pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 243
- 461
Wasaaalam wana jukwaa, leo katika pita pita zangu za mjini nilienda ofisi moja ya muhimu sana, nikakuta watumishi wako muda wa mapumziko, nilifanikiwa kuchangamana nao na kujadili mawili matatu.
Nilimsikia mmoja akisema kwamba amemaliza kusoma na hataki tena (training) ya aina yoyote kwa maana mpaka sasa bado hajapanda daraja, na akasema kwamba anataka ahamie Sekta Binafsi.
Wenzake wakaanza kumpinga kwa maneno makali kuwa kule sekata binafsi hakuna usalama wa ajira (job security). Wakaendelea kusema kuwa kule ukiiba kidogo tu unafukuzwa.
Nikajiuliza maswali mengi sana mpaka nikajua kuwa siye tuliopo Sekta Binafsi tume risk kwani ajira zetu zipo mikononi mwa waajiri hivyo kama hauna misuli ya kusimamia sheria ya mahusiano kazini basi ajira yako inaweza kuisha kizembe tofauti na wale wenzetu wanaovaa jeans na vitenge na walioruhusiwa kula urefu wa kamba zao yaani watumishi wa umma.
Baada ya kufikiria nikaona nije na wazo kuwa kiasi cha kodi tunachokatwa sekta binafsi kiwe na nafuu kidogo ukilinganisha na hawa ndugu zetu wenye ajira za kudumu ambao wameambiwa kuwa wale kidogo wasile mpaka wakavimbewa wanaovaa kama wasabato na majibu ya hovyo maana wanajua utaratibu wa kuwaondosha kazini ni mgumu ama hauwezekani.
Naomba kuwasilisha