Waumini wenu sio waadilifu! - Pinda

Mh. PINDA yupo sahihi kabisa: WATUHUMIWA KARIBU WOTE WA UFISADI NA UBADHIRIFU WA UMMA NI WAUMINI WA KANISA. NA WAMETOA MCHANGO MKUBWA KULIFIKISHA KANISA HAPO LILIPO. NDIO MAANA TUKAONA JINSI WALIVYOWAPOKEA BAADHI YA MAFISADI (EL) KISHUJAA(mou).
Mkakati uliopo sasa ni kujisafisha - au kwa lugha nyepesi KUHAMISHA UFISADI KUTOKA CCM - CDM. NI AIBU YA KARNE. Pinda kawatolea uvivu. Anayemponda Pinda naye FISADI muathirika.

FISADI NO 1 RA NI muislam anayetoa misaada mikubwa misikitini huyu hujamwona we boya kweli
 
Mafisa wakubwa wamesha asi dini limebaki jina tu hawajui milango ya misikiti na makanisa iko wapi viongozi wakuu kama pm ndo wakemee. Kwanza viongozi wa dini wakikemea wanaambiwa wanaingilia siasa
 
How dare he??!!!..... Juzi tu ametoka kuongea uongo bungeni leo anathubutu kunyooshea wenzie kidole kwa kutokua na uadilifu???? Ama kweli.. once a "msanii".... always a "msanii" Mr. PM..... practice what you preach!!!!!.... and stop playing saint!!!!..... Hypocrite!!!!
 
Nashangaa kwanini watu wana badili maana,uadilifu si kwa viongozi tu hata sisi tunaongozwa yatupasa kuwa waadilifu na kumuogopa Mungu katika yote tunayofanya!
tunawaangalia sana viongozi which is ok,lakini pia matendo yetu sisi yakoje????:hand::hand::rain:
Ndo maana DR alisema ni system kuibadili nimeamini aiseee!
 
Tunawapa nguvu wasizostahili kuwa nazo viongozi wa dini kwa kuwalilia hali kama alivyofanya WM jana. Tufike mahala tuziweke dini na haki za binadamu pembeni ili kupambana kiukweli na ufisadi na rushwa. Hii lelemama ya majukwaani, kwenye sherehe na misiba haitusaidii.
 
Kwanini Waziri Mkuu Peter Pinda hupenda sana kulalama tu?

Uadilifu wa Waumini sio suluhisho la Wizi wa watumishi serikalini!

Kwa mtizamo wangu "mafisadi" wengi wana nafasi kubwa kwenye Makanisa
 
Sawa ndugu Pinda waumini wetu sio waaminifu,sasa tufanyeje ndilo swali la kujiuliza na kufanyia kazi...................waziri mkuu hauna maamuzi kabisaa _ mara ulie bungeni,mara uwaombe watu wawazomee mafisadi kwa kelele za mwiziiiiiiiiiii,mara useme waumini sio waadilifu.....you are coward like yourself.
 
FISADI NO 1 RA NI muislam anayetoa misaada mikubwa misikitini huyu hujamwona we boya kweli

Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaa hahahahaha aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Kwikwikwikwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!
Kaka umesahau issue ya Mchungaji Mtikila na RA ????.Hata miaka miwili haijapita mzee. Halafu ni msikiti gani RA aliwahi kusaidia?? Tutajie japo hata msikiti mmoja tu na kiasi alichochangia! Kule si anajua haziwezi kukubaliwa? Lakini kanisani aa wee acha tu! KIINGIACHO SI HARAMU MZEE BALI KITOKACHO!! UPO Mr. SMART?

Halafu ni vizuri kutofautisha mambo. Si kila Muirani au mtu mwenye asili ya Irani ni Muislamu. Ni uislamu ndio uliowakomboa wairani lakini walikuwa wakiabudu moto na nyota. Fuatilia uone kama RA huwa anaswali msiktini. Tusaidiane katika hili.
 
Weak PM is trying to escape his duties "my GOd" ..hawa viongozi wa dini wakitoa matamko ya kulaani viongozi wasio waadilifu mnasema wavue majoho waingie kwa siasa wakikaa kimya mnaanza matamko ya kijinga shame on you pinda!!! we endelea kulia 2shakuzoea huna nguvu ya kuwajibisha wazembe!!!
 
Hii ni ngumu sana maana hata harambee au ufadhili mwingi wa kanisani unawalenga waaumini ambao historia ya utajiri wao ni wa mashaka.
 
watu wanapindisha hoja alichosema pinda ni sahihi kabisa.. Yaani watu wanakuwa na chuki mpaka hawataki kungalia hoja.
 
Pinda pinda pinda!!!!!!! Hivi juzi kadanganya Bunge na watanzania wote leo anawasakama waumini wa kanisa eti sio waadilifu au anadhani uongo ni uadilifu
 
Dini ni hiyari ya mtu, na miaka inavyokwenda wengi wanajitoa huko kwenye dini.........kwa hiyo mtu anaweza kufuata mafundisho au kuacha kufuata. On the contrary sheria za nchi ni lazima kwa wote wazifuate as long as kuna usimamizi mzuri na na wa haki. Unajua nchi za Ulaya majority hawaendi kanisani nowdays, wameturn to be "non-believers" lakini husikii habari za rushwa na mambo yake...Ukisikia mtu amekamatwa na anachukliwa hatua.

So hapa kina Pinda wasikimbie wajibu wao wa kuhakikisha kunakuwa na sheria, system na institution za kusimamia hizo sheria. Mfano mtu anajulikana ameanza kazi leo baada ya miezi 6 ana utajiri wa kufa mtu hakuna hatua za kuhoji zinachukuliwa, ina maana system zetu zina weakness hapo.

Nakumbuka kuna wakati JK alikuja na idea ya kutaka kutenganisha SIASA na BIASHARA naona aliingia mitini na hoja yake baada ya likely kupigwa mkwara na vingunge wa CCM. Sasa wao kama viongozi wanaogopa kuweka sera/sheria nzuri kwa manufaa ya majority then wanatia aibu kwenda kulalamika mbele ya umma.
 
Mimi nilishangaa pale PM alipokataa kutumia shangingi eti anaonesha mfano, wakati mawaziri wake wanatumia sisi inatusaidia nini, tunataka viongozi watakaokuwa na uwezo wa kuendesha nchi, eti anasemaje: kwa hiyo alitaka mapadre na mashehe ndio wawafukuze kazi waliosababisha mabomu yakalipuka kwa uzembe wao na kuuwa raia wema wa Tanzania huku wakiacha familia zao bila msaada katika kipindi kigumu namna hii.

2. nimekumbuka kuna kitengo cha intelijensia hivi nacho kilishindwa kugundua kwamba mabomu yengelipuka ili angalau kitengo chetu cha intelijensia kiwe kimetoa mchango kwa wananchi ambao ndio wanakilipa mishahara?

Sina Mengi
 
so far kwa maneno yaliyoandikwa hapo juu Mh Pinda is quite right..................

Kuna ukweli gani mkuu? Mess iko kwao anataka clerics wasafishe. Nina amini leo ukimpa nguvu za dola sheikh mkuu halafu umwambie safisa serikali in few days itakuwa safi. Serikali ndio ina nguvu ya dola ya kukamata watu ovyo na kuwashughulikia, kama anaanza kuwakosoa clerics wakati uozo mkubwa uko serikalini, ni kuongea asilia 5 ya ukweli.
 
avatar mfamaji na kapotolo ni walewale? hesabu na kemia zinamsumbua sana huyu jamaa tehetehetehete kama jk!:A S 112:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom