Wazanzibar acheni unafiki na ndumilakuwili

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Unafiki na undumila kuwili kwa sasa umewaumbua. Mlificha magonjwa kwa unafiki na sasa kifo cha serikali ya umoja wa kitaifa kinawaumbua.

Mlimtumia Abubakar Khamis Bakary Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni kuwasilisha hoja binafsi kulitaka Baraza la Wawakilishi kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu kuanzishwa kwa Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar lakini katika mlengo wa kutaka kujitenga na Tanzania Bara. Hoja hiyo, ilikubaliwa na Baraza la Wawakilishi na kupelekea kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni Nam 6, 2010.

Mliamua kujifungia kwenye vyumba vya siri bila kuwashirikisha wananchi wa Tanzania Bara na mkafikia makubaliano ya kinafiki ya kubadilisha katiba yenu kwenye Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza ambayo kwa sasa inasema, Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yoyote inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.

Mbaya zaidi, kwa kupitia katiba yenu ya kinafiki mkatuaminisha kinafiki kuwa Tume ya Uchaguzi kwa sasa ni huru na inayojitegemea katika kutekeleza majukumu yake kupitia Kifungu cha 119 (13) kwa sababu ina wajumbe WANNE waliopendekezwa na vyama vya CUF na CCM. Mjumbe MMOJA aliyependekezwa na Rais. Jaji MMOJA aliyependekezwa na Mahakama Kuu na pia Mwenyekiti aliyeteuliwa na Rais kwa kadri anavyoona inafaa.

Mkasema wazi katika kifungu cha 119(13) kuwa: “Hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba”.

Hamkuishia hapo, mkatuambia kupitia Kifungu cha 119(4), kuwa pindi Mjumbe wa Tume anapoteuliwa, hakuna mtu/kiongozi mwenye mamlaka ya kumuondoa au kumfukuza Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi mpaka atakapotimiza miaka mitano tokea kuteuliwa kama Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi mkaifanya kama Jini ndani ya chupa, kwa sasa limetoka na hamuwezi kulirudisha ndani ya chupa! Mmebaki kulaumiana kuhusu nani aliyelitoa jini kwenye chupa!

Mkatuambia mmechoka kufanyiwa maamuzi na watu wa Tanganyika na kuanzia sasa vyenu ni vyenu wakati wa raha lakini wakati wa shinda, vyenu ni vyetu. Tuliwaambia haiwezekani vyenu viwe ni vyenu pekee wakati wa raha lakini wakati wa shida, vyenu viwe vyetu.

Mkasema Watanzania Bara wanachochea mtengane lakini kwa sasa mmeamua kushikamana. Tuliwaambia hiyo ndoa yenu haitadumu lakini mkabisha. Yamefika wapi?

Unafiki na undumila kuwili kwa sasa unawatafuna!

Maji mliyavulia nguo mkiwa mmejifungia ndani ya chumba cha siri, hamna budi vile vile kuyaoga.
 
mchawi wa wa Zanzibar ni Kikwete jakaya mrisho.by Mr seff.

swissme
Wewe hata kuandika tu ni majanga, utaweza kweli kuzipanua fikra zako ziwe katika 3D thinking?

Tatizo ni kwamba, inawezekana hufahamu kama hujui hata kuandika vizuri!

Sometimes you will never know the value of your ignorance and stupidity, until it becomes open secret!
 
mchawi wa wa Zanzibar ni Kikwete by seff

swissme
 
Mtoa mada huna hoja zaidi ya chuki zako tu kwa wazanzibar,adui wa wazanzibar tayari amekwisha fahamika,leteni majeshi na vifaru mtuuwe sote lakini huku zanzibar haturudi nyuma kudai haki ya maamuzi yetu ya tarehe 25-10-2015 iliyoporwa na mkoloni.
 
Unafiki na undumila kuwili kwa sasa umewaumbua. Mlificha magonjwa kwa unafiki na sasa kifo cha serikali ya umoja wa kitaifa kinawaumbua.

