JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,053
- 14,873
"Kuna, muuza, chips mwenge anapata faida ya milioni7 kwa mwezi, kuna muuza chipsi keko anatengeneza faida ya laki 4 kwa mwezi!Hi!
Si Wajasiriamali wote kwamba wana maisha mazuri kuliko Watumishi wa Umma ila nataka kusema kuwa wapo Wajasiriamali wengi tu ambao hata leseni ya biashara hawana, Kodi hawalipi kabisa na Serikali haiwatambui lakini wana pesa kuliko wenye maduka ambao hulipa Kodi kwa VAT.
Kuna Jamaa anauza Ugali nyama choma, huyu bwana akiondoa gharama zote za uendeshaji anapata faida ya TZS 200,000/- mpaka TZS 300,000/- kwa siku. Maana yake huyu kwa mwezi amefeli amepata faida ya TZS 5,000,000/-. Pesa ambayo wanalipwa Watumishi Waandamizi Wizarani. Hapo ameshatumia pesa ya kutosha ndani ya huo mwezi mwisho wa mwezi ana TZS 5,000,000/- .
Mtumishi Mwandamizi akipata hiyo TZS 5,000.000/- ndipo aanze kutumia, atasave Million Moja au Laki 5 tu. Kuna dogo anauza chips Mwenge kwa siku analaza Laki 3.5. Huyu baada ya matumizi yake yote mwisho wa mwezi akichungulia akiba yake hakosi Milioni 7. Faida ya Milioni 7 kwa mwezi ni Watumishi wa Umma wangapi wanaipata? Labda majizi tu ambayo hawana amani maana jela inawaita kila siku.
Kuna muuza chips Keko kwa siku anapata faida ya Laki 4 . Na jinsi alivyo bahiLi yule kwa mwezi analaza mpaka Milioni 10. Halipi kodi hata mia, kajenga mjengo Madale nahisi hata baadhi ya Wabunge hawana Nyumba kama ile.
Tisidharauliane ndugu. Kuna Watumishi wengi tu wa chini wamewazidi maisha mabosi zao.
Mimi ni Mwajiriwa ila nakiri kuwa utajiri nitasikilizia redioni tu. Kwa mishahara hii tusubiri kifuta machozi cha kustaafu labda au tuibe tunawiri na mwisho tukafungwe.
Nimesoma mpaka Nika Cheka mpaka mbavu zikauma,haya maubili yako haya na tofauti na wale waxhingaji, utawasikia, wakisema" Namuona mama mmoja, mama neema, anasumbuliwa na tumbo,na kule namuona Dada nancy, mchango wa tumbo unamsumbua kwa mwaka mzima sasa"pokeeni uponyaji!
Hizi hesabu zako, kawasimulie wa Toto wa kindergarten, kama unapata faidi ya laki 4 kwa siku, chukulia kila sahani ya chips, unapata faida ya buku, ina maana itabidi uuze sahani 400! Kwa siku!
Bro unajua nyomi ya watu 400! Hakuna, uhalisia, kibanda cha, chipsi, cha kawaida kihudumie watu 400! Kwa, siku,
Pili kama mapato Yao ndio hayo,milioni 7 net kwa mwezi, mbona hatuwaoni wakisomesha wa Toto kwenye shule zetu za kimombo ambazo sie watumishi wa serikali na mishahara yetu ya vima vya chini tunasomesha?
Hatuwaoni wakiwa wapangaji wenzetu huku msasani,mbezi beach, wengi wao wapo kawe, mbagara!
Hatukutani nao kwenye ujenzi bagamoyo, kigamboni! Sasa pesa zao, zipo, wapi? Au za majini?
Acha story za kwenye makaratasi, hazina uhalisia,
Ukiwa na surplus, disposable income maisha yako, yataonwkana tu, outing nyingi, ndinga,majumba, Arya Bora, sasa unaowazungumzia,
Kwa kimombo tunawaita"wretched of the earth"