Wazanzibar Waichachafya Kamati ya Bunge

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
HATUTAKI TENA KUBURUZWA: WASEMA WAZANZIBAR

Katika ukumbi wa salama Hall, hoteli ya Bwawani mjini zanzibar, kamati ya bunge ya katiba na sheria inayoratibu maoni juu ya mswada wa sheria ya kuandaa utaratibu wa kupata maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya, imechachafywa vikali na wazanzibar wakiwamo wawakilishi, wanasiasa, wanazuoni , wanasheria na wadau mbali mbali visiwani humo.

Hali ilikuwa mbaya kwa tume hiyo iliyoitisha mkutano huo kwa taarifa za haraka haraka, baada ya Mh. Samuel Sitta, kutoa mawasilisho ya mswada huo. Mchangiaaji wa kwanza alikuwa Mh. Hamza Hassan Juma, mwakilishi wa jimbo la Kwamtipura ambaye aliitaka tume hiyo irudi na mswada huo kwa vile Zanzibar haikushirikishwa chochote katika kuuandaa hadi ulivyo sasa.

Huku ukumbi wote ukiwa na hamasa hasa pale aliposimama mwanasheria mkuu wa serikali ya Mapinduzi ya zanzibar bw. Othman Masoud Othman, aliposema kuwa mbali na mswada huo, bunge la Muungano halina Mandate ya kupitisha mswada huo kwa kuwa mamlaka yake kwa mujibu wa katiba ni kurekebisha tu.

Aliongeza kuwa katiba inayotaka kufanyiwa mabadiliko ni katiba ya muungano, ambao upo kwa mujibu wa terms za mkataba wa muungano, hivyo, alishauri kuwa ni lazima pande mbili za muungano zirudi katika mkataba wa muungano na siyo kuja na mswada kama huo.

Wachangiaji waliimbia tume hiyo kuwa kinachotaka kufanyika saivi ni kiini macho chengine kwa wazanzibar kama ilivyozoweleka huko nyuma.
" Mh. mwenyekiti mimi nitaupinga mswada huu katika baraza la Mapinduzi, baraza la wawakilishi na pahala pengine popote nitakapopata nafasi, kwa vile mswada huu hauna maslahi na Zanzibar..." alisema Mh. Mansour Yussuf Himid, waziri wa kilimo na mali asili wa SMZ.

Nao wanasheria wa zanzibar wamesema hawawezi kamwe kukubali mswada huo ujadiliwe huku mambo ya msingi yanayowahusu wazanzibar yakiwekewa vikwazo vya kuyazungumza.

"ndugu mwenyekiti, sisi wazanzibar linalotuhusu katika mkataba huu ni muungano, tuna haki ya kujadili uwepo wake na kutokuwepo kwake, hata namna ya kuwapo kwake ni vipi hili liwekewe vikwazo kulijadili?" alihoji mwanasheria wa kujitegemea Ndg. Awadh Ali Said wakati akichangia mswada huo.



inaendelea kwa kuwa tupo katika break hadi saa nane mchana:
 
Hata sisi watanganyika tuna haki ya kusema tunauhitaji muungano au la. Mimi muungano wa hivi siuhitaji kabisa; huu wa nchi ya Tanganyika kumezwa na Zanzibar ikabaki!; huu wa watu milioni 5 kuwa na haki sawa na watu milioni 45!; huu ambao hawa watu milioni 5 kila wanachoomba wanapewa wakati hawa miloni 45 wananyimwa kwa kisingizio cha kutovunja muungano! nk
Mimi nahitaji moja kati ya mawili; Muungano wa kuwa na serikali tatu, au wa kuwa na serikali moja- period
 
Tupinge hii kitu kwa nguvu zetu zote pia tukae macho na malipo ya dowans yanaweza kuwa processed wakati huu
 
Ccm wanafurahi kwani hili ni changa la macho ,kadri inavyokataliwa ndivyo 2015 inakaribia. Lakini karagwe hatupigi kura tena kwa katiba hii hilo mjue
 
:A S 2152:

Hahaaaa...Wazanzi wa bari bwana wanatia raha sana....safi kabisa na nawaonea huruma kwa kumvua nguo baba yenu wa CCM

Inafurahisha kuwa mmechoka kuburuzwa, atleast hili linatia moyo kuelekea hatua ya kutimua zenu kwenye Muungano
 
Katika mkutano huo serikali ya mapinduzi imewaleta mawaziri wake wote muhimu ambao walisimama na kukisema kipengele kimoja baada ya kimoja. Naye Mwanasheria Mkuu wa zanzibar amesimama tena na kupinga madai ya kamati hiyo, baada ya majumuisho ya Mh. Sitta kueleza na kutoa ushahidi kuwa SMZ imeshirikishwa katika kuandaa rasimu ya mchakato wa maoni ya katiba.

Waziri wa sheria wa SMZ na mwanasheria Mkuu wa SMZ walijibu kuwa huo utaratibu unaodaiwa kutumika kuishirikisha SMZ haukuwa sahihi hivyo bado wanashikilia kuwa mswada huo ni batili tokea awali (void ab initio).
Kamati hiyo imemaliza mkutano wake huo punde tu hivi katika ukumbi wa bwawani hotel na kesho inatarajiwa kuendelea na mkutano mwengine katika ukumbi wa skuli ya Haile selassie, mjini zanzibar.
 
Back
Top Bottom