Mlimtumia Abubakar Khamis Bakary Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni kuwasilisha hoja binafsi kulitaka Baraza la Wawakilishi kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu kuanzishwa kwa Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Hoja hiyo, ilikubaliwa na Baraza la Wawakilishi na kupelekea kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni Nam 6, 2010.

Mliamua kujifungia kwenye vyumba vya siri bila kuwashirikisha wananchi wa Tanzania Bara na mkafikia makubaliano ya kinafiki ya kubadilisha katiba yenu kwenye Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza ambayo kwa sasa inasema, Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yoyote inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.

Mbaya zaidi, kwa kupitia katiba yenu ya kinafiki mkatuaminisha kinafiki kuwa Tume ya Uchaguzi kwa sasa ni huru na inayojitegemea katika kutekeleza majukumu yake kupitia Kifungu cha 119 (13) kwa sababu ina wajumbe WANNE waliopendekezwa na vyama vya CUF na CCM. Mjumbe MMOJA aliyependekezwa na Rais. Jaji MMOJA aliyependekezwa na Mahakama Kuu na pia Mwenyekiti aliyeteuliwa na Rais kwa kadri anavyoona inafaa.

Mkasema wazi katika kifungu cha 119(13) kuwa: “Hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba”.

Hamkuishia hapo, mkatuambia kupitia Kifungu cha 119(4), kuwa pindi Mjumbe wa Tume anapoteuliwa, hakuna mtu/kiongozi mwenye mamlaka ya kumuondoa au kumfukuza Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi mpaka atakapotimiza miaka mitano tokea kuteuliwa kama Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi mkaifanya kama Jini ndani ya chupa, kwa sasa limetoka na hamuwezi kulirudisha ndani ya chupa!

Mkatuambia mmechoka kufanyiwa maamuzi na watu wa Tanganyika na kuanzia sasa vyenu ni vyenu wakati wa raha lakini wakati wa shinda, vyenu ni vyetu. Tuliwaambia haiwezekani vyenu viwe ni vyenu pekee wakati wa raha lakini wakati wa shida, vyenu viwe vyetu.

Mkasema Watanzania Bara wanachochea mtengane lakini kwa sasa mmeamua kushikamana. Tuliwaambia hiyo ndoa yenu haitadumu lakini mkabisha. Yamefika wapi?

Unafiki na undumila kuwili kwa sasa unawatafuna!

Maji mliyavulia nguo mkiwa mmejifungia ndani ya chumba cha siri, hamna budi vile vile kuyaoga.

Mkuu Msemaji wa Ukweli napenda nikupe hongera kwa hii `analysis`yako nzuri kuhusu Zanzibar! Inavyonesha ya kwamba kumbe Wazanzibari tayari wamevunja muungano wetu na wala hatuna sifa tena ya kuitwa JMT! Mimi nakubaliana nawe kabisa na unaonaje tukaanza kuwahukumu Wazanzibari kwa kuwaondoa wale majeshi yetu kule zenji, Uhamiaji, TRA, polisi na mambo yote yanayohusu Muungano kule Zanzibar! Hata vyama vya siasa tukagawana na kuwa CCM Zanzibar na CCM Tanganyika! Tufanye uchaguzi mwengine pia wa Tanganyika tumhalilishe Magufuli awe ni Rais wa Watanganyika! Tuwaachie wazanzibari wajiamulie mambo yao wenyewe bila ya kuwaingilia. Hayo si mawazo yangu bali ni mwendelezo wa hicho ulichokiandika hapo juu!
 
Mkoa maada una nzito sana. Wenzetu hawana msimamo kamili hupima upepo unaenda wapi.

Kwenye mafuta ni masuala yao. Rais wa JMT hana madaraka. Kwenye vurugu zao za uchaguzi wanakumbuka madaraka ya Rais wa JMT.

Inabidi wachague moja. Haiwezi kuwa sawa kwa hili ikawa hapana kwa lile wakati Rais wa JMT ni huyo huyo.
 
Back
Top Bottom