Wanzibar Ni Wazalendo Kuliko Watanganyika.

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
4,485
11,036
Utaifa ni jambo ambalo mataifa yote duniani huulinda kwa nguvu zote,hakuna taifa lenye watu wenye akili timamu wako tayali kuona utaifa wao unachezewa hovyo,hili tuna liona kwa mifano michache kupitia mataifa kadhaa mfano ni mgogoro wa Israel na Palestine.

Ni mvutano wa uwepo na utetezi wa utaifa kwa pande zote mbili,nguvu ya mapambano imesukumwa na uzalendo halisi juu ya kufia utaifa wao kwa manufaa ya kizazi Cha sasa na kijacho.

Baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo 1964 na kuundwa kwa taifa la Tanzania.Watanganyika walipoteza utaifa wao na taifa lao la Tanganyika na kujivika utaifa mpya kwenye taifa jipya la Tanzania.

Kwa upande wa pili Wazanzibar wakisukumwa na uzalendo halisi na ulio thabiti juu ya taifa lao na utaifa wao,waligoma kupoteza taifa lao na utaifa wao kama Wazanzibar kama walivyo fanya Watanganyika kwa kujivika koti la muungano.

Leo hii Zanzibar wana serikali Yao kwa mujibu wa katiba yao nje na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977.Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ipo kwa ajili ya kutetea na kulinda maslahi ya Zanzibar na Wanzibar.Lakini hakuna serikali wala katiba ya kulinda maslahi ya Tanganyika na Watanganyika.

Wazanzibar wameweka mipaka na ukomo kwa wasio Wazanzibar kujadili mambo yanayo husu Zanzibar ndio maana Wana Bunge lao na bajeti yoa,hili pia lipo katika fursa mbalimbali mwiko kabisa kwa mtu asiye Mzanzibar kufaidika na fursa ambazo zipo kwa ajili ya Wazanzibar mfano ajira,kumiliki ardhi nk ,hali ni tofauti kwa Tanganyika ambapo hakuna sehemu ya kulinda maslahi ya Watanganyika Wala ukomo kwa wasio Watanganyika kujadili mambo ya Tanganyika ndio maana hatuna Bunge la Tanganyika Wala bajeti ya Tanganyika kama ilivyo kwa Zanzibar.

Wazanzibar wanalinda rasilimali muhimu kwa ajili yao wenyewe mfano,mafuta,gesi,bandari
nk,kwa kuyafanya sio mambo ya muungano lakini Watanganyika rasilimali zetu tumezifanya kuwa kama karanga kwa Wazanzibar kupata gawio la pesa na ajira uku kukiwa hakuna gawio maalumu kwa Tanganyika.

Katika nafasi za kisiasa mwiko kwa wasio Wazanzibar Kushika nafasi za ngazi mbalimbali za kisiasa ndani ya visiwa,lakini ni fursa kwa Wazanzibar Kushika nafasi za kiserikali ndani ya jamhuri kwa mgongo wa muungano uku Watanganyika hawana fursa hiyo kupitia Tanganyika yao bali muungano.

Ni kheri umaskini wa pesa sio umasikini wa akili na fikra.Watanganyika tumekosa vyote pesa hakuna na akili hatuna.Tumepoteza taifa letu na utaifa wetu uku watu wachache wakiona umuhimu wa kulinda taifa lao na utaifa wao.

Hongera kwa Wazanzibar kwa kuwa Wazalendo kwa taifa lenu na kulinda kilicho chenu kwa maslahi ya taifa lenu na utaifa wenu.

RIP mchungaji Christopher Mtikila
G-55.
 
Hata huku tuna uzalendo lkn viongozi wetu ndiyo hujivika mamlaka ya kuwadidimiza wapigania taifa la Tanganyika.

Mfano mzuri wa hivi karibuni ni Mwabukusi. Kilichompata unakijua.

Nyuma kidogo kulikuwa na Christopher Mtiklia uliyemtaja kwenye uzi wako. Mpk anakufa alikuwa anaitaja Tanganyika.

