Waumini wenu sio waadilifu! - Pinda

Ni kweli ndugu,hakuna wa kumnyooshea kidole mwenzake katika serikali.

Yeye angekuwa mwadilifu asingetetea Kulipa Dowans, asingedanganya umma mbele ya bunge tukufu,asingekubaliana na hoja ya kutafsiri upya kanuni za bunge na kusaliti watanzania, asingekuwa kimya wakati wasaidizi wake wamekula mabilioni kwenye ruzuku za wakulima,asingedanganya wanafunzi na wahadhiri UDOM.

Angewasikiliza watoto wa wakulima walipoandamana kutaka kupewa 10,000, asingeahirisha uchaguzi wa meya kule kigoma ili CCM watafakari watashindaje.

Hakuna kiongozi mnafiki ndani ya hii serikali kama Pinda ambaye alisoma seminari. Anataka kutueleza nini huyu?

Wanadamu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, Warumi 3:23. Hakuna mtu perfect kwenye serikari yote ya Kikwete, kwa wapinzani wote na kwa raia wote. Mungu alipochungulia duniani hakupata mwenye haki hata mmoja. Hata hao mashehe, wachungaji, maaskofu, wainjilisti na wazee wa makanisa ni binadamu tena wengine wapuuzi kabisa na mjoho au kanzu zao.

Kuwaambia viongozi wa dini wapambane na maovu serikalini si jambo la hekima. Serikali ndiyo ina mandate ya kupambana na rushwa. Watua hawachukui rushwa misikitini au kanisani wanachukuo huko maofsini wakiwa wamepewa baraka na wakubwa kama yeye pinda. Awaache maaskofu waendelee kunywa mvinyo na divai na sadaka zetu ambazo zingine ni matokeo ya ubadhilifu na rushwa, Ovyo kabisa!!
 
kiboko ya "mwongo" pinda hii hapa! nilidhani angeanza na kuungama dhambi zake kabla hajavamnia maboriti ya wenzake! hapa godbless alikuwa anatangaza kuwa ana nondo 23 za kudhibitisha kuwa pinda ni mwongo wakati wa ufunguzi wa tawi chuo cha mipango
 
Attachments

  • IMAG0234.jpg
    IMAG0234.jpg
    302.3 KB · Views: 28
Mh. Pinda! Sema "nimepoteza uadilifu wangu wa kwanza viongozi wangu wa dini niombeeni nipone" na siyo Waumini wenu wengi hawana uadilifu. Ala!
 
Nashangaa kwanini watu wana badili maana,uadilifu si kwa viongozi tu hata sisi tunaongozwa yatupasa kuwa waadilifu na kumuogopa Mungu katika yote tunayofanya!
tunawaangalia sana viongozi which is ok,lakini pia matendo yetu sisi yakoje????:hand::hand::rain:
they are our role models, we are doing what they are doing, lol.
 
so far kwa maneno yaliyoandikwa hapo juu Mh Pinda is quite right..................

Is quite right for what while he Bogas like you . How comes you know the people who are stilling our things then you hawachukulii hatua huyu nae ni mpuuzi tu
 
MP usitumie mwavuli wa dini kuficha uchafu wa serikali yenu. hakuna siri chionio ya mbingu mnajidanganya tu mtaendelea kuaibika na bado
 
Hivi ni kweli au usanii jamani
Raia wanalalamika, wajumbe wa nyumba kumi, mawaziri, waziri mkuu, raisi wote malalamiko nani sasa wa kutatua?
Nilitegemea Pinda angesema kwamba ufumbuzi wa hayo yote ni mkutano wa katiba. leo anaachia maaskofu kazi kwani dini zimeanza leo? aidha tuna ombwe la uongozi ima wanafanya usanii na kufikiria bado ni zama za Juliasi.
 
