Wazanzibar acheni unafiki na ndumilakuwili

Wile,
Inakubidi usome au ufanye utafiti lau kidogo ili uwe katika hali ya kufanya
mjadala.

Nimekupa mfano wa Wajerumani ili uwe mwerevu na kuelwa mchezo wa
siasa unavyochezwa.

Huwezi kuwatia Wazanzibari katika vikosi vinavyokwenda Zanzibar.
Utasababisha matatizo makubwa kwani damu ni nzito kuliko maji.

Fanya utafiti kwa kipindi cha chaguzi toka 1995 hadi 2015.

Ndiyo maana katika mapinduzi jeshi la kupigana Zanzibar lilitoka
Kipumbwi Tanga na wengi wao walikuwa Wamakonde kutoka mashamba
ya mkonge ya Sakura na Kipumbwi.

Soma kitabu cha Harith Ghassany: Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.
mi nimependa hilo jina la kitabu , nitakitafuta
 
Hii Makala ya Mohamed Said nayo ni RUBBISH pia!!!

Hivyo mtu na akili yake timamu haijui dhulma masultani waliyokuwa wakiitenda kwa Wazanzibari? Huyo mtu atakuwa ni muenda wazimu au kichaa au hakuishi enzi hizo hapa Zanzibar!
Kwani dhulma ni kutiwa ndani tu? Kufanywa nyinyi kuwa ni kaumu ya kuwa watumishi wa ndani tu (maboi), au nyinyi kuwa kaumu ya kumaliza masomo darasa la 4 tu, au nyinyi kuwa kaumu ya wakwezi tu, etc hivyo hizi sio dhulma Shk Mohamed Said?
Ukoloni umeondoka but some of us are still living under the delirium of colonization!
 
Mkoa maada una nzito sana. Wenzetu hawana msimamo kamili hupima upepo unaenda wapi.

Kwenye mafuta ni masuala yao. Rais wa JMT hana madaraka. Kwenye vurugu zao za uchaguzi wanakumbuka madaraka ya Rais wa JMT.

Inabidi wachague moja. Haiwezi kuwa sawa kwa hili ikawa hapana kwa lile wakati Rais wa JMT ni huyo huyo.

Sasa unapinga maneno yake mwenyewe Magufuli ya leo ya kuwa hana madaraka kwa mambo tele ya Zanzibar, lakini madaraka yake ni kuzuwia vurugu tu?
 
Mkuu Msemaji wa Ukweli napenda nikupe hongera kwa hii `analysis`yako nzuri kuhusu Zanzibar! Inavyonesha ya kwamba kumbe Wazanzibari tayari wamevunja muungano wetu na wala hatuna sifa tena ya kuitwa JMT! Mimi nakubaliana nawe kabisa na unaonaje tukaanza kuwahukumu Wazanzibari kwa kuwaondoa wale majeshi yetu kule zenji, Uhamiaji, TRA, polisi na mambo yote yanayohusu Muungano kule Zanzibar! Hata vyama vya siasa tukagawana na kuwa CCM Zanzibar na CCM Tanganyika! Tufanye uchaguzi mwengine pia wa Tanganyika tumhalilishe Magufuli awe ni Rais wa Watanganyika! Tuwaachie wazanzibari wajiamulie mambo yao wenyewe bila ya kuwaingilia. Hayo si mawazo yangu bali ni mwendelezo wa hicho ulichokiandika hapo juu!

Mkuu asante sana, umemaliza kila kitu.
 
Mkoa maada una nzito sana. Wenzetu hawana msimamo kamili hupima upepo unaenda wapi.

Kwenye mafuta ni masuala yao. Rais wa JMT hana madaraka. Kwenye vurugu zao za uchaguzi wanakumbuka madaraka ya Rais wa JMT.

Inabidi wachague moja. Haiwezi kuwa sawa kwa hili ikawa hapana kwa lile wakati Rais wa JMT ni huyo huyo.
Kwenye upigaji kura vifaru na askari wa Tanganyika wanafanya nini Zbar-acheni unafki wa kujitoa akili.
 
Kwenye upigaji kura vifaru na askari wa Tanganyika wanafanya nini Zbar-acheni unafki wa kujitoa akili.
Ndugu bado sana hujakuwa kiakili ni askari gani wa tanganyika wamekuja huko mm navyofahamu askari wa tanganyika ambao wanzanzibari hawapo ni magereza pekee je niambie magereza huko wapo na kama polisi basi ni mchanganyiko ya wazanzibar na watanganyika vile vile jeshi ni wazanzibar na watanganyika hakuna jeshi la watanganyika pekee huko acha kauli ya kinafiki na istoshe kama hujui kitu jaribu kuuliza hata kama kuuliza huwez jaribu kutofautisha kati ya kifaru na hivyo vinavyopita huko nakujuza tu uliza kwamba hvyo ni vifaru sina utaalamu na mambo ya kijeshi lakin nilijaribu kuuliza nikaambiwa si vifari ni APC kama hujui basi hvyo ndo vinavyoitwa kwahyo acha mawazo mgando jaribu kupambanua kitu kabla ya kukurupuka na kupost vitu usivyovijua
 