Lkn pia kuliwahi kutokea kundi la wabunge 55 maarifu kama G55. Hili liliibuka na ajenda bungeni likitaka hadhi na mamlaka ya Tanganyika. Walibagazwa mpk wakakaa kimya.
 
Kipindi Wazanzibar wakisimamia maslahi ya Zanzibar huwa kitu kimoja,hili tunaliona hata kwa Rais Samia jinsi kwao kulivyo na miradi isiyo akisi mapato ya Kodi zao.

Mtanganyika Mbowe alipotoa mawazo yake kuhusu bandari kwanini ziwe za Upande mmoja wakati ni suala la muungano uliona jinsi Wazanzibar walivyo kuja juu kumtetea na kusimamia msimo wao ambao ni kinyume na katiba na Mbowe kushambuliwa na Watanganyika bila kumuunga mkono kuhusu Mali za Tanganyika.

Mchungaji Christopher Mtikila na kundi la G 55 hoja zao zilikuwa za msingi lakini zilikuwa zipigwa vita na Watanganyika wenyewe.Hapa ndo tofauti zipo Kati ya Wazanzibar na Watanganyika.
 
Watu wanasema Nyerere alikuwa mtu mwenye akili nyingi. huwa nacheka sana
Unaweza kuwa na akili lakini huwezi kuwa mjuzi wa kila kitu ndio maana Kuna mambo alifeli.Mzee Karume alionekana kama mjinga kumbe alikuwa na akili.Mwisho tumekuja kuona nani alichanga karata zake vizuri.
 
Kwenye hili la kutolinda maslahi ya tanganyika nyerere alizingua sana,na zaidi katiba mbovu.
Maslahi ya Tanganyika yalipewa kisogo,kwa sababu za kisiasa.fursa zote na Mali zote ziliwekwa chini ya kivuli cha muungano cha ajabu upande ule Mali zao na fursa ni zao wenyewe.

Leo hii tunatawaliwa kijinga kwa sababu ya kulinda maslahi ya vikundi vya watu na kuweka uzalendo nyuma kwa maslahi ya tumbo.
 
Kipindi Wazanzibar wakisimamia maslahi ya Zanzibar huwa kitu kimoja,hili tunaliona hata kwa Rais Samia jinsi kwao kulivyo na miradi isiyo akisi mapato ya Kodi zao.

Mtanganyika Mbowe alipotoa mawazo yake kuhusu bandari kwanini ziwe za Upande mmoja wakati ni suala la muungano uliona jinsi Wazanzibar walivyo kuja juu kumtetea na kusimamia msimo wao ambao ni kinyume na katiba na Mbowe kushambuliwa na Watanganyika bila kumuunga mkono kuhusu Mali za Tanganyika.

Mchungaji Christopher Mtikila na kundi la G 55 hoja zao zilikuwa za msingi lakini zilikuwa zipigwa vita na Watanganyika wenyewe.Hapa ndo tofauti zipo Kati ya Wazanzibar na Watanganyika.

Dah kuna point umeweka hapa. Aisee watanganyika they are so divided.

Na hii division ilitengenezwa makusudi na chama fulani ili wawez kutawala watanganyika kirahisi

Watanganyika watachagua wenyewe kuendelea kulala fofo au kuamka usingizini na kuuona ukweli
 
Sidhani kama Watanganyika wengi wanajali kuhusu Tanganyika wala kujivunia nayo.

Kuna propaganda chafu mzee Nyerere aliweka kwamba kudai Tanganyika ni kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe hili lilikuwa kosa kubwa sana.
 
Divide and rule ni mbinu iliyo tumiwa hata na wakoloni kuwa tawala waafrika kirahisi kabisa na bado mbinu zilezile zinatumiwa na wakoloni weusi,ambao kwao madaraka ndo kila kitu kufifisha harakati za kudai Tanganyika.

Ni ajabu sana tumeshindwa kung'amua jinsi tunavyo chezewa akili na kundi la wachache kwa maslahi yao kwa hoja za tunu na kulinda legacy.

Hopeless kabisa.
 
Sidhani kama Watanganyika wengi wanajali kuhusu Tanganyika wala kujivunia nayo.

