MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,223
- 22,299
Ninashangazwa na wafuasi wa CHADEMA siku ya leo wakimshambulia kiongozi mkuu wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania, Askofu Malasusa na kubaki na mshangao mkubwa. Lema na wanachama wengine waandamizi wameongoza mashambulizi makali dhidi ya kanisa na kiongozi wake. Inasikitisha sana.
Nimejiuliza je, KKKT ndo mpinzani mpya wa CHADEMA badala ya CCM? CHADEMA haioni kama inapoteza muda kushambulia kanisa? Haijui kuwa kiongozi wa kiroho anasikilizwa zaidi na watu kuliko kiongozi wa kisiasa? Askofu Malasusa kwa sasa ndo kabeba dhamana ya kuongoza waumini wote wa KKKT Tanzania na hivyo kumshambulia yeye ni kulishambulia kanisa zima. Athari zinazoweza kujitokeza ni CHADEMA kuzidi kupoteza zaidi kura zake kutoka kwa waumini wa KKKT.
Ninawashauri CHADEMA waache mara moja mashambulizi dhidi ya Askofu Malasusa. Haina faida yoyote kisiasa.