Pinda awageukia viongozi wa dini

Imeandikwa na Mwandishi Maalumu (HabariLeo), Bunda; Tarehe: 21st February 2011

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema viongozi wa dini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhimiza uadilifu miongoni mwa waumini wao, kwa sababu wengi wao ndiyo waajiriwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo Serikali.

Amesema katika kundi kubwa la waumini, wamo watumishi wasiotimiza wajibu wao na hata wengine kudiriki kuiba au kupokea rushwa, lakini wote ni waumini wao na wanahitaji
kuchungwa kiroho.

Alitoa rai hiyo katika Kanisa la Mtakatifu Paulo wilayani Bunda, mkoani Mara wakati wa sherehe za kumsimika Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bunda, Mhashamu Renatus Nkwenda.

Waziri Mkuu aliyefika Bunda kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko safarini Mauritania, alisema: "Baba Askofu umeteuliwa kushika jimbo hili jipya katika kipindi ambacho kuna changamoto nyingi za umasikini, za waumini waadilifu na wasio waadilifu, kondoo wanaotuongoza sisi, hao hao ndiyo wezi na wengine wala rushwa ambao tuko Serikalini…lakini ni kondoo wako."

Alisema viongozi wote wawe wa dini au wa Serikali hawana budi kulivalia njuga suala la uadilifu ndani ya nchi kwani hali imefikia pabaya.

"Ninyi mnayo nafasi kubwa ya kiroho na kimwili, lakini ni lazima sote tulivalie njuga… lazima tupige kelele, tukipukutisha maadili ya nchi, sote twafa," alisema Waziri Mkuu.

Akiwahutubia maelfu ya waumini walioshiriki ibada hiyo, Waziri Mkuu alisema kila mmoja ana jukumu la kulinda amani na utulivu wa nchi ambavyo vimedumu kwa miaka 50.

"Sisi tumepokea wakimbizi kutoka kila kona, leo hii tukivurugana tutakwenda wapi? Rwanda au Burundi ambako hawana ardhi ya kutosha?" Alihoji.

Alitumia fursa hiyo kuwakumbusha Watanzania kwa wasibaguane kwa misingi ya dini, kabila au jinsi kwani kwa kufanya hivyo, Taifa litasambaratika.

Mapema, akitoa nasaha katika ibada hiyo kabla ya kuweka wakfu Askofu Mteule Renatus Nkwande,
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo alisema Askofu Nkwande amepata uongozi katika kipindi ambacho kuna changamoto ya mgawanyiko baina ya viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa Serikali ambayo matokeo yake yanawaumiza wananchi walio wengi.

Alisema changamoto zilizopo, hana budi kukabiliana nazo, lakini akamtaka awe tayari kuubaini uovu na kuusimamia ukweli hata kama itagharimu maisha yake.

"Si vizuri kuunyamazia uovu na kushindwa kuutambua kuwa ni uovu. Ni vema kuwa na ujasiri wa kulitamka na kulisema hili ovu… Huu ndiyo msimamo unaotakiwa katika Tanzania ya sasa," alisema Pengo.

"Uwe na ujasiri wa kusimama nyuma ya ukweli na kufa kwa ajili ya hilo… ukiogopa kufa leo utakufa kesho.

Ukiogopa kusema ukweli leo, kesho au kesho kutwa utakufa, kikubwa ni kuhakiksha unakufa katika mikono ya Kristu na si vinginevyo."

Naye Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Askofu Juda Thadeus Ruwa'ichi wa Jimbo Katoliki la Mwanza akizungumza kwa niaba ya maaskofu wote wa TEC, alisema wao kama viongozi wataendelea kuhimiza mshikamano wa Kitaifa licha ya kudaiwa kuwa wao ni wa dini.

Alisema wanaodai hivyo wana lao na kuongeza: "Sisi siyo wadini, bali ni wakweli, wenye uwezo wa kukemea na kusahihisha mambo yanapokwenda ndivyo sivyo.

Kama hatukuwahi kuwagawa raia huko nyuma kamwe hatutafanya hivyo kesho wala kesho kutwa," alieleza Ruwa'ichi.