HIVI Dhumuni La Kuweka Huu UZI Hapa!!!? KWANI Mleta UZI Haujui Kuwa Ni KWELI VIONGOZI Kutoka BARA Ndio Chanzo Cha Mitifuano Kule Visiwani!!!!?? WW Kwa Fikra Zako CCM ZANZIBAR Wanaweza Kuamua Au Kufanya Maamuzi Yoyote Bila Ya CCM Bara Na Taifa Kuridhia!!?? JUU Ya KATIBA Yao Kuifanyia Marekebisho Hiyo Ni Haki Yao Kikatiba, Kwani Zanzibar Ni Nchi, Na Hawakukubali Kuufuta Uzanzibar Na Utaifa Wao!! Hivyo Kufanya Marekebisho Yao Ya Kuunda Serikali Ya Umoja Wa Kitaifa, Si Lazima Ww Wa BARA KUTOA MAONI YAKO!! Wazanzibar Wenyewe NDIO WALIOTAKIWA Kutoa MAONI Yao, Kama WANAKUBALI Au WANAKATAA!! PIA Suala La TUME Huru Ya UCHAGUZI, Ni Suala Zuri La Kulipongeza, Kwani Kwa Muundo Wa Tume Hiyo Ndio Ule Mchezo Mchafu Uliyokuwa Ukidaiwa Kufanyika Na Upande Fulani Umeshindwa Kufanyika 2015!! MATOKEO Yake Wamemtumia Jecha Kufuta MATOKEO Yaliokamilika!!! HIVYO Hilo Kwao Ni Suala Muhimu Na La Kupongezwa!! HUKU BARA Mbona Tumeshindwa Kupata, TUME Walau Hiyo Unayoiponda!!!! SIDHANI Kama Ni UNAFIKI Na UNDUMILAKUWILI!! Bali Ni Moja Ya Hatua Nzuri Ya Kujenga Umoja Wao!! TATIZO Ni WABARA, Ndio Wanaoivuruga Zanzibar, Na Wenyewe Wameshalijua Hilo!!!!
Sasa mnamtaka magufuli wa nini wakati zanzibar ni nchi na ina tume ilio huru
 
Mimi natamani tungevunja rasmi muungano!
MsemajiUkweli,
Kuvunja muungano tutakuwa sisi kama Waafrika tunajihujumu wenyewe.
Dunia ya leo ni mataifa kuja kuwa pamoja.

Angalia Wazanzibari wanavyoneemeka hapa Bara.

Hili ni jambo zuri sana na naamini hakuna katika Wazanzibari atafurahi
kutenganishwa na Tanganyika.
 
Hivyo mtu na akili yake timamu haijui dhulma masultani waliyokuwa wakiitenda kwa Wazanzibari? Huyo mtu atakuwa ni muenda wazimu au kichaa au hakuishi enzi hizo hapa Zanzibar!
Kwani dhulma ni kutiwa ndani tu? Kufanywa nyinyi kuwa ni kaumu ya kuwa watumishi wa ndani tu (maboi), au nyinyi kuwa kaumu ya kumaliza masomo darasa la 4 tu, au nyinyi kuwa kaumu ya wakwezi tu, etc hivyo hizi sio dhulma Shk Mohamed Said?
Ukoloni umeondoka but some of us are still living under the delirium of colonization!
Ngida,
Husemi kweli.

Akina Dr. Hassan Kingwaba walisoma wakati gani?
Juma Alley alisoma lini?

Aboud Jumbe alisoma wakati gani?

Ali Hassan Mwinyi, Hasnu Makame, Himidi Msoma
nk. nk orodha
ni ndefu.

Kuna list ndefu sana ya Wazanzibari walikwenda Makerere College.
Zungumza jela za mateso za Masultani na watu waliowauwa na kuwatesa.

Nyumba nyingi sana hapa Dar es Salaam tuna wafanyakazi wa ndani na
mashambani kwetu tunao hao wewe unawaita ''wakwezi.''

Isome mada na toa majibu stahiki sote tunufaike na mjadala propaganda
za utumwa na mama zetu kupigishwa deki kwa maziwa yao huu si wakati
wake.

Wazanzibari wengi wameuliwa kwa uongo huu 1964 ilhali utumwa ulikuwa
umekomeshwa zaidi ya miaka 200.

Tumuogope Allah tusiendeleze fitna hizi.
 
Sibonike,
Mambo si mepesi hivyo.
Bara wana majeshi ndani ya Zanzibar.

Wakitoa jeshi Zanzibar na kuwaacha Wazanzibari wamalize
matatizo yao wenyewe hutosikia lawama.

Wa kuchagua moja ni Bara.
Waingilie kuweka uwanja sawa au waondoe jeshi.
Sheikh mbona Zanzibar wana majeshi yao pia huku bara? Askari polisi pia wafanyikazi wa forodha warudishwe kwao Zanzibar
 
Ndugu bado sana hujakuwa kiakili ni askari gani wa tanganyika wamekuja huko mm navyofahamu askari wa tanganyika ambao wanzanzibari hawapo ni magereza pekee je niambie magereza huko wapo na kama polisi basi ni mchanganyiko ya wazanzibar na watanganyika vile vile jeshi ni wazanzibar na watanganyika hakuna jeshi la watanganyika pekee huko acha kauli ya kinafiki na istoshe kama hujui kitu jaribu kuuliza hata kama kuuliza huwez jaribu kutofautisha kati ya kifaru na hivyo vinavyopita huko nakujuza tu uliza kwamba hvyo ni vifaru sina utaalamu na mambo ya kijeshi lakin nilijaribu kuuliza nikaambiwa si vifari ni APC kama hujui basi hvyo ndo vinavyoitwa kwahyo acha mawazo mgando jaribu kupambanua kitu kabla ya kukurupuka na kupost vitu usivyovijua
APC ni nini na vifaru vinaangukia katika category gani?
 
Na imasemekana vita vya Kagera wanajeshi wa Zanzibar walipelekwa frontline na ndio waliokuwa wa mwanzo kuingia Kampala

Might is not right
 
Back
Top Bottom