Watu wanaoonyesha maburungutu ya hela mitandaoni bila kuonyesha chanzo wapigwe marufuku?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,595
15,389
Kuendekeza makundi ya vijana wanaoibuka kwa kasi wakiringishia utajiri wao na marundo ya fedha huku hawaonyeshi vyanzo vyao halali vya mapato ni kuharibu jamii hasa vijana.

Kama nia ni kuhamasisha vijana muhamasishe kwa kuonyesha na chanzo, mbinu na namna mnanavyopata hizo fedha za maringishio tena kwa fasterfaster.

Muonyeshe ni kiasi gani mmechangia kama kodi kwa taifa ya vipato hivyo.

Angalau na financial statements ya vipato vyenu.

Wazuiwe kutia vijana midadi ya kifedha bila kuwaonyesha njia.

Hali hii isipoangaliwa kwa jicho la kesho, tutaishia kuzalisha vijana wa hovyo, waliotayari kupoteza hata uvulana na usichana wao ili wapate fungu la kuringishia online, wauza madawa ya kulevya na punda wengi, Majambazi, Wachawi etc.


Nini maoni yako.
 
Kwani kisheria ikoje mtu kuonyesha pesa hadhani bila hitaji la msingi
Sio kama kuichezea na kuinajisi pesa ya Tanzania
Usalama wao ukoje kutembea na pesa nyingi hivo inaweza kuleta uharifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa kaongea kitu cha msingi sana. Ila wanaombeza ni wapumbavu sana. Hawa jamaa waneweza kutumika kufanya money laundry kitu ambacho ni hatari kwa taifa.
Hakuna cha money laundering.. maiaha ya mtandaoni hayana uhalisia
 
Endelea kutoa macho hvo hvo kwenye Dp haya maisha hayana part 2 kwahyo ukipata Dili pita nalo hakuna pesa nyingi bila risk haijalishi ni nn unarisk so ukiona risk unaimudu pita nayo
 
Wewe acha kashfa kwa watu mzee Raia wanachimba Madini tafuta sekta yenye hela jiingize mfano ni zile ambazo mnyororo wake ww thamani mkubwa.kilimo,ufugaji,madini,Uvuvi,mafuta,mitandao,betting,utapeli,drugs,uwindaji,n.k
 
Back
Top Bottom