Mhashamu Askofu Nkwande aliyesimikwa jana, alizaliwa Novemba 12, 1965 katika Kijiji cha Mantare, Sumve, wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 10 wa Mzee Alphonce Masalu na Mama Mamertha Masabula.

Mtoto mmoja alifariki na sasa wamebaki watoto tisa. Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Enos

Mfuru, wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Mara, maaskofu 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na mapadri na watawa kadhaa.

Source: Habari leo (Pinda awageukia viongozi wa dini)
 
Pinda awageukia viongozi wa dini
Imeandikwa na Mwandishi Maalumu, Bunda; Tarehe: 21st February 2011 @ 08:31 Imesomwa na watu: 397; Jumla ya maoni: 0

Mapema, akitoa nasaha katika ibada hiyo kabla ya kuweka wakfu Askofu Mteule Renatus Nkwande, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo alisema Askofu Nkwande amepata uongozi katika kipindi ambacho kuna changamoto ya mgawanyiko baina ya viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa Serikali ambayo matokeo yake yanawaumiza wananchi walio wengi.

Alisema changamoto zilizopo, hana budi kukabiliana nazo, lakini akamtaka awe tayari kuubaini uovu na kuusimamia ukweli hata kama itagharimu maisha yake.

"Si vizuri kuunyamazia uovu na kushindwa kuutambua kuwa ni uovu. Ni vema kuwa na ujasiri wa kulitamka na kulisema hili ovu… Huu ndiyo msimamo unaotakiwa katika Tanzania ya sasa," alisema Pengo.

"Uwe na ujasiri wa kusimama nyuma ya ukweli na kufa kwa ajili ya hilo… ukiogopa kufa leo utakufa kesho.

Ukiogopa kusema ukweli leo, kesho au kesho kutwa utakufa, kikubwa ni kuhakiksha unakufa katika mikono ya Kristu na si vinginevyo."

Naye Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Askofu Juda Thadeus Ruwa'ichi wa Jimbo Katoliki la Mwanza akizungumza kwa niaba ya maaskofu wote wa TEC, alisema wao kama viongozi wataendelea kuhimiza mshikamano wa Kitaifa licha ya kudaiwa kuwa wao ni wa dini.

Alisema wanaodai hivyo wana lao na kuongeza: "Sisi siyo wadini, bali ni wakweli, wenye uwezo wa kukemea na kusahihisha mambo yanapokwenda ndivyo sivyo.

Kama hatukuwahi kuwagawa raia huko nyuma kamwe hatutafanya hivyo kesho wala kesho kutwa," alieleza Ruwa'ichi.

Mhashamu Askofu Nkwande aliyesimikwa jana, alizaliwa Novemba 12, 1965 katika Kijiji cha Mantare, Sumve, wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 10 wa Mzee Alphonce Masalu na Mama Mamertha Masabula.

Mtoto mmoja alifariki na sasa wamebaki watoto tisa. Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Enos

Mfuru, wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Mara, maaskofu 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na mapadri na watawa kadhaa.
 
Habari imeambatanishwa na source yake "Habari leo" sasa unaposema haina source una maana gani? Hatupendi kujaza sana nafasi hapa ila maudhui ya habari na ukitaka kupata supu yote nenda kwenye source yake utaridhia ukweli.
 
Pinda awageukia viongozi wa dini

Imeandikwa na Mwandishi Maalumu (HabariLeo), Bunda; Tarehe: 21st February 2011

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema viongozi wa dini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhimiza uadilifu miongoni mwa waumini wao, kwa sababu wengi wao ndiyo waajiriwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo Serikali.

Amesema katika kundi kubwa la waumini, wamo watumishi wasiotimiza wajibu wao na hata wengine kudiriki kuiba au kupokea rushwa, lakini wote ni waumini wao na wanahitaji
kuchungwa kiroho.

