waarabu bali waafrika chini ya Karume.
Anachokusudia mwandishi ni kutaka kuwafanya wznz wajione hawana tofauti lakini anajisahau kwa kuanza kuwanyooshea mkono Waafrika.

Ukweli ni kuwa Wzn wengi wenye asili ya ZNZ ni wakazi wa Afrika hasa Tanganyika. Hawa wengine ni Wzn wenye asili zingine kama ilivyo kwa Tanganyika yenye watu wa asili nyingine lakini bado ni Watanzania.
Hii habari ya kupindisha ukweli kuwa Washirazi ni wengi ni dalili za kwanini hawa watu wanaita Watanganyika Makafir.
Nje ya muungano MZNZ mwenye nywele za kipili pili ndiye atakuwa Kafir kwasababu asili yake ni kutoka ukafirin.

Lakini pia utaona jinsi gani wznz wanavyojitahidi kuhusisha matatizo yao na Nyerere. Wanasema dhana ya Nyerere ya Pana Africanism ilikuwa na lengo la kuwatenga watu wa mataifa mengine. Ujinga na upuuzi wa hali ya juu wa waandishi wa Zanzibar hasa wenye nywele za 'katani'.

Dhana ya Pan Africanism haikuwa ya Nyerere ingawa alikuwa mshiriki.
Ni lazima hawa wamanga wasome vitabu na waelimike, huyu Ghassany ndiye jamii ya A.Rajab na M. Said, ambao wanadhani wanaweza kuupotosha umma kwa hoja nyepesi za kipuuzi zilizojikita katika fikra za uarabu na tamaduni za kiarabu. Wanafanya hivyo kwa kutumia dini.

Kama Nyerere angekuwa anachukia watu wa mataifa mengine, asingeweza kuwa na Waziri Leader Sterling wa Uingereza, Amir Jamal (Mhindi), Alnoor Kassam (Mhindi), Mbunge D.Bryceson (mzungu), Genereal Wladen n.k.
Hata kwenye serikali ya muungano akina Hassan Diria, M. Abouud na wengine wasingeonekana basi!

Hakuna mtu wa taifa lingine aliyewahi kufukuzwa au kunyanyaswa hapa Tanzania. Kinyume chake Mwalimu alikemea sana ukabila na udini. Ushahidi ni jinsi tubavyoona upuuzi uliopo na nyakati zake.

Kwahiyo WZN washughulikie matatizo yao bila kutafuta mchawi, haya tunayoyaona ni mwanzo tu, nje ya muungano ni disaster. Washirazi wameshaanza kudai shea yao. Kama una nywele za kipili pili na ngozi yako si ya 'dhahab', huna madevu basi jiandae maana Washirazi wanaidai nchi yao.

Au asinge mtorosha SALIM AHMED SALIM kumpeleka Nje ya NCHI - Ubalozini EGYPT akiwa kijana kumuokoa
 
Tunaishukuru sana serikali ya ya Dr Shein ya Umoja wa kitaifa kwani imefanikiwa kufuta madoadoa ya kibaguzi baina ya wazanzibari wenyewe kwa wenyewe na kuusimika ule ustaarabu mseto (cosmopolitanism) unaomtambua kila mzanzibari kua ni mzanzibari bila ya kuangalia rangi yake, nywele zake pua yake. Wazanzibari tusurudi nyuma haya ya kufunzwa kubaguana ndio yaliyotufikisha hapa na kuipoteza nchi yetu na hatimae kuingia mikononi mwa Tanganyika. Tuungane kwa umoja wetu turudishe heshma ya Zanzibar yetu yenye mamlaka kamili kama ilivyowahi kutamalaki hapo kabla ya 1964.

Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza
Tukiendelea kuichambua taarifa hii tunaona kuna mambo mengi sana yameandikwa na kwa bahati mbaya hayakukusudiwa. Kwa mfano hapo mwisho anasema 'tuungane kwa umoja wetu turudishe hesma ya Zanzibar yetu yenye mamlaka kama ilivyowahi kutamalaki hapo kabla ya 1964'

Kabla ya 1964 aliyekuwa anatawala ni Sultan. Kulikuwa na majaribio kadhaa ya kupinga utawala wake kwa maneno na kwa vitendo. Mzanzibar mweusi mwenye asili ya umatumbi alikuwa kijakazi wa mwarabu. Ni chuki hiyo ndiyo iliyopelekea akina Thabiti Kombo, Jumbe, Mwinyi, Moyo, Natepe,Karume kuingia mitaani na mapanga ili kumuondoa Sultan.

Ili kudhihiri jinsi chuki ilivyokuwa imetamalaki waarabu waliozwa kwa lazima na hakuna ubishi kuwa jamii ya kimanga haitaki kusikia jina Karume. Hii maana yake ni kuwa akina Karume walikuwa wanalipa kisasi cha maonevu ya wageni miaka dahari.
Sasa mwandishi anaposema Zanzibar yenye neema ya kabla ya 1964, hapa anayakana mapinduzi na waasisi wake lakini pia anatupa picha kuwa yeye ni pro-Sultan na sina shaka nywele zake ni za katani zile bora kuliko kipili pili.

Anasema serikali ya Dr Shen imefanikiwa kufuta madoa ya ubaguzi. Si kweli ni kujifariji. Chuki ya Wznz ni ya kihistoria na haiwezi kufutwa kwa miaka 2 na mtu mmoja. Labda kwa vile Shen anatoka Pemba na ana unasaba na nywele za katani basi hapo ndipo anaposemwa amefanikiwa. Endapo ni mafanikio ya umoja wa kitaifa basi sifa ziende kwa Karume aliyemkubali Seif wakakaa pamoja. Lakini Karume mdogo hawezi kupewa sifa kwani kufanya hivyo ni kumtukuza Karume Baba, na Karume mdogo ana asili ya Bara hilo tu ni doa.

Anasema kubaguana ndiko kumefaifanya ZNZ iangukie mikononi mwa Tanganyika. Hapa ni ushahidi kuwa mwandishi huu ni mnafiki na kama si mnafiki hajui anaandika nini. Nashangaa Mzalendo wameweka makala ya mtu huyu mwenye chembe za ujuha. Hajui historia kwasababu mwaka 1957 Zanzibar ilikuwa tayari imegawanyika ndiyo maana kulikuwa na ZPPP, ZPP,UMMA, Afro shirazi. Kazi uya kuwaunganisha hawa kwa hakika ilifanywa na viomgozi wengi dunia lakini Nyerere ni sehemu muhimu sana. Kwahiyo hata kabla ya uhuru wa Tanganyika 1961, uhuru wa ZNZ 1963 na Mapinduzi ya ZNZ 1964, ZNZ ilikuwa imegawanyika katika urangi, pua, madevu na hijabu.

Ushahidi wa hili pia unaonekana kwani miaka 2 iliyopita Wapemba waliamua kwenda UN kutaka jamhuri yao. Hawa ni wale wanaoamini kuwa wanafanyiwa dhulma na Waunguja kwasababu tu walizaliwa na baba wa Kiarabu iwe kwa kukusudia au kwa bahati mbaya.

Ushahidi mwingine ni ule wa maalim Seif kuambiwa kuwa nchi ya znz ilipatikana kwa damu na hawezi kupewa kwa kipande cha karatasi cha kura. Mgogoro wote ulilenga kusema kuwa Usultan hakuna tena ZNZ.
 
Back
Top Bottom