Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,502
- 9,282
Kwa mujibu wa kifungu cha 20(2) cha mswada mpiga kura aliyejiandikisha kupiga kura kwa madhumuni ya mswada huu, endapo kadi yake ya kupigi kura itapotea, kufutika au kuharibika atalazimika kufanya maombi ya kuomba kitambulisho kipya kwa afisa mwandikishaji wa eneo husika.
Afisa mwandikishaji baada ya kujiridhisha kuwa maombi tajwa yamekidhi vigezo atampatia mpiga kura huyo kadi mpya baada ya kuwa amelipia ada itakayokuwa imeanishwa na Tume.
Kupiga kura ni haki ya kikatiba iliyoanishwa kwa mujibu wa ibara ya 5 na 21 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, sanjali na mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania ni nchi mwanachama, ni haki inayoamua hatima maisha ya Watanzania kwa miaka mitano. Hivyo ni haki isiyopaswa kuingiliwa kwa namna yoyote ile na mamlaka za Serikali ikiwemo kuipata kwa njia ya malipo.