Maneno ya Naibu Waziri Pinda Yataka Kumliza Diwani wa Kisaki Singida

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

MANENO YA NAIBU WAZIRI PINDA YATAKA KUMLIZA DIWANI WA KISAKI SINGIDA

Maneno ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Geophrey Pinda wakati wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kisaki na Mwekezaji wa Sekta ya Nyuki katika eneo la Kisaki B Manispaa ya Singida mkoani Singida nusra yamlize Diwani wa Kata ya Kisaki Moses Shaban kutokana na kujaa hekima na busara.

Naibu Waziri Pinda alifika kijiji cha Kisaki kilichopo mpakani mwa manispaa ya Singida na na wilaya ya Ikungi mkoani Singida tarehe 11 Desemba 2023 kwa lengo la kusikiliza na kutatua mgogoro wa ardhi baina ya Wananchi na Mwekezaji wa Nyuki.

"Nikupongeze sana Mhe Naibu Waziri naweza kusema hata kama hutujafika mwisho wa jambo hili, umenipa hadidu za rejea kumkumbuka Mizengo Pinda alipokuwa waziri mkuu hekima yake na maelekezo yake juu ya utendaji kazi". Alisema Shaban

"Nilikuwa nimesimama na kukusikiliza natamani kulia kwa sababu umekuja katika mgogoro huu hakika umeiwakilisha vyema serikali ". Alisema

Diwani huyo wa Kata ya Kisaki amesema, maneno yaliyozungumzwa na Naibu Waziri Mhe Geophrey Pinda kuhusu utatuzi wa mgogoro baina ya wananchi na Mwekezaji ni tunu yenye afya na mbolea katika kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.

"Umeongoza kikao kilaini na kitamu hata aliyekuwa na hasira zimepotea na hata yule aliyekuwa na silaha ameshusha nakupongeza sana". Aliongeza Diwani Shaban

Kwa upande wake, Naibu waziri wa ardhi Geophrey Pinda aliwataka wananchi wa kisaki katika manispaa ya Singida mkoa wa Singida kuhakikisha wanadumisha amani katika muda wote wa kushughulikia migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.

"Niwatangazie kipande cha amani wote bila kujali ukoo wa nani na muwe na lugha moja iliyo bora. Siri ya mgongano inapata adui anayeingia bila matatizo"alisema mhe. Pinda.

Amewata wananchi wa kijiji cha Kisaki kwenda kuanza vikao vya suluhu ya mgogoro wao na suala la kukutana na serikali basi ofisi ya mkuu wa wilaya ya Singida italisimamia kwa kuwa suala hilo lishatoka katika ngazi ya kijiji.
 
Attachments

  • GBIkmIKXgAAc4zC.jpg
    GBIkmIKXgAAc4zC.jpg
    171.8 KB · Views: 3

Ukiweka clip
 
Habari imeandikwa kiboya sana hii, sasa kama mtu anaisoma kwa mara ya kwanza ataelewa nini? Inaeleza mgogoro wa ardhi na muwekezaji, for how deep? Muwekezaji na wanakijiji nani kavamiwa. Kwa maoni yangu huyo muwekezaji ndiye mvamizi, kaweka mradi wake kwenye ardhi ya kijiji. Huko nyuma kulikuwa hakuna mradi wa nyuki hapo. Huyo muwekezaji kajipatia mahekari ya ardhi kijiji hakitaweza kupanuka kuelekea magharibi mpaka mtamaa na unyanga muwekezaji atafika mpaka huko.
 
Back
Top Bottom