Watu 3000 kuhamishwa Mbagala

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
[h=3]WAKAZI zaidi ya 3,000 wa Bugudadi, Mbagala katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wako mbioni kuondolewa kwenye maeneo wanayoishi mabondeni ili kupisha uhakiki na tathimini ya nyumba zao.[/h]Tayari nyumba zao ziwekewa alama ya ‘X’ huku kukiwa hakuna taarifa za kutosha kutoka kwa viongozi kuhusu hatua hiyo.
Hayo yalibainika jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa Diwani wa Mbagala, Agrey Kayombo na wananchi.
Wananchi hao walifikisha kilio chao kwa diwani kuwa wamekumbwa na wasiwasi baada ya nyumba zao kuwekwa alama hiyo huku kukiwa hakuna taarifa za kujitosheleza kutoka kwa viongozi wa wilaya yao.

“Hii hali imetushtua sana ukichukulia miongoni mwetu tumekuwa tukilipa kodi ya majengo, hii inatufanya tusite kuendelea kulipa kodi kwa sababu hatutakiwi tena katika eneo hili,” alisema mmoja wananchi hao.
Kwa upande wake Kayombo alisema tangazo hilo ni halali na ni agizo la Mkuu wa Mkoa la kuzitaka Manispaa zote za jiji hilo kuhakikisha zinawaondoa watu wote wanaoishi katika maeneo hatarishi ya mabondeni, ili kuwaepusha na majanga kama yaliyotokea Jangwani Wilaya ya Kinondoni mwishoni mwa mwaka jana

CHANZO: GUMZO LA JIJI
 
Serikali legelege hii...ramani za miji wanazo halafu hazifuatiliwi mpaka watu wajenge ndio wanakurupuka...
 
wakazi zaidi ya 3,000 wa bugudadi, mbagala katika manispaa ya temeke jijini dar es salaam wako mbioni kuondolewa kwenye maeneo wanayoishi mabondeni ili kupisha uhakiki na tathimini ya nyumba zao.

tayari nyumba zao ziwekewa alama ya ‘x’ huku kukiwa hakuna taarifa za kutosha kutoka kwa viongozi kuhusu hatua hiyo.
Hayo yalibainika jana jijini dar es salaam, katika mkutano wa diwani wa mbagala, agrey kayombo na wananchi.
Wananchi hao walifikisha kilio chao kwa diwani kuwa wamekumbwa na wasiwasi baada ya nyumba zao kuwekwa alama hiyo huku kukiwa hakuna taarifa za kujitosheleza kutoka kwa viongozi wa wilaya yao.

“hii hali imetushtua sana ukichukulia miongoni mwetu tumekuwa tukilipa kodi ya majengo, hii inatufanya tusite kuendelea kulipa kodi kwa sababu hatutakiwi tena katika eneo hili,” alisema mmoja wananchi hao.
Kwa upande wake kayombo alisema tangazo hilo ni halali na ni agizo la mkuu wa mkoa la kuzitaka manispaa zote za jiji hilo kuhakikisha zinawaondoa watu wote wanaoishi katika maeneo hatarishi ya mabondeni, ili kuwaepusha na majanga kama yaliyotokea jangwani wilaya ya kinondoni mwishoni mwa mwaka jana

chanzo: gumzo la jiji

wao ndio wanaiweka ccm madarakani, wacha iwafundishe kufikiri, jawabu wanalo wao
 
Mh kujenga dar ni kujitafutia maradhi ya moyo,mh.sjui mikoani hali iko ivi ivi
 
Kwa hiyo chadema wakitawala wataachwa wajenge mabondeni?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Hapana, wawaondoe kwa kuwalipa stahili yao. Historia inaonyesha serikali ya CCM imekuwa ikiwalalia wananchi. Wasijenge mabondeni waondoe basi kwa staha,, utu na heshima, Mwambani Tang mradi wa bandari extension, watu walionewa sana mpaka leo wanalia with negligible compensation
 
wawalipe kwa lipi? yani mtu kavunja sheria halafu tena ukamlipe? kuwaondoa kwa staha kivipi zaidi ya hivyo wameshaaambiwa wahame na nyumba zimeshawekwa X sasa staha gani zaidi ya hiyo tena? Piga tu tinga tinga kesho watafikiria mara mbili kujenga pasiporuhusiwa!

Rafiki hizi sehemu zilikuwa wazi tangu zamani bila mamlaka yoyote. They wwere open to everybody to acquire. Ziliumbwa na Mungu kabla ya mwanadamu kuziwekea sheria, Walipoingia hawa hapakuwa na sheria ya kuwazuia kuwa pale, hivyo ukiwaingilia uwalipe.
 
Yaani apo ndo huwa nachoka ivi hao watu ambao mnawaondoa mabondeni na izi mvua ambazo kila kukicha zazidi kupunguankwa uchafuzi wa mazingira mtawalipa fedha sahikimkweli ili ukonwaendako wakajenge nyumba nasio kukaa kwenye mahema au kutelekezwa!
 
Rafiki hizi sehemu zilikuwa wazi tangu zamani bila mamlaka yoyote. They wwere open to everybody to acquire. Ziliumbwa na Mungu kabla ya mwanadamu kuziwekea sheria, Walipoingia hawa hapakuwa na sheria ya kuwazuia kuwa pale, hivyo ukiwaingilia uwalipe.

Duh! Ugumu wa maisha uko hapo sasa! manake mafuriko yakija na kuwasomba tunarudi kulalamikia mamlaka haijali watu wake!
 
Kwa upande wake Kayombo alisema tangazo hilo ni halali na ni agizo la Mkuu wa Mkoa la kuzitaka Manispaa zote za jiji hilo kuhakikisha zinawaondoa watu wote wanaoishi katika maeneo hatarishi ya mabondeni, ili kuwaepusha na majanga kama yaliyotokea Jangwani Wilaya ya Kinondoni mwishoni mwa mwaka jana

CHANZO: GUMZO LA JIJI

As if the only solution ni kuvunja nyumba ... Kwa nini wasitumie hizo nguvu & hiyo pesa kusafisha hayo mabonde maji yapite? Mto Msimbaze au Mto Mbezi ukusafishwa na kujengewa kuta vizuri tutasahau mafuriko.
 
wawalipe kwa lipi? yani mtu kavunja sheria halafu tena ukamlipe? kuwaondoa kwa staha kivipi zaidi ya hivyo wameshaaambiwa wahame na nyumba zimeshawekwa X sasa staha gani zaidi ya hiyo tena? Piga tu tinga tinga kesho watafikiria mara mbili kujenga pasiporuhusiwa!

daaah,haya kapten
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom