matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,724
- 15,703
Kuendekeza makundi ya vijana wanaoibuka kwa kasi wakiringishia utajiri wao na marundo ya fedha huku hawaonyeshi vyanzo vyao halali vya mapato ni kuharibu jamii hasa vijana.
Kama nia ni kuhamasisha vijana muhamasishe kwa kuonyesha na chanzo, mbinu na namna mnanavyopata hizo fedha za maringishio tena kwa fasterfaster.
Muonyeshe ni kiasi gani mmechangia kama kodi kwa taifa ya vipato hivyo.
Angalau na financial statements ya vipato vyenu.
Wazuiwe kutia vijana midadi ya kifedha bila kuwaonyesha njia.
Hali hii isipoangaliwa kwa jicho la kesho, tutaishia kuzalisha vijana wa hovyo, waliotayari kupoteza hata uvulana na usichana wao ili wapate fungu la kuringishia online, wauza madawa ya kulevya na punda wengi, Majambazi, Wachawi etc.
Nini maoni yako.