salisalum
JF-Expert Member
- Oct 27, 2010
- 418
- 136
Ni kweli ndugu,hakuna wa kumnyooshea kidole mwenzake katika serikali.
Yeye angekuwa mwadilifu asingetetea Kulipa Dowans, asingedanganya umma mbele ya bunge tukufu,asingekubaliana na hoja ya kutafsiri upya kanuni za bunge na kusaliti watanzania, asingekuwa kimya wakati wasaidizi wake wamekula mabilioni kwenye ruzuku za wakulima,asingedanganya wanafunzi na wahadhiri UDOM.
Angewasikiliza watoto wa wakulima walipoandamana kutaka kupewa 10,000, asingeahirisha uchaguzi wa meya kule kigoma ili CCM watafakari watashindaje.
Hakuna kiongozi mnafiki ndani ya hii serikali kama Pinda ambaye alisoma seminari. Anataka kutueleza nini huyu?
Wanadamu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, Warumi 3:23. Hakuna mtu perfect kwenye serikari yote ya Kikwete, kwa wapinzani wote na kwa raia wote. Mungu alipochungulia duniani hakupata mwenye haki hata mmoja. Hata hao mashehe, wachungaji, maaskofu, wainjilisti na wazee wa makanisa ni binadamu tena wengine wapuuzi kabisa na mjoho au kanzu zao.
Kuwaambia viongozi wa dini wapambane na maovu serikalini si jambo la hekima. Serikali ndiyo ina mandate ya kupambana na rushwa. Watua hawachukui rushwa misikitini au kanisani wanachukuo huko maofsini wakiwa wamepewa baraka na wakubwa kama yeye pinda. Awaache maaskofu waendelee kunywa mvinyo na divai na sadaka zetu ambazo zingine ni matokeo ya ubadhilifu na rushwa, Ovyo kabisa!!