Alitoa rai hiyo katika Kanisa la Mtakatifu Paulo wilayani Bunda, mkoani Mara wakati wa sherehe za kumsimika Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bunda, Mhashamu Renatus Nkwenda.

Waziri Mkuu aliyefika Bunda kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko safarini Mauritania, alisema: "Baba Askofu umeteuliwa kushika jimbo hili jipya katika kipindi ambacho kuna changamoto nyingi za umasikini, za waumini waadilifu na wasio waadilifu, kondoo wanaotuongoza sisi, hao hao ndiyo wezi na wengine wala rushwa ambao tuko Serikalini…lakini ni kondoo wako."

Alisema viongozi wote wawe wa dini au wa Serikali hawana budi kulivalia njuga suala la uadilifu ndani ya nchi kwani hali imefikia pabaya.

"Ninyi mnayo nafasi kubwa ya kiroho na kimwili, lakini ni lazima sote tulivalie njuga… lazima tupige kelele, tukipukutisha maadili ya nchi, sote twafa," alisema Waziri Mkuu.

Akiwahutubia maelfu ya waumini walioshiriki ibada hiyo, Waziri Mkuu alisema kila mmoja ana jukumu la kulinda amani na utulivu wa nchi ambavyo vimedumu kwa miaka 50.

"Sisi tumepokea wakimbizi kutoka kila kona, leo hii tukivurugana tutakwenda wapi? Rwanda au Burundi ambako hawana ardhi ya kutosha?" Alihoji.

Alitumia fursa hiyo kuwakumbusha Watanzania kwa wasibaguane kwa misingi ya dini, kabila au jinsi kwani kwa kufanya hivyo, Taifa litasambaratika.

Mapema, akitoa nasaha katika ibada hiyo kabla ya kuweka wakfu Askofu Mteule Renatus Nkwande,
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo alisema Askofu Nkwande amepata uongozi katika kipindi ambacho kuna changamoto ya mgawanyiko baina ya viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa Serikali ambayo matokeo yake yanawaumiza wananchi walio wengi.

Alisema changamoto zilizopo, hana budi kukabiliana nazo, lakini akamtaka awe tayari kuubaini uovu na kuusimamia ukweli hata kama itagharimu maisha yake.

"Si vizuri kuunyamazia uovu na kushindwa kuutambua kuwa ni uovu. Ni vema kuwa na ujasiri wa kulitamka na kulisema hili ovu… Huu ndiyo msimamo unaotakiwa katika Tanzania ya sasa," alisema Pengo.

"Uwe na ujasiri wa kusimama nyuma ya ukweli na kufa kwa ajili ya hilo… ukiogopa kufa leo utakufa kesho.

Ukiogopa kusema ukweli leo, kesho au kesho kutwa utakufa, kikubwa ni kuhakiksha unakufa katika mikono ya Kristu na si vinginevyo."

Naye Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Askofu Juda Thadeus Ruwa'ichi wa Jimbo Katoliki la Mwanza akizungumza kwa niaba ya maaskofu wote wa TEC, alisema wao kama viongozi wataendelea kuhimiza mshikamano wa Kitaifa licha ya kudaiwa kuwa wao ni wa dini.

Alisema wanaodai hivyo wana lao na kuongeza: "Sisi siyo wadini, bali ni wakweli, wenye uwezo wa kukemea na kusahihisha mambo yanapokwenda ndivyo sivyo.

Kama hatukuwahi kuwagawa raia huko nyuma kamwe hatutafanya hivyo kesho wala kesho kutwa," alieleza Ruwa'ichi.

Mhashamu Askofu Nkwande aliyesimikwa jana, alizaliwa Novemba 12, 1965 katika Kijiji cha Mantare, Sumve, wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 10 wa Mzee Alphonce Masalu na Mama Mamertha Masabula.

Mtoto mmoja alifariki na sasa wamebaki watoto tisa. Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Enos

Mfuru, wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Mara, maaskofu 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na mapadri na watawa kadhaa.