Kuna propaganda chafu mzee Nyerere aliweka kwamba kudai Tanganyika ni kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe hili lilikuwa kosa kubwa sana.
Watanganyika wamejipa jukumu la kuwa Mama wa muungano hivyo kujipa uwajibikaji kwa kila kitu na Wazanzibar wametumia tundu hili kufaidika na vilivyopo Tanganyika na kukumbatia vya kwao kuwa vyao.

Ndio maana hatuoni umuhimu wa kudai Tanganyika na maslahi yake.Mwl.Nyerere nae anamakosa katika hili,lakini zama zimebadilika.
 
Utaifa ni jambo ambalo mataifa yote duniani huulinda kwa nguvu zote,hakuna taifa lenye watu wenye akili timamu wako tayali kuona utaifa wao unachezewa hovyo,hili tuna liona kwa mifano michache kupitia mataifa kadhaa mfano ni mgogoro wa Israel na Palestine.

Ni mvutano wa uwepo na utetezi wa utaifa kwa pande zote mbili,nguvu ya mapambano imesukumwa na uzalendo halisi juu ya kufia utaifa wao kwa manufaa ya kizazi Cha sasa na kijacho.

Baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo 1964 na kuundwa kwa taifa la Tanzania.Watanganyika walipoteza utaifa wao na taifa lao la Tanganyika na kujivika utaifa mpya kwenye taifa jipya la Tanzania.

Kwa upande wa pili Wazanzibar wakisukumwa na uzalendo halisi na ulio thabiti juu ya taifa lao na utaifa wao,waligoma kupoteza taifa lao na utaifa wao kama Wazanzibar kama walivyo fanya Watanganyika kwa kujivika koti la muungano.

Leo hii Zanzibar wana serikali Yao kwa mujibu wa katiba yao nje na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977.Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ipo kwa ajili ya kutetea na kulinda maslahi ya Zanzibar na Wanzibar.Lakini hakuna serikali wala katiba ya kulinda maslahi ya Tanganyika na Watanganyika.

Wazanzibar wameweka mipaka na ukomo kwa wasio Wazanzibar kujadili mambo yanayo husu Zanzibar ndio maana Wana Bunge lao na bajeti yoa,hili pia lipo katika fursa mbalimbali mwiko kabisa kwa mtu asiye Mzanzibar kufaidika na fursa ambazo zipo kwa ajili ya Wazanzibar mfano ajira,kumiliki ardhi nk ,hali ni tofauti kwa Tanganyika ambapo hakuna sehemu ya kulinda maslahi ya Watanganyika Wala ukomo kwa wasio Watanganyika kujadili mambo ya Tanganyika ndio maana hatuna Bunge la Tanganyika Wala bajeti ya Tanganyika kama ilivyo kwa Zanzibar.

Wazanzibar wanalinda rasilimali muhimu kwa ajili yao wenyewe mfano,mafuta,gesi,bandari
nk,kwa kuyafanya sio mambo ya muungano lakini Watanganyika rasilimali zetu tumezifanya kuwa kama karanga kwa Wazanzibar kupata gawio la pesa na ajira uku kukiwa hakuna gawio maalumu kwa Tanganyika.

Katika nafasi za kisiasa mwiko kwa wasio Wazanzibar Kushika nafasi za ngazi mbalimbali za kisiasa ndani ya visiwa,lakini ni fursa kwa Wazanzibar Kushika nafasi za kiserikali ndani ya jamhuri kwa mgongo wa muungano uku Watanganyika hawana fursa hiyo kupitia Tanganyika yao bali muungano.

Ni kheri umaskini wa pesa sio umasikini wa akili na fikra.Watanganyika tumekosa vyote pesa hakuna na akili hatuna.Tumepoteza taifa letu na utaifa wetu uku watu wachache wakiona umuhimu wa kulinda taifa lao na utaifa wao.

Hongera kwa Wazanzibar kwa kuwa Wazalendo kwa taifa lenu na kulinda kilicho chenu kwa maslahi ya taifa lenu na utaifa wenu.

RIP mchungaji Christopher Mtikila
G-55.
Huu muungano unatunyonya sana Watanganyika.
 
Back
Top Bottom