Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) yapeleka kliniki maalum Mbagala

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Wilaya ya Epiphany inatarajia kuendesha kliniki maalum (MOI Mobile clinic) kwa wa kazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam.

Kliniki hiyo itahusisha huduma za kibingwa na kibobezi za mifupa, Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu.
Moi.jpg

MOI imeanzisha Kliniki ili kutekeleza agizo la Serikali ya awamu ya Sita kupitia Wizara ya Afya la kuhakikisha huduma za kibingwa zinasogezwa karibu na wananchi.

Daktari bingwa wa Mifupa MOI, Dkt. Bryson Mcharo amesema anatarajia mwitikio mkubwa hivyo anawasihi wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kupata Matibabu katika kliniki hiyo watakaposikia matangazo.

“Tunawasogezea Wananchi huduma katika Hospitali ya Epiphany kwani tunatoa huduma kwa wakazi wa Dar es Salaam kupitia kliniki yetu pendwa ‘MOI Mobile Clinic’ kwani Wananchi wanahitaji sana huduma za kibingwa na kibobezi,” amesema Dkt. Mcharo.
 
Back
Top Bottom