[h=3]WAKAZI zaidi ya 3,000 wa Bugudadi, Mbagala katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wako mbioni kuondolewa kwenye maeneo wanayoishi mabondeni ili kupisha uhakiki na tathimini ya nyumba zao.[/h]Tayari nyumba zao ziwekewa alama ya X huku kukiwa hakuna taarifa za kutosha kutoka kwa viongozi kuhusu hatua hiyo.
Hayo yalibainika jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa Diwani wa Mbagala, Agrey Kayombo na wananchi.
Wananchi hao walifikisha kilio chao kwa diwani kuwa wamekumbwa na wasiwasi baada ya nyumba zao kuwekwa alama hiyo huku kukiwa hakuna taarifa za kujitosheleza kutoka kwa viongozi wa wilaya yao.
Hii hali imetushtua sana ukichukulia miongoni mwetu tumekuwa tukilipa kodi ya majengo, hii inatufanya tusite kuendelea kulipa kodi kwa sababu hatutakiwi tena katika eneo hili, alisema mmoja wananchi hao.
Kwa upande wake Kayombo alisema tangazo hilo ni halali na ni agizo la Mkuu wa Mkoa la kuzitaka Manispaa zote za jiji hilo kuhakikisha zinawaondoa watu wote wanaoishi katika maeneo hatarishi ya mabondeni, ili kuwaepusha na majanga kama yaliyotokea Jangwani Wilaya ya Kinondoni mwishoni mwa mwaka jana
CHANZO: GUMZO LA JIJI