Source: Habari leo (Pinda awageukia viongozi wa dini)

Wana uhakika na wanalolisema (Kwenye Green)? Inakuwaje ambapo maaskofu walikuwa wanatuambia ni nani tumchague. Waendelee tu na kukosoa ila wafikishie ujumbe kuwa hekima na maarifa ni vizuri vikatumika wakati wanapokosoa serikali venginevyo vita vikianza wananchi watawaanzia wao wao wasije kukimbia tu nchi.
 
Mashekh wetu walishatowa tamko lao kwamba sisi waisilamu tunaweza kuwanyamazisha hao maaskofu serikali iseme tu kama imeshindwa wanafik wakubwa hao ndio wanaosababisha chokochoko sasa wakae kimya.
 
Leave the Bishops alone. Mnawashambulia kijinga. Wao wanawatumikieni, irrespective of your religious affiliation. Wote hapa mnataka watoto wenu wasome shule kama Marian au St. Joseph ambazo ni za Kikatoliki. Sehemu nyingi vijijini mkiugua mnatibiwa kwenye zahanati za hao hao Maaskofu.

Maaskofu wangekuwa wadini wangewatibuni na kuwasomesheni kama wanavyofanya? Hamna shukrani hata chembe.
 
Mashekh wetu walishatowa tamko lao kwamba sisi waisilamu tunaweza kuwanyamazisha hao maaskofu

Hebu tupatie mfano angalau mmoja wa jinsi mlivyofanikwa "kuwanyamazisha hao maaskofu"?

Zaidi ya fujo na mashambulio ya mabomu ya kujitoa mhanga, Historia inaonyesha jeuri hiyo hamna. Fujo, nguvu na maovu makubwa ya haki za binadamu ndiyo jadi yenu Waislamu: angalia yanayotokea Mashariki ya Kati hivi sasa.

Halafu mnadai ni nyie pekee ndiyo mliyotoa mchango mkubwa wakati wa harakati za kutafuta Uhuru kutoka Wakoloni?? Sasa tunakaa tena pembeni tukitegemea mfanye tena vitu vyenu na kuingia mitaani kuwaondoa mafisadi wa CCM kama yalivyo mapinduzi ya nguvu katika nchi za Kiislamu nyingi kwenye nyakati hizi za sasa.
 
Jamani tuache udini ndani ya JF. Mifano hii ni dalili mbaya. Tunaona ni vitu vidogo, lakini mitandao hii imeweza kuleta neema au maafa makubwa katika pande nyingine za dunia.
 
Hatuwezi kuacha udini humu as long as wadini wamejazana, hatutakaa kimya tukiwasikiliza watu kama hawa wenye narrow mind. Yote yanayosemwa juu yao humu ni kweli unafiki wa maaskofu ni upo kama sio wao wanaoiona CCM kwa macho ya udini, miaka yao imekwisha tutaona watafanyaje, Ngoja Lowasa aingie tutaona huu uchafu watauongelea nini. Majuzi nilikua mahali pakali sana eti nakuta mjadala wa pongezi kwa JK alivyofanya kweli kwa kuwapanga waislamu sehemu nyeti, wakawa wana refer nafasi za uwasiri wa elimu, fedha, mawasiliano, mambo ya ndani, jeshi la polisi, mashirika muhimu yaliyopewa directing ya kusomesha watoto wao Ramadhani Dau wa NSSF akisifiwa kama kinara wa uratibu wa hayo. Cha ajabu hata nilipojaribu kuwajulisha kwamba hiyo ni somehow public place wakazidi kusema wao hawajali wana evidence kwamba wakristo wamekamatwa ma malori ya mapanga na silaha nyingine huko morogoro wakijiandaa kuleta vita, can you imagine? such a low level of inciting uvunjifu wa amani kwa kutumia intelijensia yao. Halafu mtu akisema tu juu ya hali halisi hapa inayotumia common sense mnang'aka udini, msitumie hiyo silaha kutufumba macho